27 April 2011

Ferguson apiga mkwara wapinzani wake

BERLIN, Ujerumani

KOCHA Alex Ferguson, amewaambia wapinzani wake kuwa hakuna timu ambayo inaweza kuvunja ari ya vijana wake wa Manchester United.Manchester United jana
ilicheza mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Schalke 04 nchini Ujerumani, Real Madrid  au Barcelona mojawapo  itacheza fainali katika Uwanja wa Wembley Mei 28, mwaka huu.

Fergie ametamba kuwa kati ya wapinzani wake, hakuna ambaye anaweza kuzuia hamu yake ya kutaka kupata mafanikio ya kutwaa ubingwa wa Ulaya kwa mara ya nne.

Alisema: "Kuhusu ubora wa timu, unachokiona kama ilivyokuwa dhidi ya Everton Jumamosi, timu hii haitasinzia.

"Hakuna nafasi kabisa kwa timu hii kukata tamaa. Hakuna nafasi. Ina ubora mkubwa."

Kocha huo alisema mshambuliaji wake, Wayne Rooney amerejesha kiwango chake.

Mchezaji huyo mwenye miaka 25, jana alitarajiwa kucheza katika Uwanja wa Gelsenkirchen, ambao alitolewa kwa kadi nyekundu wakati akiwa katika timu ya taifa ya England kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2006, kutokana na kumchezea faulo mlinzi wa Ureno, Ricardo Carvalho.

Lakini Fergie anaamini kuwa sasa mchezaji huyo, amejua umuhimu wake katika uchezaji.

"Ninafikiri kwamba Rooney, zaidi ya yeyote amejua kuwa uchezaji ni kitu ambacho kila wakati kitapimwa kwa sababu kuna matarajio kwake.

No comments:

Post a Comment