03 June 2011

Babu asitisha huduma Jumapili

Na Said Njuki, Arusha

MCHUNGAJI Ambilikile Masapila ‘Babu’ wa Kijiji cha Samunge, Loliondo mkoani hapa, amesitisha utoaji dawa Jumapili kuanzia sasa kwa lengo la kufanya
ibada zaidi ili Mwenyezi Mungu amfunulie uwezo zaidi wa kuponya magonjwa sugu na kupata mapumziko baada kutoa tiba hiyo kwa muda mrefu.

Wakati Babu akitoa angalizo hilo, serikali mkoani hapa imetoa onyo dhidi ya matapeli wanaouza vibali bandia vya kuyaruhusu magari kwenda Samunge kupeleka wagonjwa kupata kikombe cha Babu wakati vibali hivyo hutolewa bure.

Msaidizi wa Babu, Bw. Frederick Nisajile alisema kuwa mchungaji huyo kwa kupata muda zaidi wa kufanya ibada siku hiyo pamoja na mapumziko ya kutosha ni wazi atafanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.

Tangu Babu aanze kutoa tiba hiyo iliyowavuta wagonjwa wengi kutoka ndani na nje ya nchi kwa zaidi ya miezi nane sasa, huku akitoa kikombe kwa wagonjwa zaidi 2,000 kwa siku hajawahi mkupata mapunziko ya kutosha kwani hata siku ya Jumapili amekuwa
akiendela na tiba baada ya kutoka kanisani.

“Kama binadamu kufanya kazi nzito kama hiyo kwa muda mrefu bila kupumzika ... kwa miezi hiyo anastahili kupumzika na kuwasiliana na Mungu wake kwa utulivu zaidi hasa siku za Jumapili..lakini wagonjwa wasihofu tiba itakuwepo kama kawaida,” alisema.

Akizungumzia idadi ya wagonjwa wanaoingia kijijini hapo, kupitia vituo mbalimbali alisema wanapata kikombe bila bughudha yoyote na kurudi makwao ndani ya siku moja kutokana na kutekelezwa kwa taratibu kadhaa zilizowekwa na serikali.

Ofisa Habari Ofisi ya Mkoa wa Arusha, Bw. Yotham Ndembeka kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Isidore Shirima kuwa imegundulika kuwepo kwa matapeli wanaouza vibali na kuwataka wananchi kujihadhari nao.

Alisema vipo vibali bandia vilivyozagaa Arusha na vinauzwa (hajataja bei) kwa wagonjwa wanaoelekea kwa babu, serikali imelitambua hilo na inalifanyika kazi suala hilo kikamilifu kwani mamlaka husika zimeshaanza kazi.

Kuhusu kusitishwa kwa tiba siku ya Jumapili, alisema kwa wiki serikali itatoa vibali vya kuondoa hadi siku ya Ijumaa ili wagonjwa wapate tiba siku ya Jumamosi na kurudi na hakuna kibali kitakachotoka Jumamosi.

Aliwataka madereva wanaosafirisha wagonjwa kuendesha ma gari yao kwa mwendo wa wastani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika kwani baada ya serikali kufanya ukarabati wa barabara ya kuelekea kijijini Samunge na kuwa nzuri baada ya
ukarabati madereva hao wamekuwa wakienda mwendo wa kasi.

12 comments:

  1. WAJINGA NDIO WALIWAO HIKWELI KATIKA KARNE HII MTU ANAKUAMBIA ANA MAWASILIANO NA MUNGU NA WEWE UNAKUBALI? KWELI TZ NCHI YA WAPUMBAVU

    ReplyDelete
  2. Huyo BABU ni mwehu na mwendawazimu kabisa!!
    Tangu lini Mungu akawa na uhusiano na waganga wa kienyeji??????

    ReplyDelete
  3. Mtoa swali hapo juu! Unamaanisha nini ukisema waganga wa kienyeji? Je mtu akitaka kupumzika kwa imani yake ili awe na sala au dua na Mungu wake kuna jambo gali la kumwita mwendawazimu! Hivi kweli watu wote wanaokwenda kupata matibabu kwa Mchungaji huyu hawana akili na niwewe tu wenye akili? Je kweli Watanzania wote niwapumbavu kama mtoa maoni awaitavyo? Kama yeye si M-TZ hana ajualo juu ya WA-TZ na kama yeye ni M-TZ basi ni mmoja wao aliwatukana na kuwaita wapumbavu.

    ReplyDelete
  4. Wengi wamekunyuwa kikombe, wengi wamepona maradhi yao. uwendawazimu wa babu uko wapi hapo?
    Imekuwa sasa kawaida ya baadhi ya watanzania kusagia wengine wanapoona wengine wanafanya mambo mema.Waache wenye kuamini wapate kikombe.

    ReplyDelete
  5. uwongo mtu idont belive this

    ReplyDelete
  6. jamani hizi ni nyakati za mwisho ambazo ni ngumu kushuhulika nazo tumeonywa kimbele na neno la Mungu kwamba wengi watakuja kwa jina lake na kusema Mungu yupo hapa yupo pale wote ni manabii wa uongo na kama kweli alitumwa na mungu kwanini dawa hiyo ni lazima aitoe kwa mkono wake tu??tena haifai kubeba? hata wa masai wanatibu kwa miti shamba lakini unapewa maelekezo ya matumizi ya dawa unamtengenezea mgonjwa wako nyumbani kwani yeye anafanya kunyume???

    ReplyDelete
  7. jamani, watanzania tunatakiwa kumshukuru mungu kwa kututumia babu aponye magojwa ya aina yote...huyo ni masiah ameelekezwa na mungu sijui watu wanatatizo gani kama wewe huamini kuponywa sizani kama unaamini kwamba mungu yupo.. hunahaki yoyote kusaliti babu... mwache aendelee kutibu wagojwa wapone..na huyo anaye sema mwendaazimu basi yeye mwenyewe ni mwendaazimu na anamashetani... mkome kabisa kuharibu jina la babu....

    ReplyDelete
  8. kutuita wapumbavu kwa chuki za kidini haikuongezei kitu. tunajua mnakwenda kimya kimya na mnakunywa kikomba, ila hamtaki kukiri hadharani kwamba uponyaji umekuja kupitia mchungaji. mlitaka awe nani???

    ReplyDelete
  9. poleni sana. Ombeni Mungu awafulie yaliyo ya sirini kwa kufunga na kuomba na kulisoma na kulitafakari neno la Mungu bila kukoma Mungu atawaonyesha maana ni ahadi yake. Msilumbane. Mungu awabariki na kuwafungua macho ya rohoni.

    ReplyDelete
  10. Naafiki kama mzee wa baraza aliyetoka usingizini.

    ReplyDelete
  11. hata india kuna kutibu athma kwa kumeza samaki mbichi mara mbili kwa mwaka then unapona,nae alioteshwa na mungu wao. na watu wanafoleni wanapona,huwezi jua imani ya mtu na mungu wake!imani inaponya.kama hujapata tatizo la gonjwa sugu huwezi jua,acha waliopona watoe ushuhuda,wee safi huwezi amini,yataka moyo!

    ReplyDelete
  12. Ni upuuzi wa hali ya juu kabisa kwa mtu mwenye akili timamu kuamini kuwa mtu kama yule mdingi anauwezo wa kutibu magonjwa yote sugu... kuna mtu ninayemjua aliyepata fursa ya kwenda kwa babu na hakuna kilichotokea zaidi ya kupoteza pesa zake za nauli. hii ni biashara na upumbwazi wa kiakili. huyu mzee ni yesu? au kuna andiko lolote linalosema kuwa kuna mdingi fulani atatokea kuponya watu??? tumieni akili karne nyingine sio zile tulizoziacha nyuma

    ReplyDelete