19 April 2011

Baloteli awekera wachezaji Man United

LONDON, Uingereza

USHANGILIAJI wa mshambuliaji wa Manchester City, Mario Balotelli uliwakera wachezaji wa Manchester United hasa Rio Ferdinand baada ya City kuibuka na
ushindi wa bao 1-0 katika mechi ya nusu fainali iliyochezwa katika Uwanja wa Wembley.

Rio alilalamika kuwa ushangiliaji wa nyota huyo kutoka Italia kwa kushika jezi yake na kuichezesha kama anabembeleza mtoto mbele ya mshabiki uliashiria kutowaheshimu.

Kwa ushindi huo City itacheza fainali ya FA dhidi ya Stoke City, ambayo iliifunga Aston Villa juzi mabao 5-0 katika mechi nyingine ya fainali iliyochezwa Uwanja wa Wembley.

Kwa sasa wakuu wa FA, wataamua kama watachukua hatua kuhusu hali ya ugomvi iliyoonekana Jumamosi, baada ya kuisha mechi hiyo.

Klabu zote zilikuwa na mashaka na refa, Mike Dean kwenye ripoti yake atajumuisha tukio hilo.

Balotelli ameshutumiwa na winga wa United Nani kwa ushangiliaji wake wa 'kutokuwa na heshima'. Mshambuliaji huyo wa Italia pia alisukumwa na Anderson, ambaye pia alimsukuma kocha wa City, David Platt alipojaribu kuingilia kuwaamua wachezaji hao.

Nani alisema: "Alikuwa akiwaonesha mashabiki bandeji yake. Anderson alimwondoa mbele ya mashabiki wetu.

"Rio alikasirika sana kwa sababu haikuwa sawa, ni kutoonesha heshima kufanya hivyo mbele ya mashabiki. Hatukufurahia."

Balotelli kisha alishangilia kwa kumuudhi Ferdinand kwa kutanua mdomo wake na kisha kumkonyeza nahodha huyo wa zamani wa England. Kitendo hicho kilimfanya Ferdinand akasirike na kumfuata na kisha kumwonesha kidole Platt.

Ferdinand alisema juzi: "Kama unafunga goli na unatakiwa kuwafanya mashabiki wa upinzani wakubali hilo. Lakini filimbi ya mwisho inapolia nenda kwa mashabiki wako na kufurahia, si mashabiki wa upinzani."

Kocha wa City, Roberto Mancini alisema hadhani kama kuna tatizo kubwa kutokana na kilichotokea baada ya mechi kuisha.

1 comment:

  1. wewe mwandishi vipi bwana ,Stoke City aliifunga Bolton goli 5-0 siyo Aston Vila usidanganye watu

    ReplyDelete