12 May 2011

Shein ateua Katibu wa Baraza la Wawakilishi

Na Mwajuma Juma, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein amefanya uteuzi wa Katibu wa Baraza la Wawakilishi kwa kumteua Bw. Ibrahim Mzee Ibrahim (45) kuwa
Katibu wa Baraza hilo.

Taarifa ya Ikulu iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee imesema kuwa uteuzi huo umeanza Mei 4, mwaka huu.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Ibrahim Mzee alikuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi Uteuzi wakea umeakuja baada ya aliyekuwa Katibu wa Baraza hilo, Bw. Khamis Juma Chande kustaafu kazi Januari 2007.

Bw. Mzee ni mwanasheria mwenye Shahada ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kabla ya kuteuliwa mwaka 2007 Mzee alikuwa kiongozi wa ngazi ya juu katika baraza hilo.

Wakati huo huo, Rais Dkt. Ali Mohammed Shein, amemteua Abdulwakil  Haji  Hafidh kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Watu wenye Ulemavu Zanzibar.

Aidha Bw. Hafidh ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifhadhi ya Jamii Zanzibar(ZSSF), ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha Umoja wa Watu wenye Ulemavu Zanzibar.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi huo huo umefanyika kwa mujibu wa kifungu Na.9 cha sheria ya mwaka 2006. na uteuzi huo umeanza Aprili 23, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment