05 April 2011

Mmiliki AC Milan amponda Balotelli

MILAN, Italia

MMILIKI wa timu ya AC Milan, Silvio Berlusconi amekana vikali timu yake kumwania mshambuliaji wa Manchester City, Mario Balotelli.Rais huyo alisema jana
kuwa tabia za Balotelli, nje ya uwanja zinamsikitisha sana na akasema kuwa haziwezi kuendana na klabu hiyo.

Berlusconi ambaye ni Waziri Mkuu wa Italia, alisema kwa jinsi mfumo wa tabia ndani ya AC Milan ulivyo hadhani kama unaweza kuendana na Balotelli: “Tabia za hapa AC Milan sidhani kama zinaweza kukubaliana na tabia za Balotelli.

"Yeye ni kijana mdogo ambaye kwa sasa na hata wakati ujao anafanya mambo ya hovyo hovyo, lakini ngoja tuachane naye. Ila sidhani kama kwa tabia zake anaweza akatufaa," alisema.

No comments:

Post a Comment