Na Juddy Ngonyani
CHAMA cha Askari Wastaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (MUWATA) wamemuunga mkono Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete kwa kuvionya
vyama vya siasa kuachana na tabia ya kuhamamisha maandamano na migomo kwa lengo la kuepuka uvunjifu wa amani ya nchi.
Aidha pia wananchi wametakiwa kuwa waangalifu na maandamano pamoja na migomo hiyo inayodaiwa kupangwa na baadhi ya wanasiasa kwa kuwa madhara ya migomo hiyo na maandamano ni kwa wananchi wa kawaida na si kwa viongozi hao.
Wastaafu hao wametoa kauli hiyo katika uzinduzi wa chama chao ulioambatana na kukabidhiwa vyeti kwa wanachama wa chama hicho mkoa wa Rukwa, ikiwa ni siku mbili baada ya Rais Kikwete kutoa onyo hilo wakati akilihutubia taifa katika Hotuba yake ya mwishi wa mwezi februari, huku wakidai kuwa chama hicho hakina itikadi zozote za vyama kisiasa.
Akifungua kikao hicho mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Bw. Asem Mahuji alisema kuwa ni lazima serikali iwe makini na nyendo za baadhi ya vyama vya siasa kwa lengo la kutowagawa wananchi.
Awali, akizindua chama hicho Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Kanali John Mzurikwao kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Bw. Daniel Ole Njoolay, aliunga mkono vigezo vya mtu akitaka kuajiriwa serikalini ni lazima apitie katika mafunzo ya jeshi lolote hapa nchini kwa lengo la kutela ufanisi katika kazi.
Akisoma taarifa ya wastafu hao, Bw. Chrisant Mzindakaya alisema kuwa moja ya madhumuni ya MUWATA ni kuisaidia serikali katika majukumu yake ya kila siku ikiwemo ile ya ulinzi na usalama, huku akishauri askari hao wastafu watumike katika ulinzi katika taasisi mbalimbali za serikali pamoja na bandari zilizopo hapa nchini ikiwemo ile ya Kasanga mkoani Rukwa.
Hawa wamechoka wakafie mbali vijana tunataka mabadiliko.mbona hawajawahi kukemea hali ya ofisadi nchini pamoja na uvunjifu wa haki za binadamu ikiwemo polisi kuua raia bila hatia? hawa na chama chao wapo kwa maslahi ya nani kama maovu ya serikali hawayaoni PEOPLES POWEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEER chadema tupo pamoja endeleeni kuandamana mpaka kieleweke kwani kelele za mafisadi hazizuii mabadiliko!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteNjaa mbaya sana.
ReplyDeleteHawa wastaafu wanataka warudishwe kazini ili wadhibiti maandamano? Badala ya wastaafu kuzungumzia mambo ya maana ndo mnazungumza ujinga kama huu- shameful!!
kuna uwezekano mkubwa sana kuwa aliyetangulia kutoa maoni kuandika hajazishughulisha akili zake kufikiria vizuri, ameacha watu wengine wafikirie kwa niaba yake pengine hana anachomiliki kwihiyo anahisi ghasia zikitokea ndio ataponea hapo ndugu fanya kazi kwa bidii ndio mafanikio yatakuja vinginevyo utashika bunduki na matokeo yake utachomwa moto usisumbue watu kwa uvivu na umasikini wako. muheshimiwa rais watanzania %61 tuko nyuma yako waache waandamane hadi sori za viatu zimalizike na watakapo kuja kukuomba viatu vingine uwapatie wakaandamane tena hakika wewe ni mpole na mchamungu ingekuwa mwengine wangeishapata wanacho kitaka. hawo sio bure
ReplyDeleteUmaskini, ujinga na maradhi ni ndugu wanaopendana sana,kibaya zaidi ni pale wajanja wanapoamua kwatumia ndugu hao kujinufaisha badala ya kuwakabili. Inakuwaje wastaafu ambao wananyanyasika na mfumo mbaya wawe wakwanza kuukumbatia na kumpongeza/kumuunga mkono anayeendeleza mfumo huo? Ona sasa wanashauriwa kufanya kazi za ulinzi wakati walitakiwa wapumzike nakutoa ushauri mzuri kwa vijana! Nawashauri wenye pesa zao wasiwape ajira vikongwe hawa wasio na busara.
ReplyDeleteUnasemaje, "huku akishauri askari hao wastafu watumike katika ulinzi katika taasisi mbalimbali za serikali pamoja na bandari zilizopo hapa nchini ikiwemo ile ya Kasanga mkoani Rukwa".
ReplyDeleteKwa vile hakuna vijana wa kufanya hizo kazi au? Jibu ni rahisi. Mnataka kuwafanya roboti wazee wa watu.
Badala ya kuwapa haki zao wapumzike ninyi mnataka kuwaongezea mzigo tena. Ndio maana ninyi hamstaafu mnapenda madaraka. Mnaona bora kuendelea kutawala kuliko kuwaachia wengine. Mnataka mpaka kifo kiwaondoe kazini? Sasa vijana watapataje ujuzi kama ndio hivi?
mwenyekiti wao tu mwizi sa wanamsikiliza ili iweje? kafieni mbali
ReplyDeletewewe uliyemwambia mwenzio maskini wewe ndo una umaskini wa milango mitano ya fahamu ziangalie kazi zake uatajielewa shwaini wewe
ReplyDeleteukweli wote wa usultani wa Tanzania utajulikana karibuni. USULUTANI WA KIUKOO NA USULUTANI WA CHAMA KIMOJA KINACHOLINDWA NA MAJESHI HAKUNA TOFAUTI YEYOTE. WATANZANIA WALILAZWA USINGIZI MUDA MREFU WAKATI WENYE ELIMU WACHACHE WALIPOUNGANA KUWAKANDAMIZA. KIKUNDI KILICHOZOEA KUTAWALA HAKIKUBALI KUACHIA HIYO PRIVILEJI KIRAHISI. MMEONEA YALE YA GADAFI NA WENGINEO.
ReplyDeletepole sana ndugu yangu unadhni chadema ikiingia ikulu utapata ajira kama unavyodhani, we wapiganie tu mbowe na marafiki zake waende wale wewe huna chako hapo
ReplyDeletewewe unaowatetea hao wahuni wa ccm ni msenge,watu wanataka mabadiliko,sio mtu analala anafikiria kesho atakula,,,WATU HAWAHITAJI UTAJIRI ,WANATAKA CHAKULA,AFYA, ELIMU BORA, AJIRA, hayo ndio muhimu ...Ukisikia nchi imeendelea usifikiri RAIA wake wote ni MATAJIRI,ila wanapata huduma zote muhimu kwa binaadam....
ReplyDeleteWafuasi wa shetani utawaona tu wakati wenzao wakitoa hoja wao wanatoa matusi, utoto na bangi mbaya, mnafikiri Massihi Dajali akisema atakupa utajiri basi utaupata utajiri kweli. Poleni mwee na nyie mlotukanwa wasameheni maana hawa si bure kiko kinachowadhuru wamekuwa kama wamerukwa na akili kila mtu wanamtukana ibilisi huyo kawasimamia mpaka lifike la kuwafika ndio watapumua! Haiyumkiniki mtui katoa maoni wewe unakasirika mpaka kumtukana sasa uzima huo au laana ya ibilisi? Maana panapo ibilisi siku zote pana shari!
ReplyDeletePeopleeeee power, power peoplee
ReplyDeleteWatoji maoni mnaotukana mnaliletea Taifa aibu, Kila mtu ana haki ya kuandika kile anachoamini kuwa ni sahihi sasa matusi yanatoka wapi? Hoja ijibiwe kwa Hoja. CHA KUKUMBUKWA SIKU ZOTE NI KWAMBA, MAKOSA 99 HAYAWEZI KULIFANYA JIBU SAHIHI 1 KUWA KOSA ETI KISA WENGI WAPE!!!!!USEMI WA WENGI WAPE KUNA MUDA HUWA HAUFANYI KAZI.
ReplyDeleteHawa tena wanatoka wapi? Walikuwa wapi? Jamani pumzikeni kwa amani au mnataka kuteuliwa kuwa Wakuu wa Wilaya kama ilivyozoeleka?
ReplyDeleteMimi kama mwanajeshi mstaafu, nasikitishwa sana na hatua ya kuanzishwa chama hiki ambacho malengo yake kusema ukweli nayatia mashaka. Niliona ile timu ambayo ndiyo wanakiongoza chama hiki. Nilishangaa sana kuona, viongozi/uongozi haukuzingatia vyeo. Ni ajabu kweli mwenyekiti anakuwa NCO na katibu ni kanali. Sijapata kuona kitu kama hicho. Jeshi lina traditions and norms hata baada ya kustaafu. Hivi wanajua kuwa bado ni wanajeshi na kama kutatokea dharura ambayo watakuwa mobilized huyo kanali atampa amri mwenyekiti wake? Halafu nashangaa bado wanaomba kuendelea kupewa kazi, of all what they want ni kuwa walinzi tena. Kwa nini basi wasianzishe kabisa kampuni ya ulinzi, kwani wakipewa hilo jukumu la kulinda watakuwa wanajitolea? Huu ubabaishaji hautakiwa kuendekezwa.
ReplyDeleteLa mwisho nyinyi chama cha wanajeshi, acheni kujiaibisha, acheni kujihusisha na siasa hasa ya kuelemea upande mmoja kwa sababu upande mwingine utawahoji. Na nyinyi serikali, vyama hivi mviangalie pia. Mnakumbuka ya Zimbabwe na wapigania uhuru. Muwaambie waende wakapumzike kwa amani au basi washiriki kilimo kwanza kama mimi ninavyofanya. Nina shamba langu la pilipili, shamba la mbuzi, umeme wa solar, Napata mtandao, ni mwenyekiti wa kijiji nakwenda mjini mara mbili kwa mwezi na hujitolea kufundisha shule ya kata. Naheshimika kweli.
Mungu ibariki Tanzania
Pensheni imeisha mmekuwa apeche alolo sasa; maandamano ni haki ya kikatiba ya mwananchi ... pumzikeni msije mkazeeka vibaya ...
ReplyDeleteMUWATA kama pensheni haziwatoshi na mnataka kuwa kama 'janjawidi' basi Kanali Gaddafi anataka askari wa kukodi na pia kazi za ukorokoroni kwa mshahara mzuri pia zipo Afhganistan na Iraq, wenzenu toka Uganda wamejaa hapa Iraq.
ReplyDeleteMkitumiwa na CCM hamtapata mshahara wa kutosha zaidi ya kiongozi wa MUWATA kupelekwa The Hague