Na Elizabeth Mayemba
UONGOZI wa Yanga umepanga kufanya jitihada za kuhakikisha zinamshawishi mfadhili wake ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Udhamini, Yusuf Manji ili
kumrejesha baada ya kuamua kujiuzulu nyadhifa hizo.
Pia uongozi huo umepanga kuelewana naye upya hata kama ni kibiashara.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa klabu hiyo Lloyd Nchunga alisema Februari 15, mwaka huu Manji aliwasilisha barua kwenye Kamati ya Utendaji ya kujiuzulu katika nyadhifa zake, baada ya baadhi ya wanachama kumkashifu.
Nchunga alisema kutokana na hatua hiyo ya Manji kujiuzulu, Kamati ya Utendaji iliamua katika kipindi hiki wakati mfadhili huyo akiwa hayupo watalazimika kubuni na kukaribisha vianzio ikiwa ni pamoja na kufungua akaunti maalumu kwa ajili mashabiki wa Yanga kuchangia.
Alisema pia kamati hiyo ilitoa tamko kulaani vitendo vya kashfa ambavyo viongozi wamekuwa wakituhumiwa akiwemo Manji na ikakubaliwa kupeleka majina ya wanachama wakorofi katika Mkutano Mkuu kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
"Kimsingi maazimio ya mkutano wa matawi na Kamati ya Utendaji ni kwamba bwana Manji bado tunamhitaji
Alisema baadhi ya wanachama wa klabu hiyo mwezi uliopita waliitisha mkutano na kuthubutu kumfedhehesha Manji audilifu wake ndani ya Yanga, kitendo ambacho kilimvunja moyo mdhamini huyo na kuamua kuchukua uamuzi wa kujiuzulu.
"Kabla ya kunikabidhi barua nilitumia uwezo wangu wote kumsihi asitishe azima yake lakini alikataa, pia makundi mbalimbali ikiwa pamoja na wazee walimsihi nadhani kuna mambo watakuwa wamekubaliana kwa manufaa ya Yanga, yaani kurejea kwake katika nyadhifa zake," alisema Nchunga.
Alisema siku hiyo hiyo, aliyokabidhiwa barua na Manji aliwaita viongozi wa Kamati ya Utendaji na moja kwa moja katika ajenda yao ilikuwa ni kuwapa taarifa za tukio la kujiuzulu kwa mdhamini huyo.
Nchunga alisema kamati kwa mara nyingine tena ikaamua kumuandikia barua Manji, ili asitishe uamuzi wake pia wapate fursa ya kuonana naye kuongelea suala hilo, hata hivyo Manji aliijibu barua hiyo na kusisitiza msimamo wake kukaa kando.
Mwenyekiti huyo alisema hatua hiyo ilimfanya aitishe mkutano wa matawi ambao ulifanyika Februari 26 mwaka huu na ajenda kubwa ilikuwa ni suala la Manji kujiuzulu, kitu kilichowashtua viongozi wa matawi.
Aliongeza kwamba Yanga kila mwaka inahitaji takribani sh. bilioni 1.2 kwa ajili ya kuendeshea mambo mbalimbali ya klabu.
hao ndio viongozi wetu wasomi.je kama yanga ingekuwa inaongozwa na watu wasio na elimu sijui ingekuwa tegemezi kiasi gani, inashangaza kuona kwa kipindi chote alichokuwa Manji anahifadhiri yanga lakini mpaka sasa inashindwa kusimama yenyewe wakati inaongozwa na viongozi wasomi, yaani pamoja na mapato ya milangoni,michango ya wanachama,pesa za udhamini wa kilimanjaro na vodacom lakini bado yanga inamtegemea mtu mmoja? aibu gani hii kwa wasomi wetu? je yanga haiwezi kuwepo bila Manji? na wewe Manji kama kweli unahitaji maendeleo ya soka katika nchi yetu kwa nini usianzishe timu yako kama alivyofanya Azam ili uondokane na matusi kwa hawa wasio na shukrani? hivi unafikiri kweli unaweza kuibadilisha yanga? ebu angalia pesa ulizotumia mpaka sasa na mabadiliko yaliyopatikana, timu imeshindwa kufika hata 16 bora katika mashindano mbalimbali ya Afrika, lakuvunda halina ubani, achana na hao Yanga anzisha timu yako maana kama unauwezo wa kusajiri wachezaji,kulipa makocha kukarabati na kujenga uwanja wa yanga kwa nini usifanye hayo mambo kwa timu yako mwenyewe ambayo kwanza haitakupa kero maana kila kitu utakuwa unamiliki mwenyewe hakuna kelele za wanachama wala nini, wapenzi na washabiki utatupata tuu kama vile azam inavyoleta mabadiliko ya soka. wapenzi wa soko tumechoka kisikiliza polojo za simba na yanga kila siku.
ReplyDeleteKweli kabisa ndugu yangu! wakati mwingine hawa wafadhili wanatakiwa kuanzisha timu zao kama Azam alivyofanya. Tuachane na usawhili wa simba na yanga ambazo mpaka sasa hazina miradi ya maendeleo ya kueleweka. Angalia Azam ndani ya kipindi cha miaka 3 imeweza kumiliki 'hostel', kiwanja tena cha kisasakitakachokaguliwa na FIFA hivi karibuni. nafikiri simba na yanga zikifa tukawa na timu nyingi zenye muundo wa Azam ndo nchi yetu inaweza kwenda world cup 2018 tu.
ReplyDeletesiasa hata kwenye club za mpira viongozi kazi kulalama tu .Chemsheni mbongo zenu muanzishe projects za kuwaingizia pesa.mtawategemea wakina manji hadi lini na huku nyie ni klabu kongwe na kubwa east africa???Wakti mnaomba kura huwa mnajitapa mtabuni mipango kibao ya kuifanya club iwe kama Zamalek lakini mwisho wa siku mnakuwa waliaji
ReplyDeleteNi kweli kabisa ndugu zangu mmetowa mawazo ya busara hapo juu kuhusu simba na yanga.Tatizo kubwa kwa wanachama wa hizi timu pamoja na watu wanaojiita wazee wa wa timu wamejisahau na kuona kama hizo timu ni mali yao na mtu anapojitokeza kusaidia hizi kuwa kama kampuni na kuwa na miradi yao kwa ajili ya kuendesha timu huwa anaonekana kama ni adui.Imefika wakati sasa hizi timu zinatakiwa kujiendesha zenyewe na sio kila siku kutegemea fedha kutoka kwa wafadhili,Hata wafadhili itafika siku nao watachoka kwani kili wazo wanalotoa kwa ajili ya kuendeleza timu huwa baya watu wachache wasio na mtazamo mzuri katika timu za simba na yanga.Mfano mzuri ni kwa timu kama Al-ahly,Arab contractor,Zamalek,Espirance,Enyimba,Asec mimosa hizi timu zote zinamafanikio makubwa kisoka katika Afrika kwa kuwa na miradi yao wenyewe inayosaidia kuendesha timu.Ni aibu kwa timu simba na yanga ambazo kipindi kingine zinakosa hata fedha za kupeleka timu mikoani kwa ajili ya mechi za ligi kuu.
ReplyDeleteMfano wangu wa mwisho ambao niliona ni wazo zuri kutoka kwa mmoja kati ya kiongozi wa hizo timu alitaka kupata watu kama kumi kwa ajili ya kupata mkopo kutoka kwa wafanyabiashara na kuazisha mradi wa kuendesha
hiyi timu na katika miaka mitatu wangerusisha mikopo waliochukuwa ambayo ilikuwa ni shillingi milioni hamsini kutoka kwa kila mfanyabiashara aliyewakopesha na kuwezesha timu kuanza kujiendesha yenyewe.
Hili lilikuwa ni wazo zuri sana kutoka kwa huyo kiongozi lakini cha kushangaza huyo kiongozi alioneka ni mbaya sana kwa wanachama wa yanga.Je simba na yanga mtaendelea kuwa ombaomba mpaka lini? na mkumbuke ya kwamba mpira wa sasa ni kazi kwa wachezaji na ndio maisha yao yanapotokea.na unapomuhitaji mchezaji mzuri lazima uwe na fedha za kumnunua na sio kugeukia kwa mfadhili kwa ajili ya hizo fedha, wakati umefika sasa wa kujiendesha wenyewe na kila timu inatakiwa kuwa na kiwanja chake na jengo la timu ambalo ni safi na vyumba ambavyo ni vizuri vinakilakitu kwa ajili ya mchezaji