KUALA LUMPUR, Malaysia
TIMU ya Chelsea itakwenda kucheza mechi za kirafiki nchini Malaysia kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao.
Kwa mujibu wa waandaaji wa safari hiyo, timu hiyo itakutana na
timu ya Malaysia XI kwenye Uwanja Bukit Jalil ambao una uwezo wa kuchukua watazamaji 87,000 ambao una Julai 21 mwaka huu. Uwanja huo upo katika mji mkuu wa nchi hiyo Kuala Lumpur.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuandaa matamasha aishie nchini Singapore, John Merritt aliliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP kuwa mechi hiyo ni sehemu ya ziara ya timu kutembelea bara la Asia.
Merrit alisema mbali na Chelsea, Liverpool, na klabu nyingine za Ligi Kuu England nazo pia zimeshasema zitakwenda kucheza mechi za kirafiki nchini Malaysia, ingawa hazijadhibitisha.
"Hivyo tunaweza kwanza kutangaza timu hii moja ya Chelsea," alisema. "Tunaweza kutangaza nyingine zaidi wiki chache zijazo," aliongeza.
Alisema kuwa tiketi za mechi hiyo zitaanza kuuzwa Ijumaa kwa njia ya mtandao.
Kwa mujibu wa tovuti ya Chelsea, timu hiyo itafungua mazoezi ya kujindaa na ligi kwenye uwanja huo kabla ya Julai 24 kwenda mjini Bangkok na Julai 27 na 30 mwaka huu itakuwa Hong Kong.
Wakati Chelsea itakuwa tayari imeshacheza mara mbili nchini Malaysia, tangu mwaka 2003, waandaaji hao walisema kuwa hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Liverpool kutembelea taifa hilo la Kusini mwa Asia.
No comments:
Post a Comment