Na Amina Athumani
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Safari Lager imetangaza kutoa sh. milioni 2.5 kwa mshindi atakayeibuka katika fainali za mashindano ya Pool ya
vyuo vikuu, zitakazofanyika Jun 4 mwaka huu mjini Dodoma.
Mshindi wa pili katika fainali hizo ataondoka na sh. milioni 1.5, wa tatu sh. milioni 1.3, wa nne sh. milioni moja na wa tano hadi wa nane wataondoka na sh. 300,000 kila mmoja.
Katika washindi wa mchezaji mmoja mmoja wa kwanza ataondoka na sh. 300,000, wa pili 200,000 wa tatu sh 150,000 na wa nne sh. 100,000.
Akizungumza Dar es Salaam jana, wakati wa kutangaza vyuo vinane vilivyoingia katika fainali hizo Meneja wa bia ya Safari, Oscar Shelukindo alisema vyuo vinane viliingia katika fainali hizo ngazi ya taifa, baada ya kuwa mabingwa katika mikoa.
Alivitaji vyuo hivyo kuwa ni Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) cha Dar es Salaam, St John University Dodoma, Sokoine University Morogoro, St Agustino University Mwanza, Ruaha University Iringa
Vingine ni Mbeya Istitute of Technology, Stefano Moshi Memorial University Collage Kilimanjaro, Tumaini University na Arusha Institute of Accountancy.
No comments:
Post a Comment