31 May 2011

Kamati ya bunge yaibana serikali

*Yagomea bajeti Wizara ya Miundombinu
*Yadai imeshindwa kufufua TRL, ATCL


Na Dunstan Bahai

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imetishia kutoipitisha bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa madai kuwa
wizara hiyo imeshindwa kuwekeza kwenye mashirika nyeti ambayo ni mhimili wa nchi.

Mashirika hayo ni Shirika la Reli Tanzania (TRL), Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) na Bandari.

Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya majadiliano ya asubuhi ya kamati hiyo, Mwenyekiti wa kamati, Bw. Peter Serukamba alisema serikali imekuwa na matumizi mengi yasiyo ya lazima lakini imeshindwa kuwekeza katika mashirika hayo na kusababisha kuelekea kufa.

“Serikali na wizara kwa ujumla inatakiwa kuweka kipaumbele kwanza kwa mashirika haya. Haya mashirika ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wa nchi, ukisema unawekeza kwenye kilimo kwanza, huwezi kufanikiwa kama huna miundombinu bora,” alisema.

Alitoa mfano kuwa ATCL ili iweze kufanya shughuli zake kwa ufanisi inahitaji sh. bilioni 23 tu wakati serikali imelaumiwa kwa kushindwa kuilipia gharama za matengenezo ndege moja iliyopo Afrika Kusini ya shirika hilo, deni la sh. bilioni moja tu.

Aidha TRL nayo inahitaji sh. bilioni 241 kulifufua shirika hilo.

“Wanaosema serikali haina fedha siwaelewi, imekuwa na matumizi yasiyo ya lazima na kushindwa kutoa fedha kwenye maeneo ambayo yanachangia uchumi wa nchi. Lazima mashirika haya yapewe fedha vinginevyo hatuipitishi bajeti hii,” alisema.

Kwa mujibu wa Bw. Serukamba, Wizara ya Uchukuzi kwenye bajeti yake kwa fedha za ndani ilikuwa sh. bilioni 95 lakini ambazo wizara imepewa ni sh. bilioni 45 tu wakati za wahisani zilikuwa ni sh. bilioni 65, lakini zilizopatikana ni sh. bilioni mbili tu.

Kutokana na mazingira hayo, alisema wizara haiwezi kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Mjumbe wa kamati hiyo ambaye ni Mbunge wa Tunduru (CCM) Bw. Mtutura Mtutura alisema serikali inachokosea haitengi vitu ambavyo ni vya kipaumbele.

Alisema kwa wakati uliopo sasa bandari ndogondogo sizitiliwe umuhimu kwani hazichangii uchumi wa nchi kwa kiasi

3 comments:

  1. Big up , kamati endelezeni msimamao mpaka watoe pesa ili tuweze kupata usafiri wa uhakika. kumbukeni watanazania hatutaki blabla tena . Serukamba endelea kuminya.

    ReplyDelete
  2. kwako PETER SERUKAMBA,
    Nyie kama wabunge kazi yenu ya kwanza ni kusimamia kodi wa walipa kodi wenu kuakikisha inatumiwa kwa maslahi ya wapiga kura wenu. unapoolazimisha serikali kuingiza pesa ATCL unakuwa na maana gani??
    ATCL haija dhalisha faida yeyote for the past 10 years leo unataka kuchukua pesa za walipa kodi kuwekeza kwenye failed company.
    kweli wewe una uchungu na kodi za Tanzania?? ni bora pesa hiyo ikatumike kujenga mahospitali au mashule kuliko kutumbukiza kwenye failed company kama ATCL.
    Unapozungumzia umuhimu wa ATCL huna maana gani?? asilmia 99% hawatumii usafiri wa ndege na kama nikitaka kutumia ndege zipo za PRECISION AIR nitapanda siitaji ATCL.
    USHAURI,
    Kama kweli ATCL is viable company kwanini mnataka kutumia pesa za kodi za wananchi kukufulia shirika lilojifia miaka mingi iliyopita kwanini msitafute mtaji kwa kuuza shares kwenye DSE muwaachie watanzania wanaoipenda ATCL wanunue share ili muweze kupata mtaji na msipoweza ku raise pesa za kutosha basi mjue watanzania hawako tayari kupoteza pesa kwa kuwekeza kwenye ATCL and if that is the case so as the Govt.

    ReplyDelete
  3. Mheshimiwa Serukamba na kamati yako,

    Msimamo ambao mmeutoa ni wa kweli na wa dhati kabisa.
    Hakuna nchi ambayo ilicheza na miundo mbinu ambayo iliachiwa na waanzilishi(Wakoloni),Tanzania imekuwa ni nchi inayorudi nyuma badala ya kwenda mbele,Ni aibu kuona kuwa fisadi mmoja anauwa shirika la ndege la umma na kuanzisha la kwake kwa pesa hiyo hiyo ya serikali(alikuwa mkuu wa wizara ya fedha wa awamu ya 2)na shirika hilo sasa linakuwa siku hadi siku hapa nchini,Naona aibu ninapoulizwa na mkenya kuwa shirika la ndege la Tanzania linaitwaje?Kabla ya jibu majonzi hunianza na kumkumbuka yule twiga wetu aliyekuwa mkiani mwa ndege zetu,lakini aibu haifichwi
    huwa najibu lipo lakini wafanyakazi hufika ofisini na kusoma magazeti kisha jioni hurudi majumbani mwao,Hawana ndege wanauza roote tuu sasa.
    Reli ndiyo usiseme wameuza mpaka mataruma,Bandari hata ukimuuliza mtanzania wa kawaida hajui ni ya nani sasa.

    Nundu wape imani hao wanatume ili waone watakubeba vipi.Safari ni ndefu kwa wizara yako.

    Lakini ni aibu
    Anga,Reli na Bandari huwa haviuzwi.

    ReplyDelete