Na Amina Athumani
UCHAGUZI Mkuu wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BD), unatarajia kufanyika Jun 11 mwaka huu Dar es Salaam.Uchaguzi huo ambao
uliahirishwa mara mbili, umepangwa kufanyika Jun 11 mwaka huu na kutolewa wito kwa wadau wenye sifa ya kuongoza mchezo huo kujitokeza kuchukua fomu za uongozi.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Ufundi wa chama hicho Zabron Manase alisema Kamati ya Utendaji ya BD, ilikaa juzi na kupanga tarehe ya uchaguzi huo baada ya awali kushindikana kufanyika kutokana na chama hicho kubanwa na ratiba ya mashindano.
"Katika kikao cha Kamati ya Utendaji, tumekubaliana uchaguzi huu ufanyike Juni 11 mwaka huu na mahali tutakapofanyia tutapatangaza baadaye, ila cha msingi ni kwamba wadau wanaojiona wana sifa za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wajitokeze kuchukua fomu ,"alisema Manase.
Alisema nafasi zitazowaniwa ni Rais, Makamu wa Rais, Mkurugenzi Mtendaji, Mkurugenzi wa Ufundi, Mkurugenzi wa Makocha, Mkurugenzi wa Shule na Watoto, Wanawake, Tiba, Mipango, Waamuzi na Mhazini.
Manase alisema hadi jana wagombea waliojitokeza kwa ajili ya kuomba uongozi katika chama hicho ni 11.
No comments:
Post a Comment