25 April 2011

Waomba Kikwete ampe Kimaro ubunge

Na Grace Michael

BAADHI ya wananchi wa Jimbo la Vunjo, wamemwomba Rais Jakaya Kikweye kuangalia uwezekano wa kumteua aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Bw. Aloyce
Kimaro kuwa mbunge.

Rai hiyo ilitolewa juzi na wananchi hao ambao waliongozwa na Bw. Sadik Mneney kuwa pamoja na kuwa na imani kubwa na mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Bw. Augustino Mrema, lakini bado wanaomba Bw. Kimaro ateuliwe ili kuongeza nguvu na kukamilisha kazi aliyoianzisha.

"Tuna imani kubwa na mbunge wetu kuwa atatekeleza kwa vitendo ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni kwa ajili ya kutuletea maendeleo ya kiuchumi hasa katika kufufua zao la Kahawa ambalo ndio zao kuu la uchumi wetu, lakini hata Bw. Kimaro bado tunamhitaji na ndio maana tumeamua kumwomba rais kwa kutumia mamlaka aliyonayo kumteua," alisema Bw. Mneney.

Alisema kuwa katika kipindi chake cha miaka mitano (2005-2010), Bw. Kimaro alijitahidi kubuni, kutafuta fedha na kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jimbo la Vunjo na miradi hiyo ni pamoja na na uanzishwaji wa Benki Vijijini (VICOBA), miradi ya maji, elimu, ujenzi wa Hospitali yenye hadhi ya wilaya na ujenzi wa barabara.

"Sisi Wananchi wa Jimbo hili tunaona kuwa miradi hii ambayo ni ya manufaa makubwa kwa Wananchi wa Jimbo hili itasimamiwa vizuri kama aliyeibuni atapata nafasi ya kuipigania katika vyombo vya maamuzi likiwamo bunge letu," alisema na kuongeza kuwa.

"Hatumaanishi kuwa mbunge wetu Mrema hataweza kutuletea maendeleo, la hasha! Bali uzoefu unaonesha kuwa pale ambapo mwanzilishi wa jambo fulani anakuwa ameondoka hasa viongozi wa kisiasa, uendelezaji wa mawazo yake na fikra zake utategemea zaidi utashi wa kisiasa wa mrithi wake," alisema.

Alisema kuwa nia ya wananchi hao ya kutaka kurejeshwa kwa Bw. Kimaro ndani ya bunge ni kutaka kusaidiana na Mrema katika kupigania maendeleo ya wananchi wa Jimbo la Vunjo.

Taarifa hiyo ilitolewa kwa ushirikiano wa Mchungaji Joram Monyo, Bw. Sadik Mneney, Bw. Shaban Ombasele, Bi. Prisca Tarimo, Bi.Monica Temba na Bw. Jullius Mkojera.

6 comments:

  1. Wananchi wenzangu wakati mwingine sijui inakaeje hii, kama mlimuhitaji huyo Kimaro kuwa mbunge wenu kwa nini hamkumpa kura zenu nyingi? Mnafikiri kwa ushawishi wenu huu Rais atawaelewa? Any way sijui!

    ReplyDelete
  2. Hili nalo ni kichekesho! Unafiki wa wapiga kura huu. Wasubiri 2015.

    ReplyDelete
  3. WAJILAUMU HAO HAO WANA CCM WALIOWEKA KAMPENI YA KUMCHAGUA CHRISPINE NA KUMWANGUSHA KIMARO KWA VISA VYAO NA WAKINA MINJA MTOTO WAKIDAI KWAMBA HAKULIPA GHARAMA WALIZOTUMIA KIPINDI CHA KAMPENI. IN GENERAL KUCHAGULIWA KWA AGUSTINO KUMEWAUMIZA SANA MATAJIRI WA HIMO NA MARANGU

    ReplyDelete
  4. SASA NDIYO WANAKUMBUKA SHUKA WAKATI KUMESHAKUCHA AAHH!!! NJAMA ZA KIMARO KWA KUTAKA UBUNGE KWA MLANGO WA NYUMA KWA KUWATUMIA BAADHI YA MWANANCHI KUMUOMBEA KWA RAISI.

    ReplyDelete
  5. Wananchi wako right sema concept yao wengi hawajua. Msipopoe hoja ya wananchi kwa fikra mgando. Fikiri kwa undani wenzenu wanataka kupiga ndege wawili kwa jiwe moja nyie mnawaponda. Thats why every where chagga are best!

    ReplyDelete
  6. mmmh nawashangaa mawazo ya mmoja sio ya wengi, anyway kuga madiwani ili kimaro hatukutaki na gamba lako. hiyo ni njama ya chama tawala kilimanjaro kuongezea nguvu halmashauri ili kuwavuruga madiwani halali kutenda kazi yao kwa ufasaha

    ReplyDelete