18 April 2011

Viongozi wa dini wadaiwa kujipenyeza kwenye siasa

Na Charles Mwakipesile, Mbeya

MKUU wa huduma ya Sauti ya Uponyaji ya Mjini Morogoro, Bw. Joshua Mwantyala amewaonya viongozi wa dini wakiwemo maaskofu kutokana na kile alichodai tabia yao
ya kuacha kuhubiri injili na kuamua kujiingiza kwenye siasa kutokana na matamshi yao yenye utata ambayo amesema mwisho wake ni maafa makubwa.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi, Bw. Mwantyala anayejitaja kama nabii,alisema kuwa hatari kubwa kuona katika siku za sasa viongozi wa dini wamevamia siasa.

"Mungu alinionyesha maono mengi kwa ajili ya Tanzania ambapo alisema wazi kuwa amechukizwa na viongozi wengi wa kanisa kujiingiza kwenye siasa na kujificha na mgongo wa kujifanya wao ni viongozi wenye kuaminika, na hivyo kila wanachosema kitapokelewa na watu wengi nawataka waacha tabia hiyo," alisema Bw. Mwantyala ambaye hivi karibuni amekuwa akikusanya mamia ya watu katika maombezi yake anayotumia maji ya kunyunyiza kinywani kwa ajili ya kuondoa magonjwa sugu ukiwemo Ukimwi.

Akionesha kuumizwa na tabia hiyo alisema kuwa viongozi wa kanisa hawana budi kurudi makanisani na kuendelea na kazi yao ya kuhubiri injili tofauti na ilivyo sasa ambapo wameonekana dhahiri kuwa wao ni sehemu ya matatizo yaliyopo nchini.

Alisema kuwa ni wazi kuwa viongozi wa dini wanayo dhamana kubwa  ya kuhakikisha kunakuwa na amani na utulivu mkubwa nchini  kutokana na maombi na makalipio yanayotolewa na viongozi safi wa Kanisa ambao wanaaminika kuwa wakisema kitu wanakuwa wanamaanianisha jambo kubwa kulingana na maono na unabii  wanaokuwa wameagizwa na Mungu.

Bw. Mwantyala alisema kuwa Mungu alimwambia wazi kuwa wapo viongozi wengi wa dini wamejiingiza kwenye vyama vya siasa kwa siri ambapo wamekuwa nyuma ya viongozi watendaji wa vyama hali ambayo alisema kuwa ni hatari kubwa kwa ajili ya kutunza amani na utulivu na hivyo Watanzania kushinda umaskini na kupata maisha bora.

Alisema kuwa kinachotakiwa kwa sasa ni kwa walengwa hao kuamua kurudi makanisani na kufanya kazi waliyoitiwa na kisha kubaki kuwa washauri wa viongozi wa siasa ili wawe na subira katika kila wanalolifanya sanjali na kuachana na maamuzi yanayoweza kulipeleka Taifa kwenye umwagaji wa damu.

Hata hivyo, alisema kuwa ni wazi kabisa kuwa kama Nabii alioneshwa wazi kuwa kama viongozi hao wa dini watakaidi kuachana na siasa na kurudi madhabahuni, alisema kuwa iko hatari kubwa ya Taifa kuingia katika machafuko makubwa ambapo alisema kuwa vurugu zinazoanzia kanisani zina maafa makubwa.

Alisema kuwa yeye alipewa ufunuo  na Mungu  kuhusu  uongozi wa Rais Kikwete ambapo kila anapopata nafasi amekuwa akifanya kazi ya kuufikisha  kwa njia anazoona zinafaa na hivyo aliwashauri  viongozi wenzake wa dini kuhakikisha wanatumia wadhifa wao  kushauri serikali kila inapobidi.

"Hii ni nchi yetu hawa wenzangu wamejichanganya wenyewe kwa kuacha kufanya kazi isiyo ya kwao ambayo ni hata kubwa wao nio wahubiri kama mimi kama wakitulia ni wazi kuwa Mungu atawapa ufunuo kwa ajili ya taifa ambao ukitolewa kwa hekima ni msaada mkubwa kwa Taifa, waache siasa, warudi makanisani," alisema bila kutaja jina hata moja.

Alisema vyama vya siasa vinapaswa kufanya mambo yao kwa hekima  kwa kutambua kuwa thamani ya Tanzania ni pamoja na mtanzania  ambaye amewekwa na Mungu ili afaidi amani na utulivu vilivypo nchini, si vurugu na hali ngumu ya Maisha ambayo watu wengi wanapitia.

2 comments:

  1. Kweli mkuu unayoyasema ndio yanatokea ndio maana watu hawataki hata ku comment wanajua wanatumwa, hata Rais aliongea baada ya uchaguzi lakina wengi walipinga na ni viongozi wa dini hao hao wa kwanza kukataa mimi pia nasema KAMA AMANI INGEPOTEA WAKATI WA UCHAGUZI HUU MPAKA SASA baadhi ya viongizi wa dini wanahusuka na wana la kujibu kwa mungu kwani wamekuwa wanAFIKI saana na kujificha mgongini kwa wanasiasa na waumini wao wanasupport hata kama ni vibaya..nashangaa siku hizi kikitokea kitu tu cha siasa lazima kwenye mahubiri ya jpili katika kanisa lolote liongelewe naona haina maana kwani sio kila kitu cha siasa kiongelewe,wengine mpaka wamefikia hatua wanasema wanatishiwa kuuwawa na wanasiasa nashangaa kwani ukifa kwa ajili ya siasa utaulizwa ila ukifa kwa ajila ya dini yako kama wewe ni mtu wa mungu huna hukumu..wao watoe tu ushauri sio kukakaa kwenye majukwaa ya dini kugeuza siasa kama wakitoa ushauri na wasiposikilizwa hawana dhambi sio wanavyong'ang'ania mbona hawakazanii matatizo kwenye sehemu zao husika tukiangalia kuna matatizo mengi kuliko ya siasa sema siasa inahusu zaidi umma.

    ReplyDelete
  2. Tumerudi kule kule tulikotoka kwenye kuonyeshana vidole, kupe, bepari, mnyonyaji na kufanya umaskini ni sifa. Nani analipa kodi ipasavyo,analipa deni la mikopo ya elimu,anatosheka na mshahara wake tu.Ukiona vijijini kuna hali ngumu ni sisi mjini ndio tuliokulekeza na tumejichimbia jijini tukidai umeme na maji. Utashangaa hata wabunge wanaanza vikao kwa kudai posho zaidi na saluti, viswanglish viingi eti katiba iandikwe kiswahili wakati wao wanasema 'dark market'.Katiba iandikwe kwa kugha ya kitaalamu kisha ifasiriwe.Istilahi zakiswahili katika sheria ni chache mno.

    ReplyDelete