04 April 2011

Vijana CCM wazidi kuraruana

Na Mwandishi Wetu

SIKU chache baada ya Baraza la Umoja wa Vijana CCM Mkoa wa Arusha kutangaza kumfukuza Mjumbe wa Baraza la Vijana Taifa, Mrisho Gambo, yeye ameibuka
jana kupinga uamuzi huo, akisema hawana mamlaka hayo.

Bw. Gumbo alivuliwa wadhifa huo kwa tuhuma za kuunga mkono vyama vya upinzani na kusababisha Jimbo la Arusha lichukuliwe na mbunge kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Hatua hiyo ilitangazwa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Arusha, James Millya, kuwa uamuzi wa kumfukuza umetokana na tuhuma na taarifa zenye ushahidi kuwa Gambo amekuwa ni kiini cha kukivuruga chama na kushawishi vijana wa CCM kuchagua upinzani.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Bw. Gumbo alisema, "Ninataka kuwafahamisha Watanzania wajue kuwa UVCCM-Arusha hawana mamlaka ya kikanuni wala kikatiba kunivua madaraka, nimeona nizungumze ili historia isije kusema nilifukuzwa".

Alisema yeye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa na mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa, kwa mantiki hiyo uteuzi wake wa mwisho unafanywa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na ambayo kwa mujibu wa Katiba ya CCM ndiyo yenye mamlaka ya kumvua uongozi.

Mbali na tamko hilo, Bw. Gumbo alisema anaandamwa ndani ya umoja huo kutokana na kauli yake kuwa kashfa za Richmond na Dowans zimeipunguzia CCM kura katika uchaguzi mkuu uliopita.

"Kabla ya kikao cha Vijana Arusha (kilichomvua wadhfa)nilipokea simu kwamba watanimaliza kutokana na kauli yangu kuwa 'Richmond na Dowans vimeiupunguzia kura CCM' hivyo watanishughulikia," alisema.

Alisema wakati kikao hicho hakijafanyika maamuzi dhidi yake yalikuwa yameshatolewa, hivyo kilifanyika wilayani Longido kwa ufadhili wa baadhi ya wanasiasa kuyabariki.

Alifafanua kuwa kikao hicho na kiliisha saa 2 usiku lakini maazimio yake aliyapata saa 9 mchana baada ya kikao chao cha kwanza kilichofanyika katika Hoteli ya Impala, mjini Arusha.

Kijana huyo ambaye amejitokeza waziwazi kupinga kauli za karibuni za viongozi wa jumuiya hiyo dhidi ya wastaafu wanaoikosoa CCM, alisema vitendo anavyofanyiwa ni njama za kumziba mdomo ili asiseme ukweli.

"Hoja kuu eti ilikuwa sikumpigia kura Batilda (Burian) lakini wanasahau kuwa kura ni siri na hakuna mwenye mamlaka ya kuhoji. Niliposikia hoja hiyo nikawauliza wana uthibitisho gani? Maana hata mke wangu sikwenda naye hivyo wao wamejuaje?.

"Tatizo ukiwa mpiga kelele dhidi ya ufisadi basi unatafutiwa namna yoyote ya kumalizwa. Umefika wakati wa kuacha kufanya kazi za watu na kufanya kazi za umma; ningependa vijana ndani ya CCM wajue hilo, Watanzania wa sasa ni wa DOT COM, alisema.

Alitoa rai kuwa wote wanaotuhumiwa wa kashfa za Richmond na Dowans washughulikiwe, hakuna haja ya kuumauma maneno. "Ukiwa mnafiki kijana, basi utakuwa mchawi ukizeeka. Mimi nitasema ukweli daima, fitna kwangu mwiko," alisema.

8 comments:

  1. Pole kijana mwenzetu Gumbo. Haya ni matokeo tu ya mitandao inayoendelea CCM. Nadhani Millya anafahamika ni mtandao wa kigogo mmojawapo wa CCM mtuhumiwa wa Richmond. Na huyu huyu ndiye aliyekuwa mfadhili mkubwa wa Dk. Batilda. Atakayelaumu kuanguka kwa Batilda anakosea sana kwani Dk. Batilda alikuwa mtandao wa Mafisadi kwa vyovyote vile hata kwa kutumia mbinu gani asingeweza kushinda ubunge mjini Arusha iwe iwavyo. Kwanza yeye alifahamika ameolewa Zanzibar halafu pili yeye ni mwanamke. Kule Kaskazini wanadharau saaana kuongozwa na wanawake. Kwa hiyo kumlaumu kijana wa watu Gumbo ni kumwonea kwani kura yake moja isingemwezesha Batilda kushinda. UVCCM ni kama kivuli cha vigogo fulani fulani kwa hiyo utetezi wao na kelele zao ni kwa maslahi ya wabwana zao. Halafu uchaguzi wa Arusha hata viongozi wakuu wa CCM mkoa walikuwa wanampinga Dk. Batilda kwa sababu aliingia Arusha kwa vishindo alikuwa anadharau hata kamati ya siasa ya mkoa kwa kumtegemea zaidi Lowassa kauli iliyotolewa na Mary Chatanda Kati wa CCM (M) baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa huyu naye alikuwa anampinga Dk. batilda kwa nguvu zote. kwa hiyo vita vyake vilikuwa hata kwenye Chama chake. Leo hii lawama isiende kwa mtu mmoja. CCM kwa ujumla vueni gamba kama alivyoshauri Mwenyekiti Taifa. Si wakati wa kutafuta mchaw. Kwani kililacho ki nguoni.

    ReplyDelete
  2. CCM ACHENI MAWAZO MGANDO WATU WANAJUA WACHOTAKA MSIWACHAGULIE, MSIENDESHE NCHI KAMA FAMILA ZENU NYUMBANI MTALETA MACHAFUKO BADILIKENI HARAKA JIFUNZENI KWA KANU MTAKUWA CHAMA CHA UPINZANI MUDA SI MREFU!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. kikwete afe na ccm yake watanzania tupone

    ReplyDelete
  4. chadema jiandaen kuchukua nchi cczm hiyoooo inakufa

    ReplyDelete
  5. kama raisi ni Kikwete tusitegemee maajabu hawezi kubadilisha kitu kwanza kabanwa na watu wenye fedha na ameingia kwenye huo mtego na kwa ujumla hali ilipo sasa uwezo wake wa kawaida ni mdogo kupata majibu muafaka ya kuiweka nchi katika hali ya utulivu watu wamekata tamaa kwa kiwango cha juu sana inahitaji nguvu za ziada kuwarudisha imani na kwa kasi ALIYONAYO HAWEZI MBAYA ZAIDI HAGUSI MATATIZO YA WANANCHI NA KERO ZINAZOWAUMIZA.

    ReplyDelete
  6. CHAMA HUZALIWA, HUKUA, HUZEEKA THEN KUFA", CCM SASA KINAKUFA. MAFISADI WANAKIUUA AU WATASABABISH VURUGU KWA GHARAMA YOYOTE MAANA WAMEFANYA MADUDU MENGI, UKIPATIKANA UONGOZI MAKINI WENYE KUFATA SHERIA NA USIOTOKANA NA UFISADI JELA INAWAHUSU, NA WATAFILISIWA. KWAHIYO YANAYOENDELEA NDANI YA UVCCM NI MAFISADI WANATAPATAPA. WATANZANIA TUUNGANE HAWA NDIO WANAOTUTIA UMASKINI. WAMEWEKA UONGOZI NA WANASHIRIKIANA NAO KUTUFILISI MFANO DOWANS. SHIME WATZ, SAA YA MWAMKO NI SASA.

    ReplyDelete
  7. Huyu Mkwere mimi nilifanya kazi na mdogo wake kule Mamlaka ya Pamba Mwanza miaka hiyo. Alikuwa akija kwa mdogo wake yeye na sketi sketi na yeye! Hata huyo Mohammed alifukuzwa kazi kutokana na tabia za kihuni alizokuwa nazo. Alipelekwa Pemba kuwa katibu msaidizi wa CCM (alisomea kilimo!) huko nako wake za watu ndio kilichomfanya atolewe baruti. Toka wakati huo yuko Bagamoyo kama Katibu. Hawa wanatoka ukoo unaoabudu chini kama sala ya bwana! Mungu ajalie afe kabla ya muda kwisha maana ameshatuharibia nchi vya kutosha. Hapa tulipofikia tunahitaji Raisi mzalendo atakayekamata hawa wahalifu wote, kuondoa kazini wezi wote, kufumua jeshi, polisi na usalama wa taifa na kuunda upya, ataifishe mali zote za wizi, awaadhibu hata wale walionza kuiba toka awamu ya pili, afute mikataba yote ya kifisadi, afute posho za wabunge na kurudisha mfumo wa zamani wa kuhudumia wabunge, anzishe viwanda na mashirika ya uma na kuweka masharti ya kuyaendesha, awakamate siku ya kwanza Kikwete, Lowassa, Rostam, Chenge, Karamagi, Mustafa Nyanganyi, Generali Mboma, Mkapa, Yona, Manji, Njolaay, mawaziri wote wenye utajii usio na maelezo, mahakimu na majaji wote waliotoa hukumu zenye utata hasa kuhusu madawa ya kulevya, mgombea binafsi, Askari walioua watu migodini, arusha na kwingineko, Basil Mramba, Serukamba, waliouwa mradi wa mabasi ya watoto wa shule, waliouza mashirika ya umma kwa bei ya kutupa, walionunua mashirika ya umma wakayahujumu, wezi wa hela za halmashauri, n.k.

    ReplyDelete
  8. Mungu Ibariki Tanzania!

    ReplyDelete