04 April 2011

Hodgson afurahia West Brom kuifunga Liverpool

LONDON, Uingereza

KOCHA Roy Hodgson amesisitiza kuwa amefurahi mno kwa kuiongoza timu ya West Brom na kuibuka na ushindi dhidi ya timu yake ya zamani ya Liverpool.Hodgson alitimuliwa
na Reds Januari mwaka huu, baada ya kuiongoza kwa miezi sita lakini alikuja kuchukuliwa Baggies wiki tano baadaye.

Vijana wa Kenny Dalglish, ndiyo walioanza kuongoza kufunga goli katika mechi hiyo iliyochezwa juzi kupitia kwa Martin Skrtel katika Uwanja wa Hawthorns lakini Chris Brunt, alikuja kufunga magoli mawili kwa penalti na kuipatia ushindi timu yake.

Hodgson alisema kuwa yeye alimalizana na waajiri wake wa zamani na kwamba amefurahia timu yake mpya kuibuka na ushindi.

Alisema: "Nimepata furaha ya ziada kwa kuifunga Liverpool. Niliongeza marafiki wengi sana nikiwa Liverpool.

"Nina muda mwingi sana kuwaheshimu wachezaji na timu ya makocha, wengi kati yao walifanya kazi na mimi na tulifanya kazi kwa uaminifu mkubwa.

Alisema anafurahi kuifunga Liverpool kwa kuwa si kitu ambacho kilizoeleka katika siku za nyuma.

Ushindi huo umeipaisha West Brom hadi katika naafasi ya 12 katika msimamo na Hodgson amefurahia uchezaji wa timu yake.Alisema: "Nimeridhishwa sana. Nimeridhishwa sana na uchezaji.

Alisema hata wapinzani wao walicheza soka nzuri sana, ukiondoa dakika 15 za kwanza.

"Tulianza kufungwa, ilikuwa ni kipindi kigumu katika mchezo. Lakini ilikuwa ni maendeleao makubwa kwa wachezaji kusahau kila kitu na kuendelea kucheza na kufunga magoli mawili.

"Magoli yote mawili ilikuwa ni matokeo ya presha kuwa iliwekwa kwenye goli la Liverpool na kusababisha makosa yaliyozaa penalti za magoli."

No comments:

Post a Comment