16 June 2011

Safari ya Hiddink kutua Chelsea yaiva

LONDON, England

SUALA la kocha, Guus Hiddink kutua Chelsea limepiga hatua nyingine tena baada ya Rais wa Shitrikisho la Soka la Uturuki, Mahmut Ozgener kuthibitisha kuwa atabwaga
manyanga mwishoni mwa mwezi huu.

Ozgener ndiye aliyemshawishi Hiddink kuwa Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Uturuki Februari mwaka jana, licha ya kupingwa na wengi ndani ya shirikisho hilo.

Na vilevile Ozgener, ndiye aliyekuwa akimuunga mkono Mdachi huyo hata timu ilipokuwa ikiboronga na Hiddink ameshaweka wazi kuwa kuendelea na kibarua hicho, amekuwa akilindwa na rais huyo.

Chelsea inatarajia kumpa nafasi kocha huyo mwishoni mwa wiki hii, baada ya kuamua kumpa muda wa kujiandaa kabla ya kuanza mazoezi ya kujiwinda na msimu ujao yaliyopangwa kuanza Julai 4 mwaka huu.

Lakini kwa sasa inaonekna kuwa huenda zikiwa wiki nyingine mbili, kabla ya kuruhusiwa kuondoka kwenye mkataba wake na Uturuki.

Hiddink (64), ambaye amewahi kuwa kocha wa muda wakati alipoifundisha Blues mwaka  2009, tayari ameshasema hatakuwa na matumizi makubwa wakati atakapowasili katika klabu hiyo ya Stamford Bridge.

Hata hivyo Mkurugenzi Mkuu wa klabu hiyo, Ron Gourlay amesema kuwa tayari wanao wachezaji wa kutosha na kikosi hicho cha sasa hakitakuwa tofauti na cha msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment