Na Zahoro Mlanzi
KATIKA kile kinachoonekana timu ya Waydad Casablanca kuipa somo Simba, uongozi wa klabu hiyo umesema haitaki tena kufanya maandalizi ya zima moto na
sasa wanaingia kambini leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuiwinda DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Simba itatupa karata yake nyingine dhidi ya Motema Pembe katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Juni 12, mwaka huu Dar es Salaam baada ya kuondolewa na Wydad kwa kufungwa mabao 3-0 katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Evodius Mtawala alisema kufungwa na Wydad kulitokana na maandalizi ya zima moto, hivyo katika mashindano yanayokuja hawataki yatokee kama hayo.
"Nadhani hata wewe umeshuhudia, tulifanya maandalizi ya zima moto lakini kwa mechi zijazo hatutaki hilo litokee, hivyo kesho (leo) tunaingia kambini hapa hapa Dar es Salaam, wapi itakaa tutawajulisha.
"Tunacheza na Motema Pembe Juni 12 na tunatakiwa tucheze Kombe la Kagame, ambalo linaanza Juni 20, hivyo ukiangalia hatuna muda wa kupoteza na hii kambi ni ya moja kwa moja," alisema.
Wakati huo huo, Motema Pembe inatarajia kuumana na Saint Elloi Lupopo Juni 9, mwaka huu katika mfululizo wa michezo ya Ligi Kuu ya nchini humo.
Kwa mujibu wa taarifa za mtandao wa klabu hiyo, timu hiyo bado haijapata taarifa kutoka kwa chama cha soka nchini humo kama mchezo huo utasogezwa mbele, ili wapate muda wa kujiandaa.
"Kiufundi si jambo zuri kucheza siku hiyo kwani timu nayo inahitaji ipate muda wa kupumzika, kwani kutakuwa na safari ya kwenda Tanzania, hivyo hilo tutaliangalia," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo ikimkariri Kocha Mkuu, Santos Mutubile.
MPIRA SIO SIASA JAMANI.
ReplyDeleteKIWANGO CHETU BADO KINAITAJI MAFUNZO YA UFUNGAJI NA KUZUIA NA UWEZO WA MCHEZAJI MMOJA MMOJA.
SISI MANENO MENGI KAMA GOLIKIPA FULANI ANADAKA SANA LAKINI KWENYE MECHI NDIO HUYO ANAFUNGWA MPAKA UNAONA HURUMA