*Wabunge wahofu ni 'malipo ya Dowans'
Na Tumaini Makene
BAADA ya mjadala mkali wa siku tatu hatimaye wabunge wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini imeikubali bajeti ya wizara hiyo, lakini wakiiwekea
masharti ya kubadilisha baadhi ya mambo kabla haijasomwa bungeni, huku pia tetesi za kuengwa fedha za kulipa Dowans zikiibuka.
Kwa mujibu wa yanzo vyetu vya habari ambavyo viko karibu na kamati hiyo, kulikuwa na mjadala mkali juu ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, ambapo moja ya vitu vilivyoibuka ni juu ya kiasi kikubwa cha fedha kutengwa kwa ajili ya dharura huku miradi halisi ya umeme ikitengewa fedha kidogo.
Imeelezwa kuwa mabilioni hayo yaliyotengwa kwa ajili ya dharura, yaliwashtua baadhi ya wajumbe ambapo wengine walianza kujadili kuwa fedha hizo zinalenga kutumika kuilipa kampuni tata ya Dowans, badala ya kupelekwa katika matumizi ya msingi kama vile miradi ya umeme vijijini.
Chanzo chetu hicho kililiambia Majira kuwa takribani sh. bilioni 115 zimetengwa kwa ajili ya dharura katika wizara hiyo, huku pia wahusika wakiwa hawana majibu juu ya bilioni 49 zilizotengwa kwa ajili ya matumizi ya namna hiyo mwaka wa fedha 2010/211 unaoelekea kuisha siku chache zijazo.
Juhudi za kumpata Waziri William Ngeleja, kuzungumzia masuala hayo ziligonga mwamba baada ya simu yake ya mkononi kutopatikana muda wote aliopigiwa na Majira, huku mwenyekiti wa kamati, Bw. January Makamba akikiri kuwa 'mjadala ulikuwa mkali sana.'
"Unajua wale watu bwana hawajawahi kuwa-scrutinized kiasi kile, yaani hoi kabisa, kwa kweli ulikuwa mjadala mkali siku tatu na jana (juzi) tumemaliza saa 2 usiku. Lakini kimsingi tumekubaliana kuna masuala wamekubali watayafanyia marekebisho.
"Kuna masuala tumewaambia wayafanyie marekebisho kama vile allocation ya matumizi, kuna matumizi si ya lazima sana, tumewaambia wafanye mabadiliko...hasa katika vipaumbele na matumizi, tunataka bajeti iwe ya maendeleo zaidi. Tunataka miradi ya umeme iwe ya mipango zaidi si suala la dharura."
"Sipendi kuwa specific sana bwana, si unajua kuwa bajeti si ya kwangu, bajeti ni ya waziri, ndiye mhusika zaidi wa kuzungumzia specific issues," alisema Bw. Makamba.
Bw. Makamba mbali ya kukiri kuwa wizara hiyo imetenga katika bajeti yake kiasi cha bilioni 115 kwa ajili ya matumizi ya dharura tofauti na mwaka jana ilipotenga bilioni 49, aliongeza "unajua kuna vitu vidogo vidogo vingi hivi mara ukarimu, mara nini, tumewaambia wabadili tunataka rural electrification (umeme vijijini) zaidi.
"Kimsingi ni tumekubaliana, maana tunajua...kama watu wao wenyewe wamesema watafanya, mnawaambia hiki vipi...wanakiri hiki sawa, wame-admitt wao wenyewe, wanakubali hiki watakifanyia kazi," alisema Bw. Makamba, akionekana kuzungumza kwa uangalifu.
HUU PIA NI UTOTO. UNAANZA KUJENGA NYUMBA NYINGINE, WAKATI UNAYOLALA INAVUJA,(HAITOSHELEZI). PIA NYIE WAONGO WATU WA MJINI WENYE ANGALAU UWEZO WA KUJIKIMU WANALALAMIKA UMEME BEI MBAYA SIO KWELI. MJINI BADO UMEME HAUTOSHI NA HAUNA UHAKIKA, HUO WA KIJIJINI UTATOKA WAPI. MNAJUA KABISA CHANZO CHA UMEMME KIMECHOKA BADO MMEKAA TU NA KUYAPA ZABUNI YA KUUZA UMEME MAKAMPUNI YENU YA KINYONYAJI SYMBIOTIC, IPTL AU WA - SONGAS KWA CAPACITY CHARGE, MAFUTA YA KWAKO ANIZIMA ANAVYOTAKA,. MNGETUAMBIA MRADI MPYA WA KUZALISHA UMEME UNAJENGWA KUONDOKANA NA ADHA HII PAMOJA NA KULIKWAMUA TAIFA KIUCHUMI MAANA BILA NISHATI HUNA PA KUTOKEA. HYDRO-POWER HAINA UHAKIKA, UNGELEA JUA, UPEPO MAKAA NA JINSI GANI TUTAFAIDA NA GESI ASILIA, MNAKURUPU KUTAFUTA HISANI ZA WATANZANIA KUMBE NDIO MNAPOTEA KWA KUTOA MANENO MATAMU AMBAYO HAYANA UTEKELEZAJI
ReplyDeleteMimi nadhani kuna mambo mengine yanafanyika makusudi. Haiingii akilini kutenga mihela yote hiyo kwa ajili ya dharura, badala ya kutumia kuhakikisha inafanya kazi ya uhakika yenye guarantee ya miaka toshelevu itakayohakikisha huduma hiyo inapatikana kwa uhakika na siyo kubahatisha. Unaweza kuona kabisa sasa ni wapi serikali ilipokuwa inapotezea fedha zake huku wananchi wakilia na makodi mengi wanayokatwa pasipo tija; kama hivyo sasa, wameshindwa kueleza dharura iliyopita imetumikaje kama haikurudishwa hazina...ni wizi tu!; na hiyo ni wizara moja tu...., unakuja kwenye hayo mashirika ya umma sasa, kama NARCO, ati ng'ombe wa serikali 2800 wamepotea! Halafu mtu yupo kila siku anaingia kazini na hana wasiwasi wowote wala haulizwi chochote, wala hakosi usingizi juu ya hilo, jamani ....ni wizi mtupu!
ReplyDeleteHongera Januari na Kamati yako.
ReplyDeletelakini misimamo yenu isiishie nje ya bunge, ndani ya bunge pia tungependa mfanye mnayofanya sasa ili kuongeza uwajibikaji wa serikali
We unayetoa hongera hebu tufafanulie hongera kwa lipi la maana alilolifanya January.Kweli Tanzania kuna kazi kubwa inahitajika kuwaamsha waliolala.
ReplyDeletejamani mwaka huu iko kazi!!!! miaka yoooote hizi kamati zilikuwepo bungeni lakini hazikuwa machachari kama mwaka huu, tutake tusipotaka kwa namna fulani kambi ya upinzani imeamsha kitu, angalao kwa kiasi fulani kambi ya ufisadi itaingiwa woga hata kama ufisadi hautakwisha lakini wapate kazi ya kutafuta mbinu mpya.
ReplyDelete