Na Dunstan Bahai
VYAMA vya Wananchi (CUF) na Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) vimesema vina historia ya kuuchukia ufisadi na kwamba havina sababu ya kutumiwa na
mtu au kiongozi yoyote katika kufichua mafisadi wote.
Kauli hiyo ilikuwa ikijibu kauli iliyotolewa na Katibu wa Itikati na Uenezi wa
CCM Bw. Nape Nnauye jana kwenye baadhi ya vyombo vya habari.
Bw. Nnaye alinukuliwa akisema kwamba vyama hivyo vinatumiwa na pia ni mawakala wamafisadi waliomo ndani ya CCM katika kumchafua na kumpaka matope Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.
Akizungumza na Majira jana, Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba, alisema
kuwa amestaajabishwa na kauli hiyo ya Bw. Nnauye kwani wao wamekuwa mstari wa
mbele na wanayo historia ya kutangaza na kuwafichua mafisadi nchini.
“Chama chetu kina historia ya kuchukia ufisadi, na tumekuwa mstari wa mbele
katika kutangaza sera zetu zikiwemo za kuuchukia ufisadi kama ule wa manunuzi ya
rada, ndege ya Rais, mikataba mibovu ya madini, EPA, IPTL na ufisadi wa ina
yoyote hiyo… na mstaajabu huyu kijana kama kweli ametoa hiyo kauli,” alisema
Profesa Lipumba.
Alisema kuwa hakuna kiongozi au mtu yoyote atakayewatumia wao kama chama, kama
mawakala wa kuchafua watu wengine kwani chama chake kinajinadi kwa sera zake na
hata masuala ya ufisadi nayo yamo kwenye sera za chama chao.
Akizungumza kwa niaba ya CHADEMA, Katibu Mtendaji wa chama hicho, Bw. Victor
Kimesele alisema kwanza Bw. Nnauye siyo saizi yake na kwamba hiyo kauli ni ya mfa maji.
“Huyu kwanza siyo saizi yangu, hizo kauli ni za kutapatapa tu kwani Chadema
ilipowataja mafisadi haikutumwa wala kutumiwa na mtu na hata huyo Rais Kikwete
alikuwemo kwenye orodha ya mafisadi tuliowataja," alisema Bw. Kimesera.
Huku akiangua kicheko cha kuashiria kuidharau kauli hiyo ya Bw. Nnauye, Bw. Kimesele alisema kuwa Nnauye anaona hodari kuzungumza sana kwenye vyombo vya habari lakini spidi aliyoanza nayo itakwisha.
Kwa mujibu wa Bw. Kimesele, CHADEMA itaendelea kuwataja mafisadi na itaendelea
kuwaeleza wananchi jinsi wanavyoharibu uchumi wa nchi.
Alisema kwamba wao wenyewe kwa wenyewe wanajuana mafisadi ni wa kina nani na
ndiyo hata kwenye vikao vyao wananyoosheana vidole.
Katibu Mtendaji huyo wa CHADEMA alisisitiza kwamba chama chake ndicho chenye
historia ya kutamka hadharani mafisadi na kwamba hata kwenye orodha ya waliyo nayo wamo viongozi wa juu CCM.
Alisema pamoja na kauli ya Nnauye, lakini wataendelea kuwafichua mafisadi na
kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano katika kuwajua walipo na wanachokifanya
katika kuuhujumu uchumi wa Tanzania.
Nauye ana mbio za skafuni ataishia ukingoni;mbona hamsemi tena Maumvi EL kuhusu ujenzi wa ofisi ya UVCCM Dar as salaam?, kanyamazishwa
ReplyDeleteMnauye hajui gharama ya goma analolipiga!!muda si mrefu anaingia kwenye kikosi cha mavuvuzela
ReplyDeletekwa nn msishuhurikie mambo yenu mnakaa tu kuchangia upuuzi wa siasa ?hamna kazi za kufanya na vichwa vyenu ndio vilivyo naomba jeshi lichukue nafasi hata kwa miaka 3 kwanza
ReplyDeleteHiro ri Anonymous kweri harijui kitu rinaongea. Rinataka watu tusiongee maswara ya siasa na kuwanyoshea fidore hao mafisadi tukae tumerara kama mazuzu. Na kwa akiri sake mbofu anadhani jeshi ndio suruhu. Askali wa jeshi nao wanakura kama mchwa. Kiboko ni Katiba nzuri na mupya.
ReplyDeleteCCM NA SERIKALI YAKE WANATUMIA UJASUSI NILISHA WAAMBIA KUWA USALAMA WA TAIFA WAMEISHA PANGA NA CCM ILI KUONDOA MAANDAMANO YA WANANCHI WAKIANZA KUCHUKUA HATUA NYIE JAMANI HAMJUI?INASIKITISHA
ReplyDeleteTANZANIA YETU KUNA USALAMA WA TAIFA HAWA JAMAA NI WATAALAMU WAKUPANGA NA WANAMSHAURI RAIS NA WANAJUA SIRI ZOTE WANANCHI WANAMATATIZO TUBADILISHE HIVI NA VILE ,KWA HIYO KWA TANZANIA NDIO HIYO ILIYOPO.
ReplyDeleteNAPE KUTANGAZA HIVYO ANAJUA FIKA KABISA ILI KUZUIA MAANDAMANO YA WANANCHI KUILAANI CCM NA MAFISADI NDIO ANATUMIA MAFISADI WANATUMIA VYAMA NA VIJANA ILI KUFANYA FUJO
MNAKUMBUKA WAKATI VYAMA VINGI VILIVYOANZA WALIWAAMBIA WANANCHI MKIVIKUBALI VYAMA VYA UPINZANI VITALETA VITA KAMA RWANDA NA BURUNDI MIMI NAKUMBUKA NILIONGELEA VYAMA UPINZANI KWA BIBI NA SHANGAZI YANGU WALINIONA MIMI KAMA MUASI KWA SABABU WALIISHA DANGANYWA NA CCM.
NA NYIE WATU WA UPINZANI MUWE WEPESI WA KUFIKILIA NA KUWAAMBIA WANANCHI MAANA WANANCHI WANAITAJI KUELMISHWA NA MFANYE MAANDAMANO YA KUELEZEA MIPANGO YA CCM ILI WANANCHI WAJUE ZAIDI SIO KUWAAMBIA TU WAANDISHI WA HABARI WANAPEWA POSHO NA MAFISADI
hatutegemei usalama wa taifa ukawa usalama wa CCM na viongozi wake. wao wenyewe watakuwa wanajidhalilisha wakiwa wanafanya hivyo na wananchi hawatawaheshimu.tunategemea walinde Taifa na sio chamaaaaaaa au mtu fulani kwa maslai binafsi...Zindukeni mliko lala.hamuoni nchi za wenzenu
ReplyDeleteHakuna usalama wa taifa hapa.upo usalama wa mafisadi na viongozi dhaifu. Ungekuwepo usalama wa taifa haya mambo yafuatayo yangetokea?
ReplyDelete-Ununuzi wa ndege mbovu ya rais ambayo haijawahi kuonwa na walipa kodi.inaelekea ilipofika tu, iliingizwa gereji.
-Ununuzi wa rada
-uingizaji mitambo feki ya richimundi
wizi wa EPA
-Utapeli wa dowans
-wizi wa mapato TRA, Tanroads na kwingineko
-Wizi wa madini , kwenye migodi nasikia ndege zinaruka bila kukaguliwa
-Ugawaji wa vitalu vya kuwinda
- uharamia usiokwisha kwenye mbuga za wanyama
- kontena la meno ya tembo lilokamatwa nje ya nchi
-biashara ya madawa ya kulevya
Huu ni usalama wa taifa wa wapi ambao hauwezi kushughulikia chochote kati ya vitu hivi? Inauma sana, umaskini wa kutisha wametwishwa wtz huku baadhi ya wengine wakiishi kama vile wapo peponi. Sidhani kama kuna usalama wa taifa nchi hii, N a usalama wa taifa unapokosekana ndipo nguvu ya umma inachukua nafasi. Ndio mbadala wa usalama wa taifa. CDM ndio wanaofanya kazi ya usalama wa taifa maana wanawaanika wezi wa nchi hii hadharani.
CDM walisema kama kuna anayeona kaonewa aende mahakamani lakini mpaka leo hakuna aliyekwenda ikimaanisha CDM ni wakweli. Shime wananchi tuwaunge mkono na tuilinde nchi yetu wenyewe maana waliochukua madaraka ni kama wakoloni tu. Kumbe heri ya mkoloni mweupe kuliko mkoloni mweusi. Mungu tubariki tuilinde nchi yetu dhidi ya mafisadi. Ninaamini ipo siku kila fisadi atatoa hesabu zake mwenyewe.
Hebu angalia utajiri mkubwa walio nao vijana wadogo walioanza kazi hivi karibuni. Waliolitumikia taifa hili kwa uaminifu mkubwa leo ni maskini wakubwa wakati vitoto vidogo ambavyo havina hata miaka kumi kazini tayari ni mabilionea. Ipo siku watatueleza hizo fedha walizitoa wwapi.
Tuache mambo ya siasa na tuangalie mambo ya kusaidia jamii kuondokana na umaskini unaoendelea kukomaa nchini. Hawa akina Mnauye na wenzanke wanapata fedha nyingi kutoka chamani ambayo ni kodi ya wananchi, na wameshiba lazima apige bede atetee nafasi yake hiyo aendelee kula. Kwani mtu atazamie nini zaidi kutoka kwa Mnauye kama analipwa na analindwa na nguvu za dola? Tafadhali tuangalie mambo ya kiutendaji zaidi kama CHADEMA kinavyofanya, ili kuwajengea jamii tumaini na kuweza kushiriki katika kuboresha ustawi wa jamii.
ReplyDeleteNaungana na mtoa maoni hapo juu, ya kwamba tuangalie mambo ya jamii ili kuondokana na umasikini unaoendelea kukomaa nchini mwetu. Naona mimi kila siku imekuwa kujadili mtu au watu kadhaa: Mwana falsafa mmoja alisema hivi: Fikira dhaifu hujadiri mambo ya watu, kama vile oh fulani amenunua hiki, jana nilimwona akifanya hivi, kaoa mke wa pili nk. Fikira za kati hujadiri matukio kama vile oh jana kulikuwa na arusi ya fulani na waliolikwa walifanya hiki na kile, Simba na Yanga walipokuwa uwanjani wali wali wali utafikiri yeye mwenyewe alikuwepo pale oh bwana we mke wa Mheshimiwa ali ali ali ali.....Fikira kubwa hujadili maendeleo: Jana nilikuwa na uwezo wa kununua hiki na kile kesho ningelipenda kufika mahali pale shabaha yangu ni hii......nifanyenini nifike pale.....Hili ndilo kwangu la msingi ya kwamba hata kwa wanasiasa wetu watuongoze kufikiria juu ya maendeleo yetu sisi na kizazi kijacho si kuishia kulumbana majukwaani tu. Iwe ni CCM, CHADEMA CUF UDP wawe Viongozi wa Dini nk kaeni jadilini la maana na mtoe ushauri kwa manufaa ya Watanzania na Afrika yetu.
ReplyDeleteHUWEZI KUONDOA UMASKINI IKIWA SERA ZA NCHI NI MBAYA NDIO MAANA SERIKALI INAYOTAWALA INATAKIWA KUWEKA SERA NZURI NA KUTENGENEZA MAZINGIRA MAZURI YA WANANCHI KUJIKWAMUA.HATA KAMA UNGEFANYAJE KAMA SERA NI MBAYA NDUGU YANGU HUWEZI KUJIONDOA KWENYE WIMBI LA UMASIKINI.WATU WANASEMA WATANZANIA HAWAFANYI KAZI SIYO KWELI.WANAFANYA SANA LKN WANAISHIA KUPATA PESA YA KUNUNUA CHAKULA CHA MLO MMOJA.HAPA MAREKANI KWA SAA NALIPWA DOLA 15 KAZI HII NI YA KAWAIDA,NIKIMALIZA CHUO NITALIPWA ZAIDI $25 KWA SAA KUTOKANA NA FANI YANGU.KAZI ZIPO NYINGI KUTOKANA NA SERA NZURI ILIYOPO.
ReplyDelete