Na Zahoro Mlanzi
SIKU moja baada ya timu ya Simba kuondolewa katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limesema timu hiyo
itaumana na DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) katika Kombe la Shirikisho Juni 12 mwaka huu, Dar es Salaam.
Simba iliondolewa katika michuano hiyo na Wydad Casablanca ya Morocco kwa mabao 3-0 kwenye mechi ya mkondo mmoja ya Klabu Bingwa.
Wawakilishi hao wa Tanzania waliipata nafasi hiyo baada ya kuondolewa TP Mazembe ya DRC ambayo ilimchezesha mchezaji asiyestahili.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa shirikisho hilo, Boniface Wambura alisema pamoja na kuondolewa katika michuano hiyo, bado wana kibarua kingine katika Kombe la Shirikisho.
"Simba imepigana kufa au kupona, lakini ndiyo hivyo wakafungwa, ila pamoja na kuondolewa bado wana nafasi katika Kombe la Shirikisho na watacheza na Motema Pembe ya DRC Juni 12, mwaka huu," alisema Wambura.
Alisema muda uliobaki wa kujiandaa na mchezo huo ni mdogo hivyo ni vizuri wakiendelea na mazoezi, ili wafanye vizuri na kutinga hatua ya makundi katika kombe hilo.
Wambura alisema wamepata bahati ya kuanzia nyumbani, hivyo ni jukumu lao kuhakikisha wanafunga mabao mengi ili wajiweke katika nafasi nzuri kwenye mchezo wa marudiano.
Timu hiyo ilitarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam jana alfajiri ikitokea Misri kuendelea na maandalizi ya mchezo dhidi ya Motema Pembe.
simba hawana lolote , kelele tu za mwenyekiti wao ambaye anajifanya afisa habari. jamaa anapenda sana kuongea.
ReplyDeletemtafungana hapa simba na yanga na sio mkitoka nje ya tz.
ReplyDeletekufungwa ni sehemu ya mchezo man utd kafungwa sembuse simba.maandalizi madogo ndio sababu ila shirikisho mambo yatakuwa mazuri
ReplyDeleteSimba mkomae hawa watz wenye msimamo wa kubeza kila kitu chao ni wafilisika wa Uzalendo. Simba songa mbele; mtafika tu; Hata Roma haikujengwa siku moja
ReplyDeleteHii inatakiwa kuwa fundisho kwa Simba.Tatizo hapa ni maandalizi yanakuwa si ya kutosha,kwanza walitarajia kuwa na mchezo wa majaribio thidi ya Zanzibar Ocean View kweli hii inaingia akilini kweli wakati timu wanayokwenda kucheza nayo ina jina kubwa tu Afrika.Simba mnatakiwa muwe na maandalizi ya kutosha pamoja na kuwa na mechi za kujipima nguvu na timu kutoka Afrika magharibi au kaskazini ya afrika kama Egypt,Tunisia,Algeria na Libya na sio kuishia kucheza na timu za nyumbani tu pamoja na Kenya.Jifunzeni kutokana na makosa yenu na muache mpira wa kucheza mdomoni tu.
ReplyDelete