Na Eric Toroka
WAKAZI wa Gongolamboto waishio mabondeni na wale ambao nyumba zao ziliathiriwa na mabomu Februari 16, mwaka huu watafaidika kwa kufidiwa
viwanja vipya na kujengewa nyumba mpya za matofali.
Hayo yalisemwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Sadiki wakati akikabidhiwa Zahanati ya Kivule na Kampuni ya Bia nchini (TBL) baada ya ukarabati. Zahanati hiyo iliharibiwa na mabomu kwa kiwango kikubwa.
“Waliojenga mabondeni tutawapa viwanja vipya katika maeneo mapya yaliyopimwa kwa sababu hatuwezi kuwafidia kwenye sehemu ambazo serikali inapinga kujenga kwenye makazi ambayo ni hatarishi na yasiyo rasmi,” Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa alisema.
Kwa mujibu wa Bw. Sadiki waliokuwa wamejenga nyumba za miti na udongo zikaathiriwa na mabomu, watafidiwa kwa kujengewa nyumba za matofali ili kuepuka kuendelea kuharibu mazingira.
“Hapa ndiyo kufa kufaana, maana wale waliojenga kwa kutumia miti, hatuwezi kuwafidia kwa kujenga tena kwa miti maana itakuwa tunaendeleza uharibifu wa mazingira. Hivyo gharama zote zitabebwa na manispaa,” Bw. Sadick alisema.
Hivi sasa, timu ya wataalamu wa ardhi wako katika kukamilisha mchakato wa awamu wa pili wa kutathimini nyumba 72 ambazo ziliharibiwa kabisa na milipuko ya mabomu.
Tayari Suma JKT wameshaanza kununua saruji na kufyatua matofali maeneo ya Gongolamboto pamoja na kusaga kokoto maeneo ya kunduchi kwa ajili ya fidia ya ujenzi huo wa nyumba.
Tofauti na watu wanavyowaponda Suma JKT, Bw. Sadick alisema kuwa kitengo cha Suma JKT kina wahandisi waliobobea wenye shahada za juu za uhandisi ambapo serikali huwatumia katika ujenzi wa majengo mengi ya serikali.
“Suma JKT wana wataalamu waliobobea kweli kweli na katika hili hata vifaa watakavyotumia kujengea ni vya hali ya juu. Madhalani watatumia mabati ya geji 28, wanafyatua matofali kati ya 30-35 kwa mfuko wa saruji,” Bw. Sadick alisema.
a haraka ili kuwezesha watu wapate mali zao kwa haraka na hali ya kimaisha iweze kurudi kama kawaida.
TUNAIPONGEZA SERIKALI KWA UAMUZI HUO NA TUNAWAOMBA HAO SUMA JKT WAKAZIDISHA BIDII WAMALIZE HARAKA, ILI WATU WAEPUKANE NA MADHILA YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA,NA PIA HONGERA KWA SERIKALI KUWAFIDIA HAO WA MABONDENI NI UAMUZI WA BUSARA, ILA TUNAOMBA PIA WAWEZE KUWAPA FIDIA WAPANGAJI WALIOATHIKA NA HAYO MABOMU, MAANA WAMEPOTEZA MALI ZAO WENGINE KARIBU ZOTE KM,LUNINGA,RADIO,VITANDA,VITI,MAKOCHAI,NGUONA VYOMBO VYOTE VYA KUPIKIA NK,KUNA BAADHI WAMEWEZA KUPOTEZA NUSU YA VIFAA VYAO, WAANGLIE NA HILO WENGI WETU HATUNA UTARATIBUWA KUWA NA BIMA,MAANA BIMA NAO NI UWEZO HILO JAMBO NI DHARURA HAKULIKUSUDIA WALA HAKULIFANYA KWA UZEMBE WAKE MTU NI JANGA LA TAIFA,LIANAGALIWE HILO NAO WAWAFIDIE
ReplyDelete