Na Addolph Bruno
BONDIA Maneno Osward 'Mtambo wa Gongo' amefanikiwa kumchapa Robert Mroso 'Cobra' wa Arusha kwa pointi 98-97 katika pambano lao lisilo la ubingwa lililofanyika
juzi katika Ukumbi wa Amana Ilala, Dar es Salaam.
Pambano hilo ambalo lilikuwa la kg. 72 uzani wa kati (middle) raundi 10 lilikua na upinzani mkali ingawa, Osward anayemzidi Mroso kwa kg. mbili alimwotea katika raundi ya tatu na nne.
Katika pambano mabondia wote walianza kwa nguvu sawa katika raundi ya kwanza na ya pili, ambapo kwenye raundi ya tatu na ya nne, Mroso alionekana kuzidiwa na kumpa nafasi mpinzani wake kushinda.
Ushindi wa Oswald ulionekana dhahiri katika raundi ya tano baada ya kumrushia konde nzito Mroso, hadi kupasuka juu ya jicho na kusababisha kuvuja damu nyingi.
Licha ya kupasuka huko, Mroso aligeuka na kuonesha upinzani mkali katika raundi zilizosalia wakirushiana makonde mazito kwa zamu na kusababisha majaji wa mchezo huo, Ali Bakari 'Chapion', Nassoro Kondo, Omari Yazidu na Sakwe Mtulya kutoa ushindi kwa Osward mchezo ulipomalizika.
No comments:
Post a Comment