Na Mohamed Hamad, Simanjiro
MWALIMU Matias Eliza (47) wa Shule ya Msingi Orkesmet iliyopo wilayani Simanjiro ametoroka mikononi mwa polisi akiwa hospitalini baada ya kutuhumiwa kumbaka
mwanafunzi wa darasa la tatu.
Tukio hilo lilitokea Feb 27, mwaka huu saa 12 za asubuhi wakati mwanafunzi ambaye jina limehifadhiwa akielekea shuleni kupitia karibu na nyumba ya mwalimu.
Kama ilivyo kawaida kwa mwanafunzi kuwa na nidhamu kwa mwalimu wao bila kujua nini anachoitiwa na mwalimu huyo, siku hiyo alimtaka aingie ndani baada ya kumtuma akachukue kitu.
Baada ya mwanafunzi huyo kuingia ndani mwalimu huyo alimfuata huko ndani na kumkamata hatimaye kuanza kumbaka, baada ya watu kusikia kelele walifika, alisema Kamanda Parmena Sumari wa Jeshi la Polisi Manyara.
Alisema miongoni mwa waliofika hapo kwa kelele hizo ni pamoja na mlezi wa mwanafunzi huyo ambaye pia ni mwalimu wa shule hiyo ambaye alikuwa akielekea shuleni.
"Mlezi huyo alipofika, alisema alisiki sauti na kujiuliza, 'mbona ni kama sauti ya mwanangu ndani'?...hapo alizidi kusogea na ndipo akaomba msaada kwa wasamaria wema kumtaka mwalimu huyo afungue mlango wa nyumba yake hiyo.
Mwalimu huyo alikataa kufungua ndipo wakaamua kuvunja mlango na kumkuta akiwa anavaa nguo, wakati mwanafunzi huyo akilia.
Baadhi ya mashuhuda hao walimpa kipigo kizito mwalimu huyo huku wengine wakisogeza mafuta ili achomwe na kuokolewa na askari waliokuwa wanakwenda kazini.
Baada ya kuokolewa alipelekwa hospitalini na katika mazingira ya kutatanisha alitoweka akiwa chini ya ulinzi na Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta.
Kamanda Sumary alisema hatua zaidi zitachukuliwa kwa askari waliohusika kumtorosha mhalifu huyo.
Hapa ukisema kuna uzembe kwenye jeshi la polisi utaambiwa unataka kuharibu amani na mshikamano wa watanzania ...
ReplyDelete