*Hati ya kukamatwa Slaa, Ndesamburo yafutwa
Na Said Njuki, Arusha
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha imeagiza tena Jeshi la Polisi kumkamata Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Bw. Freeman Mbowe baada ya kushindwa kujisalimisha mahakamani katika kesi inayomkabili.
Akitoa hukumu dhidi ya washtakiwa wengine waliojisalimisha mahakamani baada ya kushindwa kuhudhuria katika mahakamani hapo Mei 27 mwaka huu, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Bw. Charles Magesa alisema kitendo cha mshitakiwa wa kwanza katika shauri hilo kushindwa kujisalimisha labda anataka kukamatwa na polisi.
Mahakama hiyo awali, iliamuru Mwenyekiti huyo pamoja na viongozi wengine akiwemo Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dkt. Willibrod Slaa, wabunge wawili wa chama hicho, Bw. Phillemon Ndesamburo (Moshi Mjini) na Bw. Godbless Lema (Arusha Mjini) wakamatwe na kufikishwa mahakamani hapo baada ya kushindwa kuhudhuria katika kesi inayowakabili ya kufanya kusanyiko lisilo halali Januari 5 mwaka huu.
Washtakiwa wengine ambao mahakama ilitoa hati ya kukamatwa ambao hata hivyo walijisalimisha mahakamani siku mbili baadaye ni pamoja na mchumba wa Dkt. Slaa, Bi. Josephine
Mushumbusi, Bw. Richard Mtui, Bi. Aquiline Chuwa na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Bw. Samson Mwigamba.
Pamoja na washtakiwa na wadhamini wao kutofika mahakamani, hata Mawakili wao, Bw. Method Kimomogolo na Bw. Albert Msando pia hawakuwepo mahakamani wakati hati hiyo inatolewa, lakini
washtakiwa Bw. Joseph Selasini (Mbunge wa Rombo) na Bw. Dadi Igogo pia hawakuwepo mahakamani siku hiyo, na mahakama haikutoa hati ya kuwakamatwe kwa sababu wadhamini wao walikuwapo.
Washtakiwa waliohudhuria mahakamani hapo siku hiyo ni pamoja na Bw. Nai Steven, Bw. Mathias Valerian, Bw. John Materu, Bw. Daniel Titus, Bw. Juma Samuel, Bw. Walter Mushi, Bw. Peter Marua na Bw. Erick Makona.
Hakumu Magesa alisema mshitakiwa wa kwanza (Mbowe) baada ya kutolewa hati ya kumkamata au kujisalimisha mahakamani hakufanya hivyo hadi jana wala mdhamini wake, hivyo Ofisa Inchaji wa Polisi anatakiwa kumkamata kwani ni wajibu wake kutekeleza amri halali ya mahakama ni si vinginevyo.
“Wote walipewa masharti ya kufika mahakamani kama ulivyo utaratibu na iwapo wanapatikana na udhuru wa kibinadamu basi ni wajibu wa wadhamini wao kuhakikisha wanafika mahakamani kueleza kilichowasibu. Kimsingi si sahihi kutofika mahakamani bila taarifa, hivyo Ofisa Inchaji amkamate na kufikishwa mahakamani,” alisema.
Bw. Ndesamburu alinusurika kwenye hukumu hiyo baada ya Mdhamini wake, Bw. Reuben Ngowi kuibuka mahakamani hapo na kutoa udhuru uliomkuta mshtakiwa huyo pamoja na yeye mwenyewe, ambapo Hakimu Magesa alikubaliana naye na kufuta amri hiyo, hivyo kuachiwa huru.
Katika hukumu dhidi ya washitakiwa wengine waliojisalimisha pamoja na wadhamini wao, walipewa onyo kali na kutakiwa kutorudia kosa hilo kwani kufanya hivyo ni kukiuka maagizo halali ya mahakama.
Alisema amepitia hoja za wakili wa upande wa utetezi, na kwa kuzingatia sababu zilizotolewa mahakamani, aliamua kufuta amri hiyo na kuahirisha kesi hiyo hadi Juni 24, mwaka huu.
Mahakama Mnang'ang'ania nini kumkamata Mbowe?
ReplyDeleteKwani si ana Wakili ambaye amefika mahakamani kumwakilisha? Pia si mnajua aliko?
Hivi vikesi vingine jamani visituchukue kimawazo tukasahau mauaji ya polisi kwa raia. SI wangeng'ang'ania kumkata Waziri wa Mambo ya Ndani na IGP kwa kuwaamrisha polisi kuwaua raia? Au wanafikiri wananchi ni wajinga kiasi cha kutojua kuwa polisi wanafanya kazi kwa maelekezo kutoka ngazi za juu ili kulinda ten pasenti zao kutoka kwa wawekezaji?
ReplyDeleteChris John, tofauti kati ya Lissu na Magesa ni ya kisiasa. Magesa anatekeleza matakwa ya watawala wakati Lissu anaangalia zaidi mustakabali wa taifa kwa ujumla wake. Magesa hawatathubutu kwenda kinyuma na JK anavyotaka, vinginevyo atajiweka matatani ndugu yangu. Tumefika mahali sheria imeshikwa na CCM na vibaraka wake kwa maslahi ya watawala ili waendelee kutunyanyasa, kutudhalilisha, kutunyonya, kutuonea kadri wapendavyo.
ReplyDeleteIKO SIKU - YA MISRI, TUNISIA,na sasa LIBYA hayakuja kwa bahati mbaya. Wananchi walichoka na udhalimu wa watawala.
Washenzi nyie msio na akili hata hamjiulizi ungekuwa wewe mlalahoi umekaidi amri ya mahakama ingekuwaje. na upumbavu wenu mtaendelea hivyohivyo. Huo ni udhaifu wa sheria za nchi kwani zinabagua. watoto wa wakubwa wansababisha ajali kama ile ya mtoto wa Lowassa mmewahi kuisikia tena? Mtoto wa Mtei alikamatwa kwa wizi wa magari kule Babati mlisikia kinachoendelea? endeleeni na ujinga wenu huo mtapandwa na wanasiasa mpaka kwenye mikundu yenu,wapumbavu wakubwa
ReplyDeleteAnonymous wa 4:40, sikulaumu hata kidogo kwa matusi hapa kwenye blog hii. NI malezi uliyopewa na wazazi wako.
ReplyDeleteHakuna kitabu cho chote cha sheria nchini kilichoandikwa "sheria hii ipindishwe kwa mtawala, vigogo na watoto wao ili isomeke kuwapendelea". Kinachofanyika ndugu yangu ni hao watekelezaji na watafsiri wa sheria zenyewe kuzipindisha kwa sababu wanazojua wenyewe.
Wewe ni mmoja wao wa hao ambao ungekalia kiti hicho cha hukumu ungepindisha kwa sababu ya utumwa wako wa mawazo; njaa zako; na utumwa wa kiakili. POLE lakini watu makini wanaendelea na mapambano hadi kieleweke.
Mimi nadhani mara nyingine Siasa zinachangia sana kufuta Haki! Hawa akina Magesa wamesahau kuwa MAHAKAMA, BUNGE NA SERIKALI haviingiliani? wanajifanya wamesoma Katiba na sheria za nchi lakini siasa zinawadanganya wanasahau professionalism?
ReplyDeleteTunapofikia mahali hakimu tuu anakwenda kuamuru mbunge akatolewe kwenye shughuli za Bunge,eti hakuiheshimu mahakama TUMEKWISHA!
Kama tumefikia Hakimu kuamuru mbunge akakamatwe akiwa kwenye shughuli za Bunge, tutarajie hata siku moja ataamuru Rais atakayekuwa wa chama kingine akamatwe bila kujua kuna sheria inamlinda na udhalilishaji huo!Tafadhali Magesa soma Sheria za nchi hii uzielewe usije ukajikuta humtumikii kafiri bali unajichimbia shimo la kuingia mwenyewe!
ReplyDeletehakuna cha kueleweka hapo mtaona aibu siku sinyingi mnajifanya mnajua sana sheria mboe hayupo juu ya sheria nguvu ya uma mbona hationi?msijidanganye watu wachache hamuwezi kutufanya tusivute hewa kwa tamaa ya madaraka ngojeeni mwaka 2085 mtapewa nchi si kwa sasa jeuri uwezo wala akili ya kuwashawishi wabongo hamna kelele nyingi barua mabog yote mboe mboe nini sasa simuandamane?mnashindiwa nn?kukaa kimya kwa watu wenye akili sio kushinda kwenu watu wanawaangalia tu na kuwaona mnavyochukua muda wenu mwingi kufikiria mambo ya utawala watamsaidia nani sasa?chuki majigambo ubabe mwingi usio na mana juzi kwenye viwanja vya bunge dar alisema mbele yenu nyie washabiki waandishi kuwa hawezi kupigia magoti polisi yupo tayari kuwawa kilicho mpeleka jana kwa miguu yake na marando central polisi ni kitu gani?yeye si mbabe?angeacha tu kingemkuta kingine na arusha cha kukokotwa kama mwenzie lisu midomo tu mirefu ya nn hatuhitaji majigombo na majivuno ya mtu
ReplyDeletewatanzania lzm tuelewe ukweli mboe sawa kashindwa kufika mahakamani ndesamburo alikuwepo?sialienda mdhamini wake?mboe alishindiwa nn mdhamini wake kwenda mahakamani kutoa udhuru wa mboe msijifanye mnajua sana na ndiomaana nchi inazidi kuwa masikini kwa kujua kwetu
ReplyDeleteMdhamini wa Mbowe alikwenda siku zote ila siku aliyokosa alikuwa mgonjwa na Hakimu aliridhika na hilo. Magesa ameelekezwa kumkamat ana kumdhalilisha Mbowe, hili halina ubishi. Lakini nguvu ya umma ikiamua kujituma hapo, hakun wa kuizuia. JK aangalie asidhani amesimama na marais wa Misri, Tunisia, Libya,Yemen, walikuwa wamekaa.
ReplyDeleteTANZANIA USILIE!! SAA YA UKOMBOZI YAKO I KARIBU!!
ReplyDeleteHUO USHABIKI UTAWAPELEKA PABAYA TUNASUBILI YA LIBYA YAJE NYIE SI MNA NGOZI YA CHUMA!HATAWEWE UNAYE SHABIKIA SANA UTAKIONA...HAKUNA UBISHI KWAMBA MBOE KAVUNJA SHERIA ACHA SHERIA IFUATWE KWANI YEYE NANI?MNA WAVURUGA WATU WASIO ELEWA KWA KUSHABIKIA VURUGU ZI TAPIGWA NA MSHINDI ATAJULIKANA.
ReplyDeleteKuwasemea watanzania zaidi ya milioni 40 wafuete upuuzi wenu si haki.Serikali ijifunze hii yote ni kwasababu mmebania sana Elimu Watanzania walio wengi Elimu Hakuna hivyo ni rahisi kushawishiwa na kudanganywa lakini Ukweli upo pale pale Hata wao wakishika madaraka watafanya hivyohivyo angalia Zambia,Malawi,Kenya,Ujerumani enzi za hitra.SHERIA NILAZIMA ZIFUATWE POLISI WANATEKELEZA SHERIA ZILIZO TUNGWA NA HAO WABUNGE HAPO NI NINI KISICHOELEWEKA?
ReplyDelete