14 April 2011

Shitambala aanza kuwananga CHADEMA

Na Charles Mwakipesile, Mbeya

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) mkaoni Mbeya ambaye sasa amejiunga na CCM, Bw. Sambwee Shitambala
ametangaza kuibomoa ngome ya chama chake za zamani mkoani Mbeya Mbele ya Mjumbe wa Kudumu wa Kamati Kuu, Dkt. John Malecela huku akitamba kuwa kwa kadri alivyokijenga chama hicho ndivyo atavyokibomoa kwa mikono yake mwenyewe.

Alisema kuwa anathamini kwa sehemu kubwa heshima aliyopewa na uongozi wa chama ukiongozwa na Rais Kikwete, baada ya kuamua mwenyewe kujiunga na chama hicho kutokana na usaliti anaodai alifanyiwa na uongozi wa CHEDEMA.

Alisema kuwa viongozi hao badala ya kufanya kazi kwa maslahi yao wamekuwa wakifanya kazi kwa ajili ya kutafuta umaarufu wao wenyewe.

Alisema wakati akiwa katika chama hicho walikuwa wakifanya kampeni kwa kutangaza wazi kuwa wakiingia madarakani watahakikisha kuwa  wanaendesha nchi katika hali ya amani na utulivu, lengo likiwa ni kuwaunganisha Watanzania na kujipatia maendeleo yao wenyewe pasipo kufanya vurugu hali ambayo alisema kuwa imekuwa tofauti na  makubaliano hayo.

Bw. Shitambala alisema kuwa kutokana na kuwa mpiganaji na msomi wa sheria alishangaa kuona viongozi hao ambao wengi wao ameshiriki kuwapa ubunge wakigeuza ajenda na kuamua kuanzisha maandamano nchi nzima na kutoka nje bungeni wakati Rais Kikwete akihutubia hali ambayo alisema ni utovu mkubwa wa nidhamu.

"Hatukukubaliana kufanya maandamano ya kuvunja amani wala  hatukuwatuma waende wakatoke bungeni na kisha kurudi ukumbini kwa  kujadili hotuba ya rais, nawaambia ndugu zangu hii ni sababu kubwa iliyonifanya nikaamua kuondoka katika chama hicho.

Alisema kuwa CHADEMA ni chama chenye watu wasioweza kufikiri kwa haraka kutokana na ukweli kuwa Watanzania wanazo akili za kutosha kujitambua na kutoyumbishwa wala kuamuliwa juu ya amani ya nchi yao.

19 comments:

  1. mfa maji daima haachi kutapatapa,shitambala ni Yuda Eskariot msaliti wa yesu,so itafika muda ataishia kujinyonga kutokana kuwa kaingia wrong side.uchafu wa ccm utamaliza tu

    ReplyDelete
  2. Kama sababu anayiotoa ndiyi hii; Hana tofauti na Tambwe Hiza aliyesema kuliko kurudi CCM bora nimlale mama yangu. Sasa karudi CCM sijui alimlala mama yake au la?

    Sababu anazozitoa ni ze ambazo CCM wanataka kuzisikia masikioni mwao. Hawezi kwa mfano kusema nimetoka Chadema sababu hawana uwezo wa kupambana na mafisadi. Sababu hizo CCM wala hawataki kuzisikia hata kama itakuwa kweli.

    Shitambala chukua talaka yako nenda.

    ReplyDelete
  3. Maamuzi uliyochukua my friend Shitambala ni maamuzi hasi,kama basi ulikerwa na Chadema ungeenda basi hata TPL tungekuelewa lakini kuhamia CCM ni kujiua mwenyewe.I TELL YOU MY DEAR YOU WILL NEVER ACHIEVE ANYTHING MORE!!CCM imefikia mwisho wewe unahamia huko nani aliyekudanganya jamani!!Any way so far you were unbearable and incuddled burden inside the party.

    ReplyDelete
  4. Umesema ukweli Shitambala,kaza buti ukiwa msomi wa sheria, wapiga disco waachie disco lao, watasema sana ukweli hatutaki kuichezea AMAN YETU. Kaza mwendo mpiganaji huku CCM ni kutazama maendeleo siyo Maandamano.

    ReplyDelete
  5. wewe shitambala ni mtu wa watu, umesema ukweli, na ukweli siku zote unauma, watasema sana lakini ukweli umukwishausema, sasa hao wapiga DISCO watatukana wamezoea makelele kama kawaida yao, wewe ni mtu wa sheria na unaijua. Kaza buti mwendo mdundo, USIRUDI NYUMA>

    ReplyDelete
  6. Acheni dharau...masuala ya kupiga Disco na chadema yanahusianaje? Bills si kitega uchumi kama vingine. Mbona CCM ina makada wengi tu wanaomiliki kumbi za starehe na Mahoteli? Mbona Gachuma anamiliki hoteli na ni kada wa ccm mnataka kusemaje? kama kila kiongozi akiambiwa atake biashara anzomiliki si tutaanza kukimbizana? tena wengi wana biashara haramu kabisa. Mbona Ronard Reagan, Rais wa zamani wa Makani alikua mtangazaji wa redio na Mwigizaji na akaiongoza Marekani kwa mafanikio makubwa? Ni ufinyu wa mawazo na uvivu wa kufiki tu unatuponza watanzania.
    Pia ni dharau na matusi kwa wasomi na wanazuoni ambao ni wanachama wa CHADEMA kujumuisha kwamba chadema ni kundi la wapiga disco.

    ReplyDelete
  7. we shitambala una fikra nyepesi. Unajua maana ya neno amani? Watanzania hatuna amani tena. Kilichobaki sasa ni utulivu, nao pia utatoweka kama hali ya maisha itaendelea hivi. We nenda kwa mafisadi wenzako.

    ReplyDelete
  8. Nawaomba hao wanashikilia maneno ya kuwa CCM kinakufa!!Andikeni kumbukumbu zenu tokea hii siku ya leo na ya siku ya juzi mlioinakili toka kwa hao mnaowaiga baada ya miaka 4.5 tukutane hapatena tuulizane nani kafa,nani kauguwa na nani yuko mahututi!!? Acheni utani hii chama kubwa na baadhi yenu malezi mlionayo hayana maadili mema nia na mdhumuni kutukana kwa hiyo mnajiegemeza chini ya bendera ya upinzani ili mutimize dhamira yenu ya Matusi. Poleni sana Shitambala sababu hizo alizotoa ni mwanzo tuu na ndogondogo,ila za msingi anazo atapasua jipu muda muafaka ukifika.

    ReplyDelete
  9. wewe hapo juu maishayako ni yako tu ulitoka tumboni kwa mama ukiwa mwenyewe na utazikwa pekeyako huyo mtanzania aliotaka chadema au ww umtete ni nani?wote hamna maana hata kidigo we mboe unamfahamu?baba yake ulikuwa unamfahamu?ukishalijua hilo ndio uropoke kajiunge na mboe club au sikuhizi wanaiita bilcana ukafanye kazi kwake kama unashida na maisha yanakluendea vibaya hakuna wa kukubeba jibebe mwenyewe kwama ni mwanaume nakupa pole sana

    ReplyDelete
  10. Nimekubali kweli Shitambala wewe ni Ndumilakuwili! Kesi za watu mahakamani zimekushinda baada ya kudai gharama na kuingia mitini bila kuonekana siku za mahakama! Unatafutwa kwa utapeli wa hela za watu! Umekimbilia kwenye siasa tukadhani wewe ni mtetezi wa wanyonge kumbe nako ni usanii mtupu! Baada ya kupewa hela na SISIEM na kuuza ushindi wa ubunge sasa unatudanganya kuwa chama kinahatarisha amani! Tunatia mashaka hata Degree yako ya sheria kama hukuchakachua kwani umekuwa muongo katika kila idara. Huko ulikokwenda nako utatapeli na kuishia mitini! Ni bora useme wewe ni msomi kwenye fani ya usanii na uchakachuaji tutakuelewa!

    ReplyDelete
  11. Nawashangaa sana wanaoshangaa Shitambala kurudu CCM, mie naona yeye ni sawa na yule ndege mdogo autwaye KUKU MAJI ambaye kurudi mtoni ndo halali yake.Yeye ni askari wa JWTZ, ilikuwaje aache bado kijana tu aende upinzani kama hakutumwa na anaowajua yeye. Hakuna lolote, hana kipya.

    ReplyDelete
  12. Shitambala hajakosea-kuwa mpinzania ni imani. Unaweza kuwa ccm bado ukawa mpinzani-mfano wao kina Mwakyembe. Yeye aende tuu salama ccm akaongeze nguvu. Chadema ina hazina ya vijana wasomi wengi-muda ukifika wataonekana.CCM wakianza kukosa Ruzuku tuu ndio watajua kama kweli wana wanachama.

    Mbeya wana CHADEMA msiwe na wasiwasi wapo viongozi sana ambao wana uwezo kuliko Shitambala watachukua nafasi. Wala msije mkadhani mmepoteza captain.

    Mapambano daima, nchi kwanza.Tanzania tunakupenda.

    ReplyDelete
  13. Mwandishi wa habari hii naye NOMA. Mbona hakuandika juu ya ZOMEA ZOMEA iliyokuwepo mkutanoni na baada ya hapo au ndo u CCM au uSHEMEJI!!

    ReplyDelete
  14. AKILI ZAKE NI SAWA NA ZA TAMBWE HIZA.....AMEAMUA KUACHA KUWA MMILIKI WA MBWA NA KUGEUKA MBWA....POLE SHITAMBALA....YOU WILL NEVER ACHIEVE WHAT YOU HAD ALREADY YOU HAD IN CHADEMA.....

    ReplyDelete
  15. shitamba karibu baba Nyumbani wewe ndio kamanda ambae uloujuwa ukweli halisi wa siasa uliona mbali ndio mana ukakimbia hicho chama cha kikabila cha kihuni na cha kibinafsi na kwa mtaji huu ccm iko makini hatutoshuhulishwa na hawa wapuuzi wachache ccm itashinda daima na nichma makini sana ndio mana mambo yake huwenda kisomi na kistarabu nyinyi chadema mefungua mbwa kuzunguruka mikoani sasa tuko nyuma yenu mtakiona cha moto mnakopita tuko nyuma mkiwahada wananchi sisi kazi yetu kusafisha uwongo wenu mbinu zenu zinajulikana kazi uwongo na fitina tu chama cha wajanja wachache

    ReplyDelete
  16. sambwee shitambala daaaah kumbe wanasiasa wanawafanya wananchi vikatuni eeeeeh hakika cjui wangapi wataingia peponi wawe wa ccm chadema cuf tlp udp wota siwatakiiii kwendeni zenu uko na kelele zenu sheeeenzy taipu

    ReplyDelete
  17. PUMBA TUPU CCM NA CHADEMA WOTE WEZI HAO WANAGAWANA MAPESA BUNGENI WAKIJA KWETU WANAPIGA FIRIMBI ZA KUTUKANNANA NA BAADAYE WANTUACHA TUNAPIGANA. KAFIENI MBELE HUKO NA MAJINGA YENU AMBAYO CHADEMA IKISEMWA UTAFIKIRI WAMETIWA DOLE MKUND...

    ReplyDelete
  18. Shitambala ulizoea kuuza ubunge kwa ccm, baada ya ile hela kuisha umeamua kuwarudia. Pole sana.

    ReplyDelete
  19. SHITAMBALAAAAAAAAAA MGONJWA HUYO THE WORLD IS CHANGING IN POSTIVE WAY.WATU WANAZALIWA NA AKILI NYINGI NA HATUOGOPI MTU HATA HUYO MWEZI MWENZIO KIKWETE HATUMWOGOPI.ATAKUWA KAMA MWENZAKE WA VORY COAST.CCM INAUA NNCHI HIYO.TUKIICHEKEA WATAZIDI KULINDANA MPAKA MWISHO.

    ReplyDelete