Na Rehema Mohamed
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetaja mikoa 10 ambako yatafanyika maandamano ya Aprili 16 mwaka huu kushinikiza serikali
kubadili muswada wa katiba na uzingatie maoni ya wadau na kushirikisha umma.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mkuu wa operesheni ya maandamano hayo Bw. Singo Benson ambaye pia alitaka viongozi wa chama hicho watakaoyaongoza, alisema lengo lingine ni kushinikiza mswada huo uandikwe kwa lugha ya Kiswahili badala ya Kiingeleza.
Bw. Benson alisema suala lingine ni kutaka serikali kutoa muda kwa umma kabla ya muswada huo haujaenda bungeni kupitishwa.
Aliitaja mikoa itakayofanyika maandamano hayo kuwa ni Morogoro ambapo kiongoozi wa maandamano atakuwa Mbunge wa Mpanda mjini Bw. Said Arfi, Arusha Bw. Zitto Kabwe, Kigoma Bw. Ezekiel Wenje na mkoa Ruvuma yataongozwa na Bw. John Mnyika.
Mikoa mingine ni Dodoma yatakayoongozwa na Mbunge wa Arusha Bw. Godfrey Lema, Pwani Makamu mwenyekiti wa Chadema, Zanzaibar, Mtwara yatakayoongozwa na Bw. Mabere Marando, Tabora Bw. Willibod Slaa, Mbeya Bw. Freeman Mbowe pamoja na mkoa wa Kilimanjaro.
CHADEMA NI WACHOCHEZI WA VURUGU TU HAWANA LOLOTE.WATU WASHATAMBUA KUWA KINAONGOZWA NA KANISA.D... NI MOJA TU KWA HIYO HATA WAFANYE MAANDAMANO LENGO LAO KAMWE HALITATIMIA.SIO WATANZANIA WALE WA KUBURUZWA WATU WANAJUA YOTE YANAYOENDELEA.
ReplyDeleteAmma kweli la kuvunda halina ubani,hivi hawa watu wako na akili timamu?Nia na malengo yao ni kuupotosha umma kuwa wao ndio wana haki saaanna ya hiyo Katiba? huu ni muswada ni mwanzo wa mchakato wa Katiba mpya na wao wanalijuwa hilo likishapitishw bungeni ndio Kamati itateuliwa hapo muda wa kuijadili na watu kutoa maoni yao ya mfumo na vifungu visomekeje au muundo upi unatakiwa na itakuwa ni Nchi nzima na muda zaidi ya miezi 6 utakuwa wazi watu kutoa fikra na mawazo yao.Nia yao ni fujo na kuupotosha Umma kuwa muda ni mchache hv mnataka kumuhadaa nani?zaidi ya hao vibaraka wenu wanaowalipa pesa chafu kibao za kuandaa maanadamano yasiyo na Tija? Poleni viongozi kwa kuingia mtandao wa vurugu kwa maksudi kabisa.Muangalie mbinu zenu zikishazoeleka na kuwagunduwa kilicho nyuma ya pazia basi mmejimaliza wenyewe. Watu wanayo macho,masikio na akili timamu wanaona dunia ilivyo na inako elekea
ReplyDeleteWAJINGA NDIO WALIWAO SISI YETU MACHO MFUMO SASA NI KUKANUSHA,KUPINGA,KUANDAMANA MPK KIELEWEKE NK, NI UJINGA USIO MFANO TUWE MAKINI NA HAO WANAOTURUBUNI,WANAORUBUNIWA na WANAOWARUBUNI VIONGOZI.WAO YAO YANAWAENDEA NA KILA WANAPOTIMIZA HAYO NA POSHO ZAO ZINAONGEZEKA MARADUFU AKILI KICHWANI MWAKO
ReplyDeleteVulugu uchochezi mnao nyie wenyewe majumbani kwenu.Hakuna mtu anayechochea vurugu, maandamano ni lazima na tutawaunga nkono na tutaandamana kama na nyie mnataka nendeni mkaandamane nyumbani kwenu na wake zenu.Peopes power!!!!!!!!!! hakuna kulala mpaka kieleweke.
ReplyDeleteCCM MNACHEKESHA ETI CDM CHAMA CHA KANISA TUMESHAWASHTUKIA HATUDANGANYIK.MI NATAKA UNIJIBU SWAL MOJA KA CDM CHAMA CHA KANISA CHAMA CHA MSIKITI KIKO WP?ACHEN HZO BANA HATUDANGANYIK NG'O MLIANZA NA CUF MKAWACHAFUA WEE SA IV TUMEWASHTUKIA
ReplyDeleteSiamin kama bado mnautetea muswada eti uko sawa,kla m2 ameukataa si wanasheria,viongoz wa din wala wasom wote hawautak.kwanza umeandikwa kiingereza,hamjui kwamba mchakato mzur wa katiba ndo unazaa hyo katiba nzur!?nan mnataka awaambie nyie ccm muelewe?kwel dawa yenu maandamano ndo yanawafaa hadi mmevua gamba!na 2tawaunga mkono hata kama hela zinatoka kwa shetani.
ReplyDeleteswala la udini ni kichekesho mbona kuna vyama safu karibu nzima ni waislamu na bado hamuhoni kuwa ni udini tatizo la ccm ni kuwa na mawazo mgando mmejivua nguo wala sio magamba kwani mnatakiwa kuzikwa sio kuvua gamba nyoka ni nyoka abadiliki tabia ata kama anabadilisha gamba
ReplyDeleteHa ha ha ha aaaah!!! dduhh, mazi ya kwiza na nguvu yankisila yahomboke, Mhh, maji yakija na nguvu yapishe yapite ni mafuriko yanapita kwa muda tuu hayo,Sio maji ya mto hayo.
ReplyDeleteWaacheni waandamane kila siku hao hawana kazi,wao walisema katiba itapatikana ndani ya siku ndani ya siku mia,hiyo ingekuwa ya wananchi? hawakuandamana wakati Mkapa akikataa kubadili katiba,akiuza ardhi zenye madini,mashirika ya umma,akinunua ndege,rada leo wakisikia Kikwete kajamba maandamano. ni vyema Rais na viongozi wengine waachieni tu hao waandamane kila siku ila la muhimu maandamano yao yasiingilie haki ya watu wengine. KIKWETE YUPO HADI 2015 MTAKE MSITAKE.
ReplyDeletechadema tunawapa moyo endeleeni na ari hiyo tupo nyuma yenu, lazima tufanye maandamano hadi kieleweke.
ReplyDeleteKwani mna wasiwasi gani nyie CCM-mbona kelele zao zilisababisha tulioyaona kama vile;
ReplyDelete- serikali nzima ikavunjwa
- Waziri mkuu kajiuzulu
- Mawaziri waliokuwaandamizi wakajib kesi mahakamani
- Tukajua Epa, Richmond, Kagoda, deep green, Dowans
- Sekretariet imevunjwa
- Vijana Wakatukana Wazee
- Na mengine mengi.
Sasa kwa hayo yote yaliotokea bila wao tungeyajuaje. CCM sasa imekuwa ya watu wa bora liende. Watu wamechoka na nyinyi fungeni mikanda. Harafu kama mnaijua Amani vizuri mbona vijana wanatukana wazee.
Safari yenu imefika..kaeni mkao wa kuwa dei waka
CCM imeozaaaaa. nawashangaa sana mnaopinga maandamano. haya maandamano mnaoyapinga hamjui ni kitu gani Mfanyacho. Big up sana Chadema. tuko pamoja hadi kieleweke
ReplyDeletekwa mara ya kwanza tangu tupate uhuru kazi ya siasa ndio inafanyika sasa!!!!ni kelele kelele hizo hizo zimewafanya wajivue gamba..mwendo mdundo ndio kazi ya siasa.....chadema kaza mwendo tunataka tanzania iendeshhe kwa taratibu ambazo wote tunazitambua!!
ReplyDeleteNa at last wameitambua list of shame ile ya mwembeyanga eti wamewapa siku 90 wafisad waondoke..b4 walisema wanawasingizia..na bado mtakoma mbona,maandamano yanawakera nn kwan na nyie si muandamane aishi
ReplyDeleteNilikuwa nafikiria ni propaganda tu wale waliosema kuna pesa chafu inatoka nje ili kuleta vurugu hapa nchini kupitia vyama vya siasa. Haiingii akilini kuwa mtu anaweza kuitisha maadamano wakati huu wakati ndio mchakato wa kupata katiba unaanza. Sasa hivi tumeanza mchakato ambao lazima upate nguvu za kisheria. Watanzania wote hawawezi kuandika mswada. Lazima watu wachache waandike halafu wengine washiriki katika kuboresha kilichoandikwa. Viongozi wa chadema wamekuwa wakifanya kila liwezekanalo kuona mjadala hauendi vizuri badala yake kufanya upotoshaji. Sasa hivi inatakiwa kutolewa maoni ili kuboreshwa mswaada, sasa kama hayo maoni hayatachukuliwa na mtu au kikundi anaona kuwa hayo maoni ni muhimu, ndipo maandamano yanaweza kuitishwa. Haya siyo maoni ya katiba, ni maoni ya mswaada. Sasa naamini kuwa chadema mmelipwa kuimaliza nchi yetu. Kuandaa maandamano nchi nzima ni pesa nyingi, mnazitoa wapi? Na yale maandamano yalioanzia kanda ya ziwa na yalikuwa yawe kwa nchi mzima mbona hatuyasikii tena? Ningeshauri viongozi wa chadema kuwa na subira, bahati nzuri wengi ni wabunge, washiriki kuboresha mswaada ulioletwa bungeni, kama maoni yao hayatachuliwa hapo waitishe maadamano. Mimi pia nitawaunga mkono kwa sababu nakubaliana nao kuwa huu mswaada jinsi ulivyo lazima ufanyiwe marekebisho, na sijasikia serikali ikisema haitasikiliza na kulazimisha upite kama ulivyo. Sasa hii haraka ya kuandamana ya nini? Viongozi wa chadema wasipoangalia mtakosa mwelekeo. Kama ni kweli mmechukuwa pesa kuivuruga nchi na kuhakikisha haitawaliki, zirudisheni na Mungua atawabariki. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI CHADEMA IWEZE KUTANGULIZA MASLAHI YA NCHI.
ReplyDeleteMAANDAMANO HAYANA FAIDA HEEE??? NENDA UKAWAMBIE HAYO WATU WA MISRI AU TUNISIA KAMA HAWAJAKUCHEKA MPAKA UZIMIE.
ReplyDeleteWatangulize maslah ya wananch mara ngap?hv ccm wanatanguliza maslah ya wananch au mafisad?miaka 50 ccm imefanya nn la maana.wananch wanafanya kaz sana lkn hawafaidik umaskin unazd kukithr na kuwanufaisha mafisad ambao ndo nyie ccm..ccm imechokwa yan bora kumchagua shetan kuliko ccm yan imeoza afu mnavozidisha propaganda zenu mara udin,mara ukabila mara hela za marekan mnazid kujidhihirisha nyie ni waongo..CHADEMA TUITENI NAS TUTAITIKIA.
ReplyDeleteNi lini wapenzi na wanaCCM mtaacha maswala ya Udini? mnatukwaza sisi ambao familia zetu zimechanganyika kati ya Ukristo na Uislam. teteeni hoja. leo mnasema umejivua magamba je umeyaweka wapi? mbona bado yapo yanaonekana chumbani kwenu? Je ile hasara uliyoisababishia nchi na hayo magamba yatarudisha? fikiri ni watu wangapi wamekufa kutokana na kukosa dawa kwa sababu ya wizi wa Pesa za Radar?
ReplyDeleteAcheni unafiki,mbona watu walipomsema mkapa wakristo hawakusema niudini lakini akisemwa kikwete eti ni ukristo unaonea uislamu tangu lini hii nchi haki ya mtu ikatambuliwa kwa dini yake sidhani katika nyakati hizikuna mtu anazuiwa kusoma eti kwa sababu ya imani yake,Tuacheni longo longo CCM lazima iwajibike MIAKA 50 bado watoto wanakalia matofali na sakafuni shuleni,mabilioni ya fedha yanatoweka kusikojulikana,miradi mingi ya barabara imesimama kisa pesa imetoweka CHADEMA kazeni nyie ndio kiranja wa nchi hii.
ReplyDelete