Na Gladness Mboma
CHAMA cha Wataalamu Washauri Tanzania kimesema kuwa Tanzania inalipa sh. trilioni mbili kwa mwaka katika shughuli mbalimbali za kishauri, lakini asilikia 95 ya
shughuli za kitaalam zinafanywa na watu wa nje.
Mwenyekiti wa Chama hicho, Bw. Aloyce Mushi aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wao mkuu utakaofanyika leo Dar es Salaam.
Alisema kuwa wataalamu na washauri hao kutoka nje ya nchi wanalipwa fedha nyingi kuanzia asilimia tano hadi kumi ya mradi na kudai kuwa kazi ya ushauri siyo kubwa, bali mtu anatakiwa kumuonyesha mtu tatizo alilonalo.
"Tatizo la umaskini nchini linatokana na kutotumia watu wao kupigana na umaskini wao, hivyo inabidi ifike mahali tusitegemee misaada ambayo haituondolei umaskini," alisema.
Alisema pamoja na misaada mbalimbali ya kifedha ambayo nchi inapatiwa kutoka katika nchi mbalimbali duniani, anashangazwa na umaskini ambao unaendelea kukithiri kila kunapokucha .
Bw. Mushi alisema kuwa Watanzania hawatambuhi umuhimu wa rasilimali watu kwa sababu ya kutoelewa mfumo unaoeleweka.
Alisema kuwa mkutano wa leo utajadili ni jinsi gani kutakuwepo chombo cha sheria kitakachowaratibu wataalamu wanaoingia nchini ili kuangalia kazi walizozifanya na zina faida gani kwa nchi.
No comments:
Post a Comment