19 May 2011

Mbunge wa Tarime apopolewa Nyamongo

*Katibu Mkuu CCM aahirisha mikutano yake
*Serikali kugharamia mazishi ya waliouawa


Veronica Modest na Timothy Itembe, Tarime

WAKATI Mbunge wa Tarime, Bw. Nyambari Nyangwine amepopolewa kwa mawe na wapiga kura wake wa Nyamongo wilayani Tarime ambao ndugu
zao watano wameuawa na polisi katika Mgodi ya Nyamongo, Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Wilson Mukama ameahirisha mikutano ya hadhara ambayo ilitegemewa kufanyika katika eneo hilo.

Ingawa, Bw. Mukama hakuhusiaha na mbunge huyo wa CCM kurushiwa mawe na wananchi kwa madai ya kutokutoa kauli juu ya unyanyasaji wa polisi dhidi yao, wachunguzi wa mambo wanasema sababu hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa.

Akiwa katika ziara yake ya kwanza katika mkoa wa Mara baada ya kuchaguliwa, Bw. Mukama alisema kuwa si vema kufanya mkutano wa hadhara jirani na eneo lenye msiba.

"Kwa desturi yetu sisi waafrika hatuwezi kufanya mkutano wa hadhara hapa karibu na eneo lenye msiba kwani hao waliokufa ni binadamu wenzetu hivyo yatupasa kuheshimu msiba," alisema Mukama.

Uamuzi huo umekuja baada ya Bw. Nyangwine akiwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Bw. Amos Sagara kunusurika kujeruhiwa baada ya kupopolewa kwa mawe wakati wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.

Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa mbunge huyo alipata tetesi kuwa watu waliofiwa na jamaa zao wamekataa kuzika miili ya marehemu hao mpaka serikali itoe tamko, hivyo alikwenda katika eneo la tukio ili kufanya  mkutano wa hadhara na kutoa 'tamko la serikali' juu ya mauji yanayoendelea kutokea katika mgodi huo mara kwa mara.

Akiwa katika mkutano huo baadhi ya watu walianza kurusha mawe na kuponda magari na kupasua vioo ambapo Mbunge huyo alifanikiwa kukimbia, huku mwenyekiti wa halmashauri akichaniwa shati na kukimbia kifua wazi.

Hali hiyo ilijitokeza baada ya wananchi kukasirishwa na mauaji yanayotokea mgodini hapo mara kwa mara ambapo warifikiri kuwa mbunge huyo angeweza kukomesha mauji hayo, lakini hajafanya lolote.

Wakati vurugu zinaendelea Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Bw. John Henjewele aliyekuwa eneo hilo aliomba aongezewe nguvu kutoka Jeshi la Polisi ili kunusuru maisha ya viongozi pamoja na watu aliokuwa ameongozana nao, wakiwamo waandishi wa habari.

Mbunge azungumza

Mbunge wa Tarime Bw. Nyambari Nyangwine amekiri kushambuliwa kwa mawe yeye kwa msafara wake ambao ulikuwa na lengo la kwenda kutoa tamko dhidi ya mauaji yaliyotokea Nyamongo, anaripoti Grace Michael.

Msafara wake ambao ulikuwa umeongozana na waandishi wa habari pamoja na viongozi wa CCM ulipata msukosuko huo jana mara baada ya kufika eneo hilo ambapo mkutano huo ulitarajiwa kufanyika.

"Tulipofika eneo hilo, tukawasikia wananchi wakisema kuwa hawataki serikali wala mbunge na mbaya zaidi wakaanza kuhoji kwa nini baadhi ya viongozi wa chama niliokuwa nao wamevaa nguo za chama...nilipoona kuna kila dalili ya hatari walinzi wangu waliniondoa na kunipandisha kwenye gari na kuondoka," alisema.

Alisema kuwa msafara wake ulikuwa na magari manne na kutokana na vurugu zilizotokea hapo, magari mawili yalishambuliwa na mawe na kuharibika vibaya.

Alisema kuwa magari ambayo yalishambuliwa kwa mawe ni yale ambayo yaliwabeba waandishi wa habari na wengine waliokuwa wameongozana naye lakini gari alilokuwamo yeye halikuathirika.

Bw. Nyangwine alitupa mzigo huo kwa wanasiasa, akisema kuwa vijana waliofanya vurugu hiyo waliandaliwa na Diwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Serikali kugharamia mazishi

Naye Agnes Mwaijega anaripoti kuwa serikali imeahidi kushughulikia na kugharamia shughuli za mazishi ya watu waliouawa wakati akipora mchanga wa dhahabu katika mgodi wa Nyamonge.

Pia imeunda timu maalumu inayojumuhisha wawakilishi kutoka katika wizara hiyo na Jeshi la Oolisi kwa ajili ya kufuatilia mauaji hayo.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Balozi Khamis Kagasheki alisema serikali inachukua jukumu hilo kwa sababu waliokufa katika tukio hilo ni Watanzania.

Alisema kuwa sheria itachukua mkondo wake dhidi ya wale wote waliohusika katika tukio hilo.

"Sisi kama wizara tutafuatilia kwa ukaribu zaidi ili kupata taarifa kamili juu ya tukio hilo. Tuna imani kwamba timu tuliyounda itafanya uchunguzi na italeta majibu yatayotusaidia," alisema.

15 comments:

  1. SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI TAYARI KUNA SENSE OF GUILTY.CHANZO HAPA SIYO CHADEMA WALA NINI BALI NI MIKATABA MIBOVU AMBAYO SERIKALI YA NCHI HII IMEKUWA IKIISAINI AMBAYO HAINUFAISHI WANANCHI BALI WAWEKEZAJI NA VIONGOZI WANAOSAINISHA MIKATABA NA KUWAACHA WANANCHI WALIOZUNGUKA MAENEO YAO WAKIWA MASKINI WA KUTUPWA. WANANCHI WAMEVUMILIA WAMECHOKA SASA WAMEANZA KUCHUKUA HATUA MIKONONI MWAO.

    ReplyDelete
  2. Lema njoo Nyumbani Arusha tokatumekuchagua hatukuoni kuchakutwa uko maandamanoni.Mama zetu bado wananyang'anywa mboga zao kwenye vikapu na halmashauri wa ya Arusha.

    Slaa hongera kwakuwekeana mkataba nahao.we kweli ni msomi maana unajua unachofanya lakini tumia busara na usomi wako ili mbunge wetu Lema atutumikie.

    Chadema Arusha tunataka mbunge wetu jamani kama tungejua kama wabunge tuliowachagua mtawafanya vinyago wa kuwatembeza nchi nzima naapa Arusha tungekwenda TLP.

    Hawa wabunge munawatembeza bila wao wenyewe kujawa kwa uhakika madhumuni yenu ndiyo maana tumeona mbeya mbunge anatoa mwito kwa watu wake wampopowe mawe kiongozi wanchi WA NCHI, aliye chaguliwa toka kyaka hadi pemba namanga hadi hadi tandaimba. CHADEMA be serious otherwise you will popularity and no longer the Tanzania shall witness the demise of the Chaggaland founded party.

    ReplyDelete
  3. Tuwashughulikie viongozi walio kubali mikataba mibovu.itakuwa rahisi zaidi kuliko kweda kwenye migodi.

    ReplyDelete
  4. CHADEMA MUNAWIVU,ACHENI TULE TUSHIBE,KILA MBUZI ATAKULA KWA UREFU WA KAMBA YAKE.MNAZUNGUKA KUWAELIMISHA WANACHI HAMJUI USEMI UNAOSEMA USIMWAMSHE ALIYE LALA, UTALALA WEWE.

    ReplyDelete
  5. hata mwaka mmoja tangu tuchague serikali mpya haujapita hv kwel miaka mitano itafika kwel?

    ReplyDelete
  6. Tunaomba nguvu hii iendelee kwa wanaouza ardhi yetu kwa watu wengine. Juzi serikali wamesaini mkataba wa kuwaleta Wabangladeshi kwa ajili ya kilimo miaka 99. Wanadanganya ni mkataba kumbe wanauza artdhi yetu.

    Kila mbunge awe macho na jimbo lake wananchi wasikubali kuwapa hayo mashamba, kwa nini wasipewe wazawa wenye juhudi wakalima na wakatafu[NENO BAYA] soko. Wabangladeshi wakifunguliwa wapo kama nyuki mtashangaa watasambaa kuliko hata wachina ninawafahamu na ninaona usumbufu wanaoupata nchi waliowapokea kama wakimbizi. Hawa watu ni wavivu kama nini halafu wanaona Tanzania ndio dampo la kutupia yaliyowashinda wao.

    Serikali badala ya kufikifia maisha ya watanzania wao wanafikiria kuwaletea matatizo. Mimi sioni sababu ya maana kuchukua watu katika nchi yao eti kwa ajili ya kilimo wakati wazawa wanateseka.

    Tetesi ninayosikia kwa sababu nipo na wao wanasema rais wao wa Bangladeshi amenunua sio mikataba kama walivyoandika. Asanteni

    May 19, 2011 12:30 AM

    ReplyDelete
  7. Nafurahishwa sana na haya yanayotokea. Maana ni mazao ya ujinga wenu watanzania wa kutotaka kubadili uongozi. Acheni tuuane wenyewe kwa wenyewe kwa kulinda wageni na mashamba nayo yauzwe kwa Wabangladesh. Labda ndo tutashtuka!

    ReplyDelete
  8. Serikali ya awamu hii imekuja na mtindo w kuwaua wananchi kisha kuwasaidia kwa kugharamia mazishi.

    Hii serikali ya wakati huu inaweza kuingia katika rekodi ya kufanya mauji mengi zaidi ya raia wake kuliko serikali zozote za awamu zilizotangulia hii!

    ReplyDelete
  9. Tarime oneni mlichochagua je hamkujua. wishes are now not horses

    ReplyDelete
  10. HIYO NDIO SERIKARI YENU MLIOICHAGUA. IMEANDAA MAJENEZA KWA WATAKAO KUFA KUMBUKA MBAGALA,GONGOLAMBOTO. SERIKALI HII HAIJALI MAISHA YA WATU WAKE ILA INAJALI MAZISHI YAO. SERIKALI INA MASLAHI KATIKA MIGODI HII NDIO MAANA HAICHUKUI HATUA MAPEMA KUTATUA TATIZO.MPAKA KUFIKIA 2015 WATAUWAWA WENGI SAAANA.KAMA WATZ HATUTA BADILIKA KUWAONDOA HAWA MAFISADI IKULU TUTAISHA.

    ReplyDelete
  11. Sikujua kuwa mbunge uwa anakuwa na bodyguard akiwa jimboni kwakwe,walinzi wa nini wewe mbunge kama kweli ulipita kihalali?Unaogopa wananchi wako hadi utembee na walinzi?

    ReplyDelete
  12. Lema alienda huko kama wazir kivuli wa mambo ya ndan na ulinzi..afu wabunge wa chadema wa kitaifa..CHADEMA ENDELEEN KUTUTOA TONGOTONGO..IV KWANN POLIS WANAUA SANA UTAFIKIL MAPOLI WA MAKABULU WA S.AFRICA.KWEL CCM MAKABURU WEUSI

    ReplyDelete
  13. Wewe Kagasheki unaongea nini? Uliua ili uje ugharamie mazishi? Unaona fahari kuzika? wewe ni muuaji kama hao polisi. Watanzania tumechoka.

    ReplyDelete
  14. Jk na wenzako hebu angalieni hiyo mikataba ambayo wewe umeirithi toka kwa mkapa. Ni mjinga tu anayeweza kuruhusu kitu km hicho kiendelee. Yes, najua mtaleta sababu kwamba potential investors wataona nchi yetu ni unpredictable/investment risk ni kubwa, siyo kweli maana hata wao wanajua kabisa kwamba wanachofanya ni wizi mtupu. mtupu.Kama hao waliopo wanakataa kukubali facts za kwamba wanatupunja, tuwaondoe investors wanaotufaa watakuja tu maana wanayataka hayo madini na sisi ndo wamiliki. Mfano tunasema Botswana ni success story, mbona hao walowekeza Botwsana walikubaliana na mashariti ya nchi, au tuseme Botswana inawataalamu zaidi wa mikataba kuliko siye, la hasha, ni kwasababu wakuu wa nchi ile wanautashi wa kujenga uchumi wao kwa manufaa yao na watu wao. Mchumi(Profesa) mmoja mjerumani hapa Munich nilikuwa napata naye chakula ktkt mgahawa wa Kituruki akataka niseme km ni kweli Watanzania tumeruhusu makampuni ya madini yasafirishe zahabu kutumia private airports na statistics za wanachosafirisha ni za uongo. Nilimjibu kuwa sina maelezo reliable kwasababu ni kitambo sipo Tanzania. Akauliza pia km wages ratio ni 1:70+, akimaanisha mshahara wa mzungu mmoja kwa mwezi unaweza lipa wafanyakazi zaidi ya sabini wa kitanzania wanaofanya kazi migodini. Nilimwambia sinatakwimu hizo prof. Nilichojifunza ni kwamba makampuni haya yanainyonya sana nchi yetu, na wanyonyaji wanajua hilo, kwa kihiyo tunapokaa kimya bila kuchukua hatua wanatushangaa kabisa. Hao wananchi ambao nahisi serikali itasema wanafanyafujo kwa kwenda kuchukua mchanga wa dhahabu wanatoa ujumbe kwa serikali kuwa bora wafe kuliko kuishi maisha magumu wakati wageni kwa mwamvuli wa uwekezaji wananeemeka. Kwa hiyo mheshimiwa rais jipange vizuri na wataalamu wetu hususani wa sheria muangalie jinsi gani muongee na hawa wezi namna ya kuleta win-win situation badala ya hii iliyopo (win-loose) ambayo wanajua kabisa kuwa wanaiba.

    ReplyDelete
  15. sijui itakuwaje masaki kukigunduliwa alimasi sipati picha wataondolewa au kutapitishwa marekebisho yasheria kazi kwenu wabishi na warithi na wabia wa ufisadi sasa ni saa kumi na moja alfajiri saa za kitanzania watz wameanza kuamka mungu ibariki tz wabadilishe mioyo mafisadimaana sasa wameleta usa ndani ya dowans hii ni hatari mh. raisi wa wananchi na mafisadi wengi wape kemea amani ya tz hipo mikononi mwako mimi mnyonge

    ReplyDelete