18 April 2011

Sumaye hakutajwa orodha ya mafisadi-CHADEMA

Na Tumaini Makene

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimetoa ufafanuzi juu ya orodha mpya ya ufisadi na mafisadi nchini, iliyosomwa juzi Mjini Tabora na Katibu Mkuu wa
chama hicho, ikiwa ni mwendelezo wa ile iliyotolewa mwaka 2007, Mwembeyanga, Dar es Salaam.

CHADEMA kimelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya taarifa ya baadhi ya vyombo vya habari jana kumnukuu Dkt. Slaa akisema kuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Bw. Fredrick Sumaye ni mmoja wa watuhumiwa wa ufisadi nchini, kwa mujibu katika orodha hiyo mpya.

Akizungumza jana Dar es Salaam na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni, Bw. Kigaila Benson, alisema kuwa wamelazimika kufafanua jambo hilo kwani hawataki kumtuhumu mtu bila kuwa na ushahidi wa tuhuma hizo, kwani kufanya
hivyo haingekuwa sahihi.

"Hili suala tumeamua kulifanyia ufafanuzi kwa sababu hatutaki wala hatuwezi kumtuhumu mtu au watu bila kuwa na ushahidi, kama mnavyojua sisi tunapoamua kusema fulani na fulani ni fisadi huwa tunaweka ushahidi bayana, kwa maana kuutaja ufisadi
waliofanya, si maneno matupu.

"Sasa imeandikwa kuwa katibu mkuu wetu Dkt. Slaa amemtaja Sumaye kuwa ni mmoja wa walioko katika orodha mpya ya mafisadi, hii si kweli, katika orodha hiyo hatukumtaja...hatusemi kuwa Sumaye ni fisadi au si fisadi, tunachosema ni kuwa sisi hatujamtaja katika orodha yetu.

"Kama kuna mtu anao ushahidi juu ya ufisadi wake anaweza kumtaja, hata sisi siku tukipata ushahidi juu ya Sumaye tutamtaja ...asubuhi nimeongea na Dkt. Slaa na Marando
(Mabere) wanasema Sumaye hakutajwa katika orodha, mazingira ambayo Dkt. Slaa alimzungumza Sumaye hayakunukuliwa sahihi," alisema Bw. Benson.

Aliongeza kuwa Dkt. Slaa alitaja jina la Bw. Sumaye alipokuwa akisema kuwa mafisadi na ufisadi ambao ameutaja mara kwa mara haujali dini, uhusiano, kabila, rangi wala umri wa mtu, hivyo akatolea mfano jinsi alivyowahi kumshambulia waziri mkuu huyo
mstaafu ambaye anatoka naye eneo moja huko Arusha, wakati akiwa madarakani kwa kushindwa kudhibiti ufisadi serikalini.

Bw. Benson pia alizungumzia kauli iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri ya Taifa (NEC) ya CCM, Bw. Nape Nnauye kuwa kuna vyama vya upinzani vimetumwa na mafisadi kumchafua Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, huku pia akidai kuwa kuna
wanasiasa wa upinzani wametumwa Tabora kufanya kazi hiyo hiyo.

"Unajua kitu kimoja ambacho mtu mwenye akili hawezi kuwaelewa CCM, hususan wanapoamua kutuhumu, wanaimba sana ngonjera. Unapoamua kusema kuwa kuna mafisadi wanatumia vyama vya upinzani kumchafua rais, ili ueleweke na kuaminika unawataja hao mafisadi
au huyo fisadi na vyama au chama kinachotumika.

"Ndiyo maana sisi tunapenda kuwaonesha njia sahihi ili wajikosoe vizuri, tukitaja mafisadi tunaonesha na ufisadi wao, hatubahatishi, sasa wao wanaimba tu ooh tunawapatia mafisadi siku tisini wajiuzulu lakini hawana ubavu wa kuwasema kwa
majina hao mafisadi ni akina nani na ufisadi wao uko wapi na wanachukua hatua gani za kisheria juu ya ufisadi wao.

"Tena sasa wanataka kuleta utamaduni mbaya sana ambao utatengeneza mwanya kwa watu walioko madarakani kufanya ufisadi maana wanajua wataambiwa wajiuzulu tu, hakutakuwa na hatua za kisheria juu ya yao, tulitegemea kwa chama chenye serikali kama CCM, kuiagiza serikali kuchukua hatua si kulalamika au kuimba ngonjera kama wanavyofanya sasa."

Bw. Benson alisema kuwa si sahihi watu wanaotuhumiwa ufisadi katika chama kinachounda serikali, huku wakiwa na dhamana ya uongozi sehemu zote mbili, kuachia nafasi zao ndani ya chama husika pekee, badala ya kuchunguzwa, kisha kufikishwa
mahakamani kwa ajili ya hatua za kisheria.

"Alitakiwa ataje jina la huyo fisadi au mafisadi na hivyo vyama vya upinzani. Pia fisadi ni mwizi, amefilisi taifa, raslimali za nchi sasa unaposema ajiuzulu nini kinafuata sasa, mwizi anakamatwa, mwizi hasemwi tu, sisi hatuna serikali sasa, lakini
tumewataja, hawa wana serikali mbona hawachukui hatua."

Juzi katika mkutano wake wa ujenzi wa chama hicho mkoani Tabora, Dkt. Slaa akiwa na pamoja makada wengine wa chama hicho, wakiwemo wanasheria Profesa Abdalla Safari na Mabere Marando pamoja na baadhi ya wakurugenzi na maofisa wa chama hicho walitaja
orodha ya watuhumiwa wa ufisadi nchini.

Dkt. Slaa ambaye aliwahi kutoa orodha aliyoita ya aibu ya watuhumiwa 11 wa ufisadi mkubwa unaolifilisi taifa, mwaka 2007, juzi aliongeza majina mengine matatu, ambapo alimtaja Dkt. John Magufuli kuhusiana na uuzaji wa nyumba za serikali, Bw. Phillip Mangula na Dkt. John Malecela kuhusiana na Fedha za EPA, huku
akimtaja Rais Kikwete kwa kushindwa kuwachukulia hatua mafisadi na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, katika uuzaji wa nyumba za serikali bila kufuata utaratibu. 

21 comments:

  1. jamani waandishi mbona mnakurupuka sana kwann msisikilize vitu kwa umakini? kama vitu hamna uhakika msiwe mnakurupuka tu tanzania daima walimuandika sumaye naye katajwa kuweni waangalifu mbona mwananchi hawakutaja kabisa? coz wako makini acheni kukurupuka tambueni nyie mwaweza kuharibu hata amani katika taifa letu msipokuwa makini ona sasa mnamtuhumu mtu asiye kuwepo? hatahivyo nilishangaa kumuona coz kunarafiki yangu alikuwepo kwenye huo mkutano alinitajia wengine hakumtaja sumaye.this is shem fanyeni kazi yenu kwa maadili na siyo ushabiki wa kisiasa mtatuvurugia amani yetu.

    ReplyDelete
  2. Mtu muongo na mropokaji husahau kila mara alilosema,Slaa anaimba sana. kwanza hakuna gazeti lililotaja majina zaidi ya la kwao wenyewe chadema.

    ReplyDelete
  3. Anonymous wa pili (12:50 am),mbona unakimbilia kumhukumu Dkt Slaa kabla hata aliowataja kuwa mafisadi hawajajitetea wenyewe?Unaposema hakuna gazeti lililoandika unarejea (refer) magazeti mangapi?Na kuna ubaya gani kutoa ufafanuzi iwapo zimejenga tafsiri tofauti?Kwanini warekebishe kwa Sumaye tu na sio Magufuli,Mangula au Malecela?

    Inawezakana Slaa anaimba sana,lakini kuimba si dhambi.Jiulize,anaimba kwa manufaa ya nani kama sio wanyonge wa Tanzania wanaokabwa na mafisadi?

    ReplyDelete
  4. Hiyo ndio Tanzania, hakuna kuongea maendeleo ila ni maneno tu. Ufisadi upo, wale walituhumiwa wachunguzwe na sheria ichukue mkondo. Unaweza kuhukumu mke na watoto kuwa wamefanya vibaya ila baba amefanya vizuri, mzungu mmoja alisema if you start you must finish

    ReplyDelete
  5. Slaa wakati mwingine ni mtu wa ajabu sana sana! Ni nani Tanzania asiyefahamu kwamba Sumaye naye ni fisadi wa kutupwa. Yaani kweli Slaa anaufunua utu wake wenye ngozi ya ukabila. Hajamtaja Sumaye kwa kuwa wanatoka naye kabila moja. Tena magazeti yanayotumika ni magazeti ya Chadema yakiwa na malengo maalum. Tunachosema ni kwamba Chadema itapata sifa ikisha kuwa na sura ya utaifa. Sera si tatizo lakini tatizo kubwa sana kwa Chadema ni wakiweza kuacha itikadi zao za kikabila na ueneo. Nchi hii haiwezi kuongozwa na watu wanaotoka sehemu moja ya nchi lazima nchi iwe balanced na hili ndilo linalowasaidia CCM. Dr Slaa ninamheshimu sana kwa sababu ya integrete yake anafikiri critically na ana uwezo kufanya analysis tatizo dhambi ya ukabila na ukanda ina haribu haiba yake nzima. Kama si yeye Dr Slaa basi itakuwa ni kundi linalomzunguka.

    ReplyDelete
  6. hongera Dr slaa, hongera Chadema...hivyo ndivyo tutaipata tanzania mpya yenye neema tele!

    ReplyDelete
  7. KAZI YA KUTAJA MAFISADI CO YA DR SLAA PEKEYAKE KM UNAUSHAHIDI KWAMBA SUMAYE NAYE NIFISADI WA KUTUPWA PELEKA USHAHIDI MAHAKAMANI USISUBIRI DR SLAA ATAJE KWA NIABA YAKO.

    ReplyDelete
  8. I Love CDM, It does talk openly! I wish they had the government to clean up this country.

    How can PCCB, Police force, and other law enforcers keep quit and look!

    How shame for a CCM cadre come to us and say Slaa is working for same corrupt which he is againist to.

    Jesus said well, If a kingdom is againist to itself, it is split and will fall.

    ReplyDelete
  9. tumewachoka na mnajijua kuwa tumewachoka, unafiki na uzandiki mtupu, sasa tunaamini, kwa nini kanisa lilimtosa Slaa au ukipenda silaha kwanza hana hata huo mvuto, hata hao wanaojigonga kwake ni wizi mtupu.Chadema ni waongo wahuni, siuju kwakuwa wapiga disco wamezoea makelele, sasahivi haitupi tena shida twajua wanachotaka. nchi hii siyamajaribio tumekwisha jifunza kawadanganyeni wake zenu. CCM kama kawa kwenda mbele, tekeleza Ilani tuonane 2015.

    ReplyDelete
  10. mawazo yako yanafana na akili zako ndio maana hata jina lako hujataja, umejaa uccm kama kuku na vifaranga vyake, nahisi umetumwa na wezi wenzio wa ccm coz huoni hata namna taifa linavyoangamizwa na hao vibaka wawenzio wa ccm

    ReplyDelete
  11. Have gone through the Chadema/Benson's clarification on the subject, then to all above comments before finding myself automatically drawn to make mine for good!Let's not in the first part concentrate on which party is either pretty good or bad for rulling the state, rather zero in commenting on the facts on the ground in Tanzania. We are all (regardless of party affiliation) witnesses of the ever escalating corruption, bribes and looting practices major players being both top and junior central/local government officials, and some known business men/indian society. These gangs (Corrupts and looters)are well known to the Government executives and the general public even by names. Yet the state house at Magogoni backed by the rulling party has chosen to watch helplessly despite the country's economy and peace depletion as the result of such evils. State house/Executive's decision to watching helplessly in the name of lacking legal evidences to put the gangs under task is the shame at its best, as corrupts and looters' evidences are obvious/readily available and known even without employing the PCCB (white elephant)and alike. The consistency sleepy state house's behaviour leads any reasonable person to a conclusion that either the top exuctive or the rulling system as a whole is behind the gangs' pitty tippy tappy looty games. If hat is the case, then the top executive/whole rulling system re-arctecturing is neccessarry for good!. I therefore call upon all bonafide Tanzanians to stand firm for the overall country's positive change and not for the mere party's reshuffle done recently.

    ReplyDelete
  12. Tanzania inahitaji mtu anyeweza kuwatumikia watanzania na awe MWAMINIFU na MKWELI. Hatuangalii anatoka chama gani au dini gani. Kwa maana hiyo Slaa ameshashindwa kwani sifa hizo HANA. Historia yake imemshitaki kwa mambo matatu muhimu. "HANA UAMINIFU"
    1. Slaa,alishindwa kuwa mwaminifu kwa kushindwa kutimiza ahadi alizozitoa mbele ya Mungu, mbele ya Kanisa na mbele ya watu waliohudhuria misa ile. Kama mtu anasema hiki leo kwa Mungu, na kesho anambadirika hata Mungu, je atawatii watu na kuwa mwaminifu kwao? Tafakari.
    2. Slaa, baada ya kuacha upadre alioa.Lakini akashindwa kutekeleza hata kile kiapo chake na mkewe. Hata kama hawakuoana kanisani, lakini ndoa ni ndoa. Leo hii mke huyo anahudumiwa na nani? Slaa alimdanganya mkewe. Tafakari.
    3. Slaa, hakuishia hapo. Amediriki hata kuchukua mke wa mtu mwingine. Mme bado anaishi. Jamani tutafakari. Je leo hii kiapo anachotaka kuapa kukaa ikulu kweli ameshaongoka? Atakuwa mwaminifu kweli? Tafakari.
    Ukweli unauma lakini UNAWEKA HURU.
    Sidhani kama angekuwa hata na nguvu ya kumpatia kiongozi mwingine siku 90, kwani kwa maoni yangu na mtu yeyote mwenye akili timamu ni kwamba Slaa angekuwa anfahamu UDHAIFU wa mtu mwingine, kwani hata yeye yuko vile. Nadhani anaijua biblia. yesu anasema "Mtu anayemwacha mwenzi wake wa ndoa, naye atakuwa amefanya dhambi kwani atasababisha mwenzie atende uzinzi"

    ReplyDelete
  13. Mwanaharakati wa Kimarekani marehemu Malcolm X aliwahi kusema hivi" Faint hearts never win decisive battles" akiwa na maana kuwa watu wenye mioyo dhaifu hawawezi kushinda vita kikamilifu. HAO NDIO CCM. Maneno mengi, vitendo hakuna. UNAMPA MWIZI SIKU 90? WALALA HOI WANGAPI HUWA MNAWAPA SIKU HIZO?

    Huu ni utani katika kuendesha nchi. Jamani tuwe serious. Tunajenga misingi gani katika nchi hii?

    Rais Kikwete aliwahi kusema kuwa zamani mtu akikaguliwa na kukutwa ana pungufu ya fedha za serikali ambazo ziko chini ya dhamana yake, kulikuwa hakuna maswali. Anaitiwa polisi na kuchukuliwa hatua za kisheria. Sasa hizi 90 zinatoka wapi, kama si kulindana?

    Mimi ni Mtanzania naililia nchi yangu. Watanzania tusifanye makosa 2015. Tujaribu chama mbadala. Tunacho hivi sasa.

    NYOKA akijivua gamba anaotesha jingine, na anabaki kuwa nyoka, ni kitu hatari kwa uhai wa mwanadamu.Nyoka ni kumkimbia kwa usalama wako!

    ReplyDelete
  14. Kama CHADEMA wamewasingizia hao waliowataja kuwa mafisadi mbona hawajaenda mahakamani? Na we unayesema Dr. SLAA aende mahamani huelewi lolote, UFISADI ni kosa la jinai na kosa la jinai inayoshtaki ni JAMHURI (SERIKALI) sasa Dr. SLAA ni serikali? Kama huna hoja si lazima kuandika maona usitujazie utumbo.

    ReplyDelete
  15. i just cannot understand what Slaa is trying to tell this country which is an island of peace and tranquility amidst an ocean of chaos. If what he says has even a grain of teruth, why cant he go to the courts of law and sue the fisadis? Who or what is stopping him from doing that? Is he not aware of citizen's arrest that can be carried out? I am of the opinion that he is crying wolf just because he was rejected by the peace loving Tanzanians and now that his masters and financiers are screaming for their funds and donations he is looking for a scapegoat. poor Dr Slaa the ex-communicated so called priest. Imagine a person who was leading a congregation of beleivers and then turning his back on them just because of MONEYYYYYY
    during the visit of Pope Paul John II. If Dr Slaa was a ORIGINAL FISADI at that time, these fisadis of today can be safely called PHOTOCOPIES. Dr Slaa high time for you to retire and go back to your ORIGINAL WIFE.

    ReplyDelete
  16. Tanzania is not a peaceful country, in any sense. For those who are eating glutinously our money and resources, are the ones who think this country is a peaceful one.
    We huna uhakika wa kula hata mlo mmoja kwa siku, huna uhakika wa kusafiri na kufika nyumbani kwa muda unaotakiwa kwa ajili ya msongamano wa magari, wewe unishi kwenye tope la mbagala,tandika, keko, manzese, mwananyamala, una amani gani?
    wewe ukienda uwanjani iwe hata mashindano ya kula hushindi, unaamani gani
    wewe ndugu zako wanasoma shule za kata, wametoka na ziro wanataka kupata msaada wa kielimu ambao serikali inaweza kufanya, serikali inaajiri walimu watatu kwa vidato vinne, unaamani gani?
    wewe unataka kupeleka shule za kati ada milioni kadhaa wakati unashindwa wewe unamani gani
    Unapenda mke wako azalie hospitali nzuri lakini anazalia Temeka ama Mwananyamala analala kitanda kimoja na mwanamke mwenzake ama chini wewe unaamani gani?
    Slaa anatusaidia sana kufichua watu wanaotumia madaraka vibaya. Hivi ni mtu gani anaweza kukubali uchuro wa kuuza nyumba za serikali, mfano za mawaziri ama wakuu wa polisi kisha wakalala gesti house? hiyo pesa ingeajiri mwalimu? unauziwa nyumba kwa miloni tatu uzauza bilions kwa kuwa maeneo yote yalikuwa ni maeneo maalumy

    ReplyDelete
  17. NTECHI(UDSM)
    The facts don't require any support or any opposition, CCM is at its highest stage of decline and to God be the glory that we are throwing away slavery and adopting humanity.
    CHADEMA should continue bringing to the innocent Tanzanians the true picture of their country!They will fight but they will not win the battle.

    ReplyDelete
  18. WEWE ULIYEMCHOKA DR SLAA NI MMOJA WA HAYA MAJAMBAZI YA CCM....
    ULITAKIWA UMPENDE DR SLAA KWA KUIBUA WIZI HUU KWA TAIFA LA TANZANIA.
    WANANCHI WANAUCHUNGU MKUBWA NA PAMOJA NA JITIADA ZENU KUMTUKANA DR SLAA ZITAGONGA UKUTA MWAKA 2015.
    MUULIZE KIKWETE ANAJUA KILICHOTOKEA UCHAGUZI ULIOPITA.
    CHAMA CHA MAPINDUZI KINA WATU HODARI WATAKAOWEZA KUINGIA NA KULETA MABADILIKO MBALIMBALI, TATIZO KUNA WATU WANAZUIA VIPAJI VYA WENZAO NA WENGINE UDUGU NA WENGINE UKABILA/UDINI NA CHAMA HAKITAKI WACHAPAKAZI.
    MSIWATUKANE CHADEMA CCM INAHITAJI MABADILIKO ZAIDI NGAZI ZOTE...

    ReplyDelete
  19. Msirukeruke mada,tunachosema Sumaye hakutajwa na Slaa ndio tunapoona kioja,hivi kweli unapomshutumu Magufuli kwa ufisadi ati kwa kuuza nyumba za serikali kwa kushirikiana na Mkapa bila kumuhusisha na aliyekuwa mkuu wa Magufuli yaani waziri mkuu Sumaye hivi hii kweli inaingia akilini? Sumaye wananchi wa Arusha wanamjua vizuri na mali alizolimbikiza,nenda hapo uhuru road ukaone complex alizouziwa Sumaye.kuna wakati Sumaye alikuwa akipita mitaa ya Arusha anazomewa,halafu leo nyie Chadema mnatuambia nini? mmemsakama Kikwete fisadi lakini hamsemi ufisadi wake.wapuuzi nyie,nchi haitamilikiwa na ukabila na udini wenu. SUMAYE HASAFISHIKI BURE SLAA ANAJIDANGANYA KWA SABABU NI KABILA YAKE. TUNAWAJUA SIKU NYINGI.

    ReplyDelete
  20. Sio kwamba Sumae sio fisadi ila CHEDEMA hawana ushahidi kwa hiyo huwezi kukurupuka na kumtaja mtu eti ni fisadi akikupeleka mahakamani uthibitishe sijui utajibu nini.Watanzania inabidi tuamke na tuelimike.

    ReplyDelete
  21. Christ I hate blogging...you got all your rules and fucking codes and I can tell you right now, we got a hundred people working on it and you piss them off, they're going to do you the same.
    Case in point- WALALA HO...wtf....she's related to EVELLAVA ?
    Terrific.
    And they all are into KILYZA with OCTST- and THE ROCCE- ROKST?
    And that's right by MUNDST?
    So says YSCRO - CRISCRO and PORKELA and they got the BACEN- LA VIANDE
    with METMEATE?
    Are you kidding?
    You got boners, cocks, balls, ASPET all over the nets and you think we don't pick up on ASOCHER- ASETORS?
    SKESTE.
    RAFERST.
    LEMPORST.
    NTECHIS.
    In GESSIS?
    Between SUCCO- SUCTIM- INTALL, you got way too much HERMAKEL - LICATO....with OJUNNE.
    And yeah, it's about RGYCO - DINGSC- SCULLS.
    It's what "y'all" call PHONC- PORKMJ.
    And RAPOST- MANTH, are giving it all away with NAZI JERMAN.
    RELPHY?
    Is he related to DETQU?
    DASSAULT?
    ARCHSEA?
    Because if he is, they got every SEA imaginable with TED TOTS and DIANDUCT .
    Now , it's YOURTURR.
    " Assholes".

    ReplyDelete