Na Agnes Mwaijega
SHIRIKA la Umeme nchini (TANESCO) limesema kuwa mgawo wa umeme umepungua na kurudi katika hali yake ya zamani kutokana na kukamilika kwa matengenezo ya
visima vya kuzalisha gesi asili katika kisiwa cha Songosongo.
Visima hivyo vilikuwa katika matengenezo kuanzia tarehe 19 hadi 26 Mei, mwaka huu, hivyo kusababisha upungufu wa hali juu wa umeme katika Gridi ya Taifa na kuwaathiri watumiaji umeme
Upungufu huu ulitokana na Visima na Mitambo ya gesi asili iliyopo katika Kisiwa cha Songo Songo, mkoani Lindi, kuzimwa na wamiliki wake – Pan African Energy Tanzania Limited – kwa ajili ya ukaguzi na ukarabati.
Taarifa iliyotolewa na shirika hilo Dar es Salaama jana ilieleza kuwa lengo lilikuwa kuboresha viwango vya gesi inayozalishwa na kusafirishwa kutoka kisiwa hicho hadi Dar es Salaam kwa ajili ya kufua umeme na kutumiwa viwandani.
Ilieleza kuwa vituo ambavyo hutumia gesi asili ya Songosongo kuzalisha umeme ni Songas, Ubungo Gas Plant na Tegeta Gas Plant. Umeme wa gesi huchangia karibu nusu ya umeme unaofuliwa kwenye vituo vyote nchini.
Hata hivyo taarifa hiyo ilieleza kuwa kina cha maji kwenye Bwawa Kuu la Mtera bado kipo chini na hakiridhishi, hasa ikizingatiwa kuwa msimu wa mvua unakaribia kumalizika.
"Leo hii tarehe 26 Mei 2011 kina cha maji kwenye bwawa la Mtera ni mita 691.08 juu ya usawa wa bahari. Kina cha juu kwenye bwawa hilo ni mita 698.50 na kina cha chini ni mita 690.00, juu ya usawa wa bahari.
"Hivyo basi kutokana na kina cha Mtera kuwa chini shirika litaendelea na mgao wa MW 182,"ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
hawa`watu wanachezea akili zetu. mwisho wa mwezi wa pili walitoa kina hicho hicho cha maji. ni kama vile maji ya mvua zilizonyesha hayakupitia huko mtera. tukubali tu kwamba umeme wa maji na hata wa mafuta sasa basi tuangalie namna ya kuvuna upepo na jua
ReplyDeleteWANAKULA NJAMA NA WAUZA MAJENERETA
ReplyDeleteFunga shirika la umeme na kampuni nzima, rudisha mtsungu atutawale tena tuwe chini ya himaya ya viboko. Inaleta hasira sana kuona watu waliokabidhiwa dhamana ya taifa wanatuchezea akili. Kikwete ruhusu viboko kwa watendaji wabovu; wapigwe fimbo wakaoneshe kwa wake zao au waume zao! Bull-goat!tumechukia fridge zetu tunajaza chakula cha watoto kila siku tunamwaga!paipmbafu!
ReplyDelete