12 May 2011

Pinda ataka miuondombinu kuboreshwa kukuza uwekezaji,uchumi

Na Agnes Mwaijega

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema ili Afrika ivutie wawekezaji, kukuza uwekezaji na kukuza uhuru katika maeneo huru ya bara lazima miundo mbinu iboroshwe
kama umeme maji na barabara.

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Maeneo Huru ya Uwekezaji Afrika (AFZA), Bw. Pinda alisema katika nchi nyingi za bara la Afrika changamoto kubwa ambayo inachangia uwekezaji kuwa mdogo ni kuwepo kwa miundo mbinu mibovu.

"Miundo mbinu ni mibovu, lakini ikiboreshwa na kuwa katika hali nzuri nchi za Afrika zitawavutia wawekezaji," alisema.

Pia alisema serikali katika nchi zote za Afrika zinatakiwa kutoa msaada kwa AFZA ili uwekezaji ukue na kuendelea kwa manufaa ya bara zima.

"Jitihada za ziada zinahitajika ili kuhakikisha nchi za Afrika zinajitangaza na kuwavutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya Afrika," alisema.

Aliongeza kuwa kuna umuhimu  wa kujikita katika kukuza uwekezaji kwa sababu una mchango mkubwa katika kufikia malengo ya milenia,kuondoa umasikini,kuboresha maisha ya wananchi na kuongeza ajira katika jamii.

Aliongeza kuwa kuna umuhimu  wa kujikita katika kukuza uwekezaji kwa sababu una mchango mkubwa katika kufikia malengo ya milenia,kuondoa umasikini,kuboresha maisha ya wananchi na kuongeza ajira katika jamii.


Bw. Pinda alisistiza kuwa sera za serikali katika nchi za Afrika juu ya uwekezaji kwa maendeleo ya kiuchumi zinatakiwa kuwepo ili kukuza uwekezaji.

"Serikali zinatakiwa kuonesha nguvu,kuwa mstali wa mbele na kuweka misimamo ambayo itakuwa msingi katika kukuza na kuendeleza uwekezaji," alisema.

Aliongeza kuwa ana imani kubwa kwamba mkutano huo utaleta mabadiliko makubwa katika sekta ya uchumi nchini na kuisaidia serikali kufikia malengo yake ya kufanikisha kuanzisha viwanda.  

Alisema maeneo huru ya uwekezaji Afrika ni mbinu mojawapo ya ambayo ikutumiwa vizuri itasaidia kukuza maendeleo ya kiuchumi na yatasaidia katika kuondokana na suala la kuwa tegemezi kwa nchi za nje.

Naye Mkurugenzi wa EPZA, Bw.Adelhelm Meru alisema katika mkutano huo wa siku tatu watapata fursa ya kubadilisha utaalamu ili kuleta maendeleo.

No comments:

Post a Comment