10 May 2011

Slaa anasa waraka wa siri CCM

*Unaeleza sababu za chama hicho kushuka umaarufu
*Auponda kutozungumzia hali ya maisha ya Watanzania


Na Tumaini Makene

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia (CHADEMA) ameibua madai mapya akisema amenasa waraka wa siri wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao ameuponda
akisema hakuna hata sehemu moja umezungumzia hali ya maisha ya Watanzania na taifa kwa ujumla, huku pia akiibua tuhuma za ufisadi wa bilioni 365 aliodai umefanyika kupitia hazina.

Dkt. Slaa, mwanasiasa ambaye amejijengea umaarufu nchini kwa kulipua masuala mbalimbali masuala yanayohusu uadilifu wa uongozi, alisema "kama CCM wanasema wanajivua gamba, basi sisi tutawavua nguo kuwa uwezo wao wa kuwatumikia Watanzania umefikia mwisho, watupishe."

Dkt. Slaa alidai kuwa pamoja na waraka huo kupigwa mhuri mkubwa wa neno 'siri', alisema wao CHADEMA wameupata, ambao ndani yake CCM imeeleza sababu zilizosababisha kushuka kwa umaarufu wake, miongoni mwa Watanzania, lakini yeye akasema kuwa chama hicho kimegundua mapungufu hayo kikiwa tayari kimechelewa, kwani wananchi wameonesha kila dalili ya kukichoka.

"Ndugu zangu hivi karibuni mlisikia tulipoandamana huko Mwanza, Kikwete (Rais, Jakaya) akaagiza sukari ishuke na pia alipokuwa akizunguka katika wizara zote hivi karibuni alikuwa akirudia yale yale ambayo sisi tulikuwa tukiyasema, anaagiza bei za sukari, mafuta, sembe na vitu vingine vishuke, lakini sisi tunamwambia hawezi kushusha bei namna hiyo bila kuanzia kule kiwandani ambako serikali inaweka kodi yake.

"Tunamwambia kuwa hiyo ni danganya toto, alikurupuka...tunataka mafuta, sukari na vitu vingine vishuke bei ili wananchi wapate ahueni ya maisha. Lakini kwa nini mpaka asubiri sisi tuandamane...basi kama kashindwa atuachie sisi tuingie tuongoze...nchi inatawalika vizuri kama watu wako wana uhakika wa kula, kulala katika nyumba za hadhi ya binadamu, kuvaa na wanapata haki zao za msingi.

"Hivi karibuni wamesema wamejivua gamba...mimi nataka niwavue nguo kabisa kuonesha kuwa wamefikia mwisho wa kuwaongoza Watanzania...wanaume tumekamata waraka wao hapa umebandikwa mhuri wa siri, lakini wanaume tumeupata...katika waraka huu CCM inakiri imepoteza ladha kwa Watanzania, wanasema kuwa wanataka kubadilisha sura yao kwa wananchi...ndiyo maana umeona wamemwondoa Makamba wakamwingiza Makamba mwingine.

"Sasa sisi tunasema kuwa wamechelewa mno kuweka vionjo ili ladha yao ikubalike tena kwa wananchi...katika waraka huu pia wanasema kuwa wananchi wameikataa kwa sababu imeshindwa kutekeleza siasa ya ujamaa na kujitegemea...tumewauliza mara kadhaa bungeni CCM nchi hii inafuata ujamaa na kujitegemea ama vipi...kwani mabilioni ya Kikwete na Ridhiwan ndiyo ujamaa huo...Inakiri pia kuwa imepoteza kura na kuporomoka kwa kiasi kikubwa sana.

"Wanasema kuwa imekuwaje kura zao na umaarufu wao umeporomoka kwa asilimia 20 kwa sababu ya mtu mmoja tu ambaye alikuja miezi mitano kabla ya uchaguzi, wanahoji vipi (ingekuwaje) mtu huyo angekuja miezi mingi kabla ya hapo. Wanasema pia kuwa wamepoteza umaarufu kwa sababu wamepoteza tunu ya uadilifu kwa sababu walipigiwa kelele za ufisadi na hawakuchukua hatua mapema, wakasema watarudisha uadilifu haraka.

"Mimi nasema hilo ni jambo zuri, lakini namwambia Kikwete hawezi kurudisha uadilifu katika nchi hii kama yeye bado hajajiuzulu, maana kwenye listi yetu ya watuhumiwa wa ufisadi yumo...JK kaa pembeni, huwezi kurudisha uadilifu nchi hii maana wewe nawe si msafi...waliofikishwa mahakamani si wote tuliowataja katika orodha ile, wameshindwa kuchukua hatua mpaka leo wengine wanaita fedha ni vijisenti.

Aliongeza kuwa katika waraka huo hakuna hata sehemu moja ambapo CCM wamezungumzia juu ya hali ya maisha ya Watanzania na taifa kwa ujumla, akisema kuwa hali inazidi kuwa mbaya kadri siku zinavyozidi kwenda mbele.

"CCM hawaoni usumbufu wanaoupata wananchi katika michango ya elimu, michango ya madawati kila mwaka, CAG katika ripoti yake kabainisha kuwa fedha zile ambazo zilipaswa kuja katika shule kwa ajili ya watoto wenu yaani dola kumi kwa kila kichwa haziji tena badala yake serikali imetoa mwaka jana shilingi elfu saba, ambazo hata hivyo Watanzania hamzioni wala ninyi hamhoji ziko wapi," alisema Dkt. Slaa kwa kirefu.

Katika suala la tuhuma za ufisadi wa bilioni 365, Dkt. Slaa alisema "wanasema katika waraka wao na sisi tumewapigia kelele sana katika hili, wanakiri juu ya ufisadi, lakini bado wanauendeleza...katika taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ameeleza kuwa bilioni 365 zimepotea hazina mahali ambako fedha zetu zinahifadhiwa, najua wengi wenu hapa mkitajiwa bilioni 365 hamjui vizuri lakini nitawaelezea kwa lugha rahisi mnielewe.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Bw. Kabwe Zitto amesema kuwa taifa limeparanganyika na kupasuka pande mbili kutokana na tofauti ya kipato iliyopo nchini sasa kati ya walionacho na wasiokuwa nacho, huku kadri siku zinavyokwenda makundi hayo mawili tofauti yakizidi kupishana hali na kujenga pengo kubwa katikati yao.

Alisema kuwa tofauti ya makundi baina ya maskini (wasionacho) na matajiri (walionacho) inazidi kuongezeka kila siku, ikijidhihirisha katika muktadha wa aina tofauti tofauti kama vile katika matumizi ya huduma za jamii, zikiwemo huduma za elimu, afya na kipato.

"Ndugu zangu wana Sumbawanga, taifa sasa limepasuka sehemu mbili, walionacho na wasiokuwa nacho, maskini wanazidi kuwa maskini na matajiri wanazidi kuwa matajiri. Hali imekuwa tofauti kabisa na wakati wa mwalimu ambapo mtoto wa maskini hakuwa na tofauti na mtoto wa tajiri au kiongozi...watoto wa Mwalimu Nyerere walikuwa wakipishana na watoto wa wakulima katika shule na vyuo vile vile.

Alisema kuwa CHADEMA kimejipanga kwenda kuwapigania wananchi bungeni wakati wa bajeti, ambapo alisema yeye akiwa kama Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, ameagizwa na chama hicho kupeleka bajeti mbadala ambayo itahakikisha kodi katika bidhaa kama vile mafuta inashuka kwa silimia 50 na kupunguza misamaha ya kodi ili ishuke mpaka asilimia 1 ya pato la taifa badala ya sasa ambayo ni asilimia 2, hivyo wataweza kuokoa takribani sh. bilioni 400, kwani sasa inagharimu zaidi ya sh. bilioni 600.

Alisema huo mfumo wa kodi unaotoa misamaha mikubwa ya kodi unamkandamiza mwananchi wa kawaida na kuwabeba matajiri wachache ambao ndio wanapata misamaha mikubwa ya kodi, akisema kuwa chama hicho kimejipanga kuhakikisha hakuna kodi inayomhusu mwananchi wa kawaida itapandishwa bungeni mkutano ujao.

"CHADEMA tumejipanga, tuko tayari...CCM wameona tumejipanga vizuri kuwa tayari kuongoza nchi, wameanza kusema CHADEMA ni chama cha kikabila na kidini, uongo, CHADEMA iko kila mahali, iko hapa Sumbawanga, iko Arusha iko Pemba iko kila mahali nchini, hatuulizani dini sisi, hata dini za wengine hatuzijui, hiki ni chama cha kitaifa sasa, kiko tayari kuongoza nchi hii, tuungeni mkono tuzidi kuwasemea," alisema Bw. Zitto.

12 comments:

  1. Natafakari sana na maneno ya Dr, Slaa katika mambo yake mengi asilimia 42.5 ndio yana ukweli asilimia zilizobakia ni uzuri,uongo na hazina utafiti wa kina.Kuna mtandao wake ulioko serikalini na ndani ya ccm anawalipa kiasi cha pesa kila mwezi ili wampe data lakini kwa tamaa ya hao jamaa wanampa ripoti zisizo na ukweli nae anakurupuka na kulipuka hivi ni mpk lini atakuwa na mitindo aina hii?Ajitahidi kuvaa mkanda wa suruali yake vizuri maana kabla hajawavua wenzake watamvua yeye!!

    ReplyDelete
  2. Sahihisho: asilimia zilizobaki ni UZUSHI,UONGO

    ReplyDelete
  3. nafikili ccm imefilisika sela na dhamila yao kwa uma nimbaya. na nyinyi mlio kunywa maji ya kijani acheni kuchonga. by the way hamna point zaidi mnadandia danditu kama abiria aliye lkosa nauli. namtakoma 2015 cjui mtafikaje wakati imani yenu kwa wananchi nikiwemo mimi imekufa. MZIKI WA CDM UPOJUUU SANA. dawa si kuchonga dawa kuacha ufisadi.ccm habari ndio hiyo.

    ReplyDelete
  4. UJINGA WANAO WALIOSHINDWA KUJIVUA MAGAMBA. Nafikiri mmetumwa humu kuisafisha CCM, kwa taarifa yenu CCM ni kama SAMAKI hata umuoshe kwa sabuni SHOMBO yake haitoki. MKIWEZA kushughulikia UFISADI tutawaamini. CCM si chama cha wananchi tena, ni chama cha MAFISADI. Bora tuunge mkono chama chochote kile kuliko hiyo CCM iliyojionyesa rangi yake halisi ya KIFISADI.

    ReplyDelete
  5. Eti samaki hata umuoshe kwa sabuni shombo yake haitoki!!Hivi wewe ni muumini wa dini ipi? Maana hata katika dini zote kuna kuungama na ukasamehewa ikiwa ni mkristo au muislamu kwa Mungu hakuna dhambi isiyosameheka.Ina maana mtu akiachana na uovu akaokoka anabadilika anakuwa sio mtu?au ni mtu yuleyule ila matendo yake ndio mapya? Basi ikiwa CCM hawakubaliki basi hata hao wanaojiita wameokoka au wametubia basi hakuna nafuu kwao ni bora waendelee na maovu.Hakuna point wewe una point gani zaidi ya kuiga na kurudia wimbo huohuo? wewe ndio ukae kimya sio unajifanya unalia wakati hujajuwa msiba ni wa nani!!Kashangae feri uone meli inaeleya wewe kijiwe unazama!!

    ReplyDelete
  6. Chadema ili msilie tena lazima mwende vijijini. Watu walio wengi wa tanzania hawako mijini kama mnavyodhani. Wafikieni watu wasio na radio. Kuhusu uchaguzi pendekezeni tutumie automated machines zinatumika nchi masikini kama philippines kwa nini tanzania ishindwe tuachane na wizi. Ni rahisi na matokeo hutoka mara baada ya sekunde tano. Zipo za umeme na betri na box hubebwa na mtu mmoja ni la kilo kumi. Tuachane na chaguzi za kale za wizi.
    Pili achani jazma na migongano kati yenu na muwaaminishe wananchi na kuwapa uwazi kwa jinsi mtakachofanya ili nchi isongee mbele ambacho hakifanyiki na CCm, vinginevyo mtabaki kulia na wezi wakaendelea kuongoza nchi. Wenye vyama hongera mie sijakipata cha kujiunga! Niachagua anayefaa si chama

    ReplyDelete
  7. Hata ujifanye kutumia kigezo cha dini bado dhamira yako inakusuta tu. Kama kuungama kwa kuvua MAGAMBA kumeshindikana, then haijaungama bado. Usitake kunizubaisha eti viongozi wa juu wa chama ndiyo waliokuwa MAGAMBA. Maana tulitegemea makubwa sana na tulianza kurudisha IMANI yetu kwenye chama. Kwa jinsi mlivyonogewa na dhami ya UFISADI imeshindikana kabisa kuungama kwako unavyokuita. Namshangaa Mwenyekiti wetu kushindwa kufanya maamuzi magumu kwenye chama na hata serikalini. Tumekata tamaa na kuchoka sana, tunatamani 2015 ije haraka ili tuondokane na JINAMIZI hili. Huyu samaki badala ya kunukia shombo, sasa ameanza na kuchina kabisa. Muende mkaongopeane kwenye vikao vyenu mnavyojifariji, msitudanganye na kutukebehi humu. Eti wakereketwa....???? Njaa na uchu tu.

    ReplyDelete
  8. HUYU "SLAA" NA VIONGOZI WENGINE WA CHAMA CHAKE MNAWAVIMBISHA VICHWA KWA KUTOA KWENYE VYOMBO VYA HABARI KTK KILA UTUMBO WANAOUSEMA. ISHU NI KUWAKAUSHIA TU,WAWE WANASEMEA KWENYE MAGAZETI YANAYO WAUNGA TU. KAMA VILE "MWANAHALISI" (gazeti chochezi hili,kuweni nalo makini jamani)

    ReplyDelete
  9. Mwanahalisi na slaa ndo wamewafanya mvue magamba na bado mtakoma mwaka huu..mnatapatapa tu mara magamba,mara siku 90 mara tena mmehairisha cjui barua hamuandikian tena teh teh teh

    ReplyDelete
  10. hii kwa habari ya gaziti la mwananchi
    'SLAA ACHAFUA HALI YA HEWA KWA PINDA'
    MIMI SINA CHAMA LAKINI NAWASHAURI CHADEMA WAWAELEZE WATU MADHAMBI YA CCM LAKINI WAWAELEZE WATU WA SUMBAWANGA KUWA IMANI ZA KISHIRIKINA HAZILETI MAENDELEO. Rukwa Ni moja ya mikoa inayoamini uchawi kuliko sehemu yeyote ya tanzania. Ni huko na mbeya wanakochuna ngozi na kuua watoto wachanga.
    Maendeleo hayaletwi na chama na serikali pekee. Serikali ya Tanzania inajitahidi kuliko ya kenya na Rwanda na ukanda mzima wa afrika mashariki lakini watu wa kenya hujishughulisha sana kutafuta mahitaji kuliko sisi watanzania hata wakiwa kwenye hali mbaya.
    Jiulize tu, kwa nini moshi kumeendelea na kunazidi kuwa safi kila kukicha na wakati kwingineko kunazidi kuwa na hali mbaya? Hapa japan watu wametoka kwenye tsunami lakini utawakuta wanakofanya kazi kwa masaa zaidi a nane,utashangaa.
    Nawapongeza chadema kwa kwenda vijijni lakini msisahau kuwaambia watu kuwa maendeleo huchochewa na serikali lakini above all ni 'attitude of mind'. Wapo wenye hela hapo baada ya kuuza mahindi wanaenda zambia kununa uchawi, nimeishi hapo zamani.KUNA KITU TENA!

    ReplyDelete
  11. jamani wanasiasa waacheni kama walivo siasa ni siasa tu chadema wakiingia madarakani usitegemee kwamba wanayoyazungumza hapa wataboresha no ni wizi mtupu sipendi siasa na siamini mwanasiasa yeyote yule wote ni wamoja tu

    ReplyDelete
  12. Enyi mnaotetea hili dubwan CCM Mbona hamuwatendei haki wananchi na huu ugumu wa maisha?hamuoni?au mnaishi kwa neema za ufisadi?alichosema zito ni serikali kupunguza kodi katika mafuta ili kuwe na ahueni!sawa kwenye soko la dunia mafuta yanapanda lakin serikali ya mafisadi ipunguze kodi ya mafuta1Kenya wanaweza vp?fikirini kwa kichwa sio matumbo yenu!Tuangalie maslahi ya nchi si chama!

    ReplyDelete