01 June 2011

Drogba kusaini mktaba mpya Chelsea

LONDON, Uingereza

DIDIER Drogba anajiandaa kusaini mkataba mpya katika Klabu ya Chelsea, ambao utafanya kumalizia uchezaji wake hapo.Mshmabuliji huyo awali alielezewa kuwa
huenda angeondoka katia majira ya joto, baada ya Chelsea kumsaini, Fernando Torres kwa ada ya pauni milioni 50.

Lakini chanzo kutoka Blues kilisema: "Mara baada ya kutajwa kwa kocha mpya kitu cha kwanza kitakachofanyika ni Didier, kusaini mkataba mpya.

"Hakuna njia kwamba klabu inataka aondoke, ni mmoja wa washmabuliji wazuri duniani."

Torres hajawa katika kiwango kizuri, alifunga goli moja kati ya mechi 12, ikiwa na maana kuwa nyota wa Ivory Coast mwenye miaka 33 ni wa muhimu.

Chanzo kutoka ndani kilisema: "Unaweza kuhisi kilio kama, Didier angeuzwa na Torres kuendelea kutaabika? Maamuzi yamefikiwa kuwa ni bora kuendelea kuwa nao wote."

Drogba ambaye amebakia mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa anaolipwa pauni 130,000 (sawa na zaidi ya sh. milioni 312) kwa wiki, alikuwa akihusishwa na kutakiwa na timu za Real Madrid na Spurs.

Kwa sasa anaweza kuongezwa mshahara na malipo yake ya mwaka, ambapo mkataba wake utaisha 2013.

No comments:

Post a Comment