Na Richard Konga, Arusha
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati Thomas Laizer amempongeza Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini Bw. Godbless Lema kwa
kufanikisha harambee ya
ujenzi wa shule ya Kanisa hilo.
Akizungumza wakati wa Ibada ya harambee ya ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kimandolu Lutherani mkoani Arusha Askofu Laizer alisema ukarabati wa shule hiyo utagharimu sh. milioni 85
Alisema kwamba tayari dayosisi hiyo inazo shule za sekondari 12 zenye wanafunzi 6700 hivyo unahitajika moyo wa uzalendo kusaidia kuinua kiwango cha elimu nchini.
Naye Mgeni rasmi katika harambee hiyo,Bw. Godbless Lema alisema hatadharau jitihada zinazolenga kuinua maendeleo ya jamii na badala yake ofisi yake itakuwa bega kwa bega kuhakikisha mafanikio yanapatikana
Aliongeza kuwa suala la elimu ni muhimu katika maendeleo ya nchi na kwamba kiasi hicho cha sh
milioni 85 si fedha ya nyingi iwapo wataamua kwa dhati kushikamana kwa pamoja.
Katika harambee hiyo zimepatikana fedha taslimu pamoja na ahadi jumla ya zaidi ya sh milioni 20
Kwa upande wake Askofu Mkuu msaidizi wa Dayosisi hiyo Solomoni Masangwa amemshukuru Bw Lema kwa kuendesha shughuli hiyo kwa moyo mwema.
mnasikitisha sana moto waja wala msikonde
ReplyDeleteAnalipa fadhila kwa waraka wenu mlioutoa wakati wa uchaguzi
ReplyDeleteGood job Lema!
ReplyDeletemzee laizar hujakosea huyo ni mtu wenu
ReplyDeleteAH! PONGEZANENI TU,TUNAJUA KAMA MNALIPANA FADHILA BAADA YA KUFANYIANA KAMPENI MAKANISANI.ILA ITAFAHAMIKA TUU IPI CHACHU NA IPI CHUNGU.
ReplyDeleteMusa acha ujinga wewe!!nenda shule ndio ujue maana ya michango mashuleni,hizo sio kampeni,ni kusaidia elimu,inawezekana huna elimu hata moja ndio maana unaandika upuuzi hapa...kyekue
ReplyDeletewatu wasiopenda elimu ndivyo mlivyo fadhila gani laizer amemfanyia lema wewe musa usiongee kama unaongea na makalio mbivu zipi zitajulikana acheni usenge na huyo anayesema moto waja labda moto wa mkunduni kwa mama yake muwe na adabu wakati mwingine
ReplyDelete