*Ni kwa madai ya kukiuka amri halali
Na Said Njuki Arusha
JAJI wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha, Kakusulo Sambo, ameamuru kukamatwa kwa Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania, (ACT)
Dkt. Valentino Mokiwa, na Askofu Stanley Hotay wa Kanisa hilo aliyesimikwa juzi, kwa madai ya kukiuka amri ya mahakama.
Maaskofu hao wanadaiwa kukiuka amri ya mahakama iliyotolewa Ijumaa wiki iliyopita iliyositisha kusimikwa kwa Askofu Hotay baada ya waumini watatu wa Kanisa hilo kutoka Parish ya Mtakatifu James kufungua kesi wakipinga kuweka wakfu kwa kiongozi huyo wa kiroho.
Hata hivyo baada ya mahakama kukubali ombi la waumini hao na kusitisha shughuli za kuwekwa wakfu kwa Askofu huyo huku wageni mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wakiwa wamewasili mjini hapa kwa kazi hiyo, Dkt. Mokiwa alimsimika Hotay kuwa Askofu wa ACT badala ya kuwa Askofu wa Dayosisi ya Mount Kilimanjaro hadi hapo kesi hiyo itakapotolewa uamuzi.
Akitumia dakika 30 kutoa uamuzi huo baada ya kusikiliza ushauri kutoka pande zote mbili, Jaji Sambo alisema viongozi hao wakamawte haraka kwa kuwa wamekiuka amri ya mahakama.
Awali mawakili wa pande zote mbili, Bw. Meinrad D’souza wa upande wa walalamika na Bw. Joseph Tadayo naBw. Issa Rajabu upande wa utetezi, walitopa hoja mbalimbali kila upande ukitetea mteja wake kuwa ana haki.
“Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Dkt. Valentino Mokiwa, na anayeitwa sasa Askofu Stanley Hotay, wakamatwe mara moja kwa kukiuka amri ya mahakama na itekelezwe mara moja”alisema jaji Sambo.
Katika kesi hizo moja ya madai namba 18/2011 na ya jinai namba 48/2011 zilifunguliwa dhidi ya Wadhamini wa Kanisa hilo na Askofu Mteule wa Dayosisi hiyo, Hotay na Bw. Lothi Oilevo, Bw. Godfrey Mhone na Bw. Frank Jackob, pamoja na mambo mengine waliiomba Mahakama kuzuia kusimikwa kwa Askofu huyo kwa madai ya kudanganya umri.
Akinukuu vifungu mbalimbali vya sheria, Jaji Sambo alisema Askofu Mokiwa na Hotay walichokifanya kwa yeyote ni ukiukaji wa amri ya mahakama.
“Nimeridhika kuwa amri halali ya mahakama imekiukwa na ieleweke bayana kuwa nchi hii inatawaliwa na Utawala wa Sheria na hilo limekuwa likisisitizwa mara kwa mara na Rais wetu (Jakaya Kikwete) na viongozi wengine wa juu," alisisitiza Jaji Sambo katika uamuzi wake na kuongeza.
“Nashangaa kuona viongozi wakuu wa dini ndio wa kwanza kukiuka amri halali za mahakama…huku ni kuingilia mahakama chombo huru, mtu yeyote bila kuhitaji mwenye PHD, aliyesoma vyuoo vikuu kama UDSM, Arusha University au Tumaini anayefuata sheria za nchi analizimika kufuata utaratibu wa kuheshimu sheria…Mokiwa na Hotay walichokifanya kwa vyovyote ni kukiuka amri ya mahakama, ninafahamu na wasomi wanafahamu maana ya Order namba 37 rule (2) kwani ipo wazi katika kuwashughulikia wanaokiuka amri za mahakama,” alisisitiza.
Alisema kitendo cha viongozi hao kwenda kinyume na amri ya mahaka ni hatari kwa utawala wa sheria na kwamba ni wajibu wake kutumia vifungu kadha wa kadha kama kifungu cha 114 (i) c, k pamoja na (iii) pamoja na kifungu namba 124 vinavyoipa mahakama uwezo wa kuwaadhibu wanaokiuka amri ya mahakama.
Awali, Jaji Sambo alisema walalamikaji waliwasilisha ombi kwa mahakama kuzuia sherehe hizo kimya kimya lakini kwa busara mahakama hiyo iliamua kuita upande mwingine ambao nao ulitoa pingamizi.
Alisema kutokana na pande zote mbili kuvutana mahakama iliamuaa kusitisha shereeh hizo hadi jana jumatatu itakapotoa uamuzi lakini jitihada hizo za mahakama hazikuheshimiwa badala yake waliendelea na kumsimika Mchungaji huyo kuwa Askofu wa ACT.
Alisema ni vigumu kutoa maamuzi kwa kuwa kitendo cha kusimikwa kwa Askofu huyo ni sawa na mwenendo mzima wa mashauri hayo kumevamiwa na kukosa nguvu.
Jaji huyo alisema wadai katika madai yao walieleza kuwa Katiba ya Kanisa hilo inaelekeza kuwa mgombea wa kiti hicho anatakiwa kuwa na umri kati ya miaka 40 na 60 ambapo Askofu huyo alidaiwa kuwa mwaka jana alitimiza miaka 38.
Sanjari na hilo Jaji huyo alisema wadai hao waliiomba Mahakama hiyo itoe tamko kuwa Askofu Mteule huyo amedanganya katika cheti chake cha kuzaliwa na kwamba nyaraka hiyo ilitolewa kwa njia ya udanganyifu.
Pia alisema walidai Askofu Hotay alitoa taarifa za uongo kwa msajili wa Vizazi na Vifo (RITA) akieleza kuwa alizaliwa 1969 huku Mkuu wa Shule ya Sekondari Ilboru alikosoma akidai alizaliwa mwaka 1972.
Awali Wakili D’souza aliileza mahakama hiyo kuwa amri iliotolewa na Mahakama haikutekelezwa hivyo sherehe za kumsimika Uaskofu Hotay zilishafanyika Jumapili iliyopita jambo ambalo ni kukiuka amri halali ya mahakama.
Kutokana na hali hiyo aliiomba mahakama kuchukua hatua kwa kuwa amri hali imekiukwa na kwamba kuna ushahidi wa kutosha juu ya hilo na kuongeza kuwa kwa mujibu wa Katiba ya ACT Askofu wa Dayosisi anapaswa kutoka ndnai ya eneo husika.
Akijibu hoja hizo, Wakili Tadayo wa upande wa utetezi alisema kilichofanyika ni kumsimika Uaskofu wa Kanisa hilo Tanzania na si Askofu wa Dayosisi hiyo na kwamba kitendo cha kumsimika uaskofu hakina maana kuwa ndiyo Askofu wa Dayosisi hiyo.
Alisema hatu hiyo haizuii mahakamakuendelea kusoma maamuzi yake juu ya maombi ya walalamikaji kwa kuwa hajawekwa wakfu kuwa Askofu wa Dayoyo iliyopingwa.
Askofu Mokiwa amekuwa akitetea umuhimu wa Askofu Mkuu wa ACT kuwa na Mamlaka ya kumsimika Mcngunjaji yeyote mwenye sifa zinaotakiwa kuwa Askofu bila kuwa na Dayosisi au kuhamisha askofu kutoka Dayoyosisi yoyote na kuachana na kasumba ya miaka mingi kuwa askfu lazima awem mwenyeji wa Dayosisi husika jambo ambalo halina maslahi kwa maendeleo ya kiroho.
Kanisa la Mtakatifu James imekuwa na mgogoro wa muda mrefu wa Askofu wake aliyekwepo huku mwako wa kiroho ukitajwa kuwa ni moja ya chanzo cha mgogoro huo huku upande mmoja ukitaka kufutwa kwa taratibu za kanisa na wa pili ukitaka mwamko mpya wa kiroho.
ndg zangu,mambo ya Utumishi wapi na wapi na mahakamani kama kanuni za kanisa zimekiukwa,hakuna mabalaza ya usuluhishi na kazi ya Mungu na Umri cyo hoja ya Msingi hiyo kanuni muibadilishe,nabii Yeremia aliitwa kuwa nabii(aliongea na Mungu) akiwa na umri wa miaka 17 tu....
ReplyDelete“Nimeridhika kuwa amri halali ya mahakama imekiukwa na ieleweke bayana kuwa nchi hii inatawaliwa na Utawala wa Sheria na hilo limekuwa likisisitizwa mara kwa mara na Rais wetu (Jakaya Kikwete) na viongozi wengine wa juu," alisisitiza Jaji Sambo katika uamuzi wake na kuongeza.
ReplyDeletehuyu JAJI NI KADA MWINGINE WA CCM ambaye anatekeleza amri ya kikwete ya kuwasumbua watu wanaotafakari wakiwa wima.......
wanataka kumfanya kama wanavyowafanya kina mbowe, zitto, tundu lissu sakaya na wengine...
haya ni matumizi mabaya ya mahakama zetu...
huo moto si mdogo, hilo ni sikio la kufa haliwezi kusikia dawa .....
Serikali ya Tanzania haina Dini, sasa iweje leo Mahakama ambacho ni chombo cha serikali kinaingilia mambo ya dini. Serikali yetu ni ya kikafiri. Kafiri na mambo ya mungu wapi na wapi. Mambo ya dini yatatuliwe na wenye dini sasa kafiri atakuwaje tena msuluhishi kwenye mambo ya Mungu?
ReplyDeleteWanaopinga kuaskofishwa kwa huyo askofu mpya wana busara lakini hawana hekima!! Na moto aliouwasha huyo jaji hataweza kuuzima - imani ya dini ina nguvu kuliko mvuto wa siasa, asilete mchezo hapa! Arudi Kanisani/Msikitini ili apewe hekima ya kuihandle hii kesi
ReplyDeletewamezoea kama mkapa alivyowaua waislam mwembe chai, ole wao yupo hakimu wa mahakimu .tizama mungu muumba alivyomuumbua mkapa kwenye mgodi wa kiwira kwanza mtu mwenyewe hana hata mtoto.damu za waislam wa mwembe chai zitakusumua sana lanakum wewe pamoja na serikali hii ya kikafiri na mfumo kristo.haya mkamateni huyo mkiristo tuone kama kweli kuna utawala wa sheria.
ReplyDelete