*Yailaza Sri Lanka
MUMBAI, India
INDIA imetwaa Ubingwa wa Kriketi wa Dunia, baada ya kuifunga Sri Lanka kwa wiketi 277-4 kwa 274-6 katika mechi ya fainali iliyochezwa katika Uwanja wa
Wankhede juzi mjini Mumbai.
Ushindi huo wa kwanza tangu mwaka 1983 ulizua nderemo, vifijo na shangwe nchini India inayofahamika kuwa na uwendawazimu wa mchezo huo katika bara la Asia.
Mchezaji wa Sri Lanka, Mahela Jayawardene alicheza vizuri na kuisaidia timu yake kupata alama 103 katika mipigo 91 katika Overs za mwisho na kupata alama 274-6 mjini Mumbai.
India haikuwa na wachezaji wake nyota, Virender Sehwag na Sachin Tendulkar, lakini Gautam Gambhir na Mahendra Dhoni waliimarisha timu katika mitupo.
Gambhir alitolewa nje akiwa na 97, lakini nahodha Dhoni akiwa na 91 bila kutolewa aliisaidia timu kutofungwa na ikashinda huku ikiwa na akiba ya mipira 10 ya kurusha.
Nahodha huyo, hakuwa katika kiwango cha juu katika mashindano hayo lakini alicheza kwa kujitolea maisha katika fainali na kuisaidia timu kuibuka na ushindi na kufanya mashabiki kulipuka kwa furaha uwanjani na sehemu mbalimbalia, ambako walikuwa wakifuatilia kwenye runinga.
Ilikuwa ni mechi iliyokuwa na ushindani mkubwa, lakini ni India ilikuja kuibuka na ushindi.
Washindi wengine waliowahi kutwaa taji hilo na miaka yao ni kama ifuatavyo: 1975: West Indies, 1979: West Indies, 1983: India 1987: Australia, 1992: Pakistan 1996: Sri Lanka, 1999: Australia, 2003 na 2007.
No comments:
Post a Comment