*Wadai viongozi wanazuia baada ya wao kuponywa
*KKKT yapeleka mafundi kuweka sawa miundombinu
*Ndesamburo apeleka helikopta kusaidia walio mahututi
Na Said Njuki, Arusha
MAELFU ya watu wanaomiminika kwenda Kijiji cha Samunge Loliondo kusaka tiba ya
magonjwa sugu wamegoma kuondoka bila kunywa dawa wakipinga agizo la serikali na kuwataka wasitishe shughuli hiyo ili kupunguza msongamano na suala la usalama.
Habari za uhakika zilizopatikana kutoka Kijiji cha Samunge kwa Mchungaji Mwasapile zimeeleza kuwa wagonjwa waliokuwa tayari wamefika huko hawako tayari kuondoka hadi watakapotibiwa, licha ya serikali kuagiza waondoke hadi muda muafaka utakapofika kwa mchungaji huyo kuendelea na tiba.
“Hili agizo la Serikali limekuja wakati si wake, wao walichotakiwa kufanya ni kuhakikisha wagonjwa hawaondoki majumbani mwao, lakini huwezi kumwagiza mgonjwa aliyoko katika foleni ya tiba kituoni aondoke kabla hajapata tiba bila kujali gharama alizotumia, muda wake na mbaya zaidi alichokifuata hajapata,” alilalamika mtu mmoja aliyejukana kwa jina moja la Ezekiel.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti watu mbalimbali waliohojiwa na Majira walisema uamuzi huo si sahihi kwa kuwa unakwenda kinyume na shauku ya wengi ya kupata tiba hiyo inayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile.
Miongoni mwa waliopinga uamuzi huo ni Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati likisema uamuzi huo utahatarisha uhusiano mzuri uliopo baina ya serikali na kanisa hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Arusha, Askofu wa Kanisa hilo, Thomas Laiser alisema si sawa kusitisha huduma ya Mchungaji Measapile yenye 'elementi' ya kiroho bila kuwahusisha wadau ambao ni kanisa hilo.
Juzi Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Haji Mpanda alisitisha tiba hiyo kwa maelezo kuwa wanasubiri ripoti ya Kamati ya uchunguzi wa tiba hiyo iliyoundwa na wizara hiyo mapema wiki hii hadi kamati hiyo itakapotoa taarifa yake.
Pia Dkt. Mponda aliitaja sababu zingine kuwa ni kuweza kuichunguza dawa hiyo kisayansi na pia hali mbaya ya kimazingira yanayohatarisha afya za watu na wagonjwa waliofurika katika eneo hilo wakisubiri tiba hiyo mbadala, ya saratani, Ukimwi, kisukari na magonjwa mengineyo.
Askofu Laiser alisema lililotokea kwa mchungaji huyo si jambo la kisayansi bali ni jambo la kiimani na kimaombi na kuhoji iwapo jambo hilo Mwenyezi Mungu amelikubali kiimani na kimaombi ni vipi utalijaribu kisayansi.
“Mti huo kwa kabila la Kisonjo unaitwa ‘Olmorjoy’ na wanaamini kuwa una sumu kali, lakini sisi Wamasai tunauita ‘alamkriyaki’ na tulikuwa tukila matunda yak, lakini hata kama ndio huo sasa Mungu ameubariki na watu wanapona wakiwemo mawaziri na viongozi mbalimbali wametoa ushuhuda huo, lakini pia hao wachunguzi wanajua kuwa haiwezekani dawa ya kiroho kupitia maabara,” alisisitiza Askofu Laiser.
Alishauri huduma hiyo iendelee kadri Mwenyezi Mungu atakavyoamua kwani kinachowaponyesha watu ni imani yao kupitia kikombe alichokiita cha ‘uokovu’ cha Mchungaji Mwasapile.
“Utakapomwambia mtu yeyote aliyeteseka kwa muda mrefu kuwa tiba imesitishwa ni wazi utasababisha matatizo yasiyokuwa ya lazima, hivyo jambo muhimu ni kuhakikisha serikali inashirikiana na wadau katika kufanikisha tiba hiyo kwa utaratibu mzuri usiokuwa na madhara ikiwa ni pamoja na kuweka miundombinu imara itakayowahakikishia usalama…lakini kuondoa mgonjwa aliyekuwa amefika huko haikubaliki,” alisema kwa msisitizo.
Askofu Laizer alisema tayari wataalamu wa ujenzi wa kanisa hilo wameondoka kuelekea kijijini huko kuandaa michoro na kutathimini gharama za ujenzi wa mahema na miundombinu mingine kwa kushirikiana na serikali kwa lengo la kuondoa ugumu wa tiba hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana viongozi wa taasisi na mashirika mbalimbali ya kiraia wamedai hizo ni hila za serikali za kuzuia wananchi wake wasipate tiba hiyo, kwani kitendo cha kusitisha tiba hiyo kimefanyika baada ya idadi kubwa ya viongozi serikalini kutibiwa.
Mkurugenzi wa Shirika la Haki za Binadamu lenye Makao Makuu yake mjini Loliondo la LARETOK, Bw. Ole Ndangoya amesema tangu tiba hiyo ilipoanza miezi kadhaa iliyopita tayari zaidi ya nusu ya viongozi wa taasisi mbalimbali na serikali wameshapatiwa dawa hiyo na anaamini ndiyo sababu ya kusitisha ghafla bila kujali idadi kubwa ya wagonjwa walioko katika foleni wakisubiri.
Bw. Ndangoya aliyeeleza kuwa neno LARETOK ni neno la kabila la Kimasai lenye maana ya Wasaidizi wa Kisheria na Haki za Binadamu, alisema anakubaliana na uwekaji wa miundombinu murua katika eneo hilo ili kudhibiti uharibifu wa mazingira unaoweza kusababisha afya za watu kuathiriwa, lakini suala la kuweka urasimu wa tiba hiyo halikubaliki na shirika hilo halitanyamazia jambo hilo.
“Viongozi wa dini, wa serikali wameshafika huko na kunywa dawa hiyo, labda ndicho walichokuwa wakisubiri ili wasitishe tiba hiyo na kuwataka wagonjwa waliotumia fedha, muda na nguvu nyingi kuondoka bila kupata tiba hiyo, jambo hili halikubaliki,” alionya Bw. Ndangoya bila kueleza shirika lake linakusudia kufanya nini baada ya hapo.
“Kusitisha kwa ajili ya kuweka mazingira yawe mazuri ni utaratibu mzuri, sawa, nakubaliana nao, lakini wengi wamepata dawa na kukiri kuwa wamepona, hivi hao unaowazuiliwa hawana haki hiyo?” alihoji Mkurugenzi huyo.
Aliongeza Katiba inaainisha kuwa serikali haina dini, bali watu wake ndio wanayo dini, ndio wanaoponywa kwa imani za dini, na iwapo itang’ang’ania kuwa imsajili mchungaji huyo basi serikaili inayo dini ni vema itaje hiyo dini yake.
Akithibitishwa kusitishwa kwa tiba hiyo, Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw. Elias Wawa Lali alisema usitishaji huo ni wa muda ili kutoa nafasi kwa Mchungaji Mwasapile kusajili dawa hiyo Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na tayari fomu ameshazipata huku taratibu mzuri za kimazingira zikifanywa ili kuepuka magonjwa ya milipuko yanayoweza kuhatarisha afya za watu.
Alisema hali inazidi kuwa mbaya katika eneo hilo finyu lililoshsheni idadi kubwa ya magari na watu kiasi kwamba hakuna na hakuna njia nyingine mbadala zaidi ya kusitisha tiba hiyo kwa muda na wagonjwa waliyoko huko kuondoka.
“Serikali haina nia mbaya na tiba hiyo, kinachotakiwa ni usajili ya tiba hiyo na tayari mamlaka husika imeshampatia fomu Mchungaji huyo ili azijaze, lakini kubwa zaidi serikali inashirikiana na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kuhakikisha hali ya mazingira inaboreshwa kwa kiwango cha juu.
Hofu yangu ni jinsi ya kudhibiti uingiaji wa wagonjwa kutoka sehemu mbalimbali lakini tayari suala hilo limewekewa utaratibu wake,” alisema Mkuu huyo kwa njia ya simu jana.
Naye Richard Konga anaripoti kuwa Mwinjilisti wa KKKT wa Kanisa la Samunge lililokuwa likiongozwa na Mchungaji Masapila, Bw. Daniel Mbario ameiomba serikali iwe bega kwa bega na babu huyo ili kuboresha mazingira na kurahisisha utoaji wa huduma na kurahisisha upatikanaji wa dawa.
Kwa upande wao watumiaji wa dawa hiyo, akiwemo Paschal Mbise ambaye mdogo wake Philipo Mbise alikufa katika foleni kabla ya kufikia tiba ya pumu baada ya kutoka Hospitali ya Kibong’oto ameiomba serikali kuingilia kati kuboresha huduma katika eneo hilo.
Hamna lolote Serikali. Wivu tu umewajaa. Mmeona ninyi mna uwezo wa kwenda kutibiwa India na China mnasitisha huduma ya bure kabisa iliyotumwa na Mungu, halafu eti mnataka ufanyike uchunguzi, uchunguzi gani wakati mmeambiwa dawa imetoka mbinguni, Mungu hachunguziki kamwe. Tunawajua Serikali hamjali afya za wananchi wenu. Mbona "Babu" aliwaumba mahema, huduma za vyoo na maji hamjamsikiliza. Au mmeona hospitali zenu za Muhimbili zimepungua mapato?
ReplyDeleteSerikali ya CCM haijatokana na Mungu. Ndio maana kazi yao ni kubomoa nyumba za watu. Kubomoa biashara za watu. kuvunja mabango ya biashara. Kupiga na kuuwa watu wanaoandamana. Haiwezi kuleta umeme. Kazi yake ni ubishi bungeni na kudanganya wananchi. Sasa Mungu ametuletea msaada ili tupone.Serikali inampiga Mungu marufuku asiponye watu wake. CCM haifai kabisa
ReplyDeleteMUHIMU KUHAKIKISHA WALIOKUWA TAYARI WAKO KULE WANAPATIWA HIYO DAWA NA KUONDOKA HUKU WATU WENGINE WAKISUBIRIA KWA MPANGO MAALUMU LAKINI KUWAAMRISHA WASITISHE NA WARUDI NI UONEVU NA KUTAKA KUZIDI KUWAPA MATESO NA HASARA,FIKIRIA MTU KATUMIA ZAIDI YA LAKI 4 AU 5 NAULI TU,MAANA MGONJWA HAWEZI KWENDA PEKEYAKE LAZIMA KUNA MSINDIKIZAJI,KUNA GHARAMA ZA CHAKULA NK, LEO IWEJE ARUDI? WASIKURUPUKE. NA SASA HILI JAMBO LITAGEUKA LIWE LA KIDINI AU KISIASA MAANA NAONA WASEMAJI NI WENGI MNO!!TUWAPE WATU UHURU WA KUAMINI IMANI ZAO,SERIKALI IHAKIKISHE USALAMA WA RAIA KUWAWEKEA MAZINGIRA MAZURI, VYOO,MIUNDOMBINU NK; SIO KUZUIA
ReplyDeleteWaziri angeshauri watu wasio amini upoyaji wa Mungu wetu wa Wakristo wawe na amani tu. siyo lazima waje. waruhusiwe kwenda kwenye dini zao au kwa waganga wao wanaowaamini. Mchungaji hatafuti waumini. Ametumwa na Mungu kutusaidia sisi tunaomwamini Yesu.
ReplyDeleteEeh maajabu haya serikali inasitisha huduma ilhali pana watu lukuki pale!huo ndio mwanzo wa kutaka kumwaga damu za watu wasio na hatia.vipi hii serikali isitishe huduma wakati huu wakati huyo mzee ameanza kutoa huduma muda mrefu na watu wengi wameshapata hio huduma vipi isiwapime wale waliokunywa!serikali ingeliweka kipau mbele katika kuimarisha huduma hio sehemu na sio kuzuia hio huduma.pia tunamuomba huyo mzee atibu watu wote kwa usawa bila kuweka itikadi za kidini na ukabila kwa kuwa sisi wote ni wa MUNGU.
ReplyDeleteMUNGU NI MKUBWA.leo hii tunashuhudia maajabu ya MUNGU kwa kupatikana dawa katika nchi yetu.tunamshukuru MUNGU kwa kutupa hii dawa.pia MUNGU ametupa vitu vingi tu vizuri lakini vingi vipo mikononi mwa hii serikali ndio maana leo hatuoni maendeleo ya hivyo vitu sana sana ufisadi tu.(nakusudia hapa tuna madini,bahari,ardhi,mito,gass na vingine vingi tu lakini havina maendeleo.)lakini MUNGU akatujaalia kupatikana dawa lakini ipite kwa mtu wa chini ili asaidie jamii yake.Alhamdulillah sasa watu wanapata hio huduma.hapo sasa angalia kama ingelipita hio dawa katika mikono ya serikali nadhani wenye nguvu ya fedha ndio wangaliipata, sijui ingalikuaje kwa sisi watu wa chini.MUNGU hatupi waja wake na tunamuomba mungu azidi kutupa neema zake.wewe pia ni mtu unayeonyesha unamuamini MUNGU ndio sababu ukachaji sh 500 kwa kila mgonjwa na pia hio pesa nasikia unazitolea sadaka bimaana sh 300 ni kwa ajili ya msikiti,kanisa na watoto yatima na 200 ni ya kuendesha huduma zako.MUNGU akupe umri mrefu na afya iliyo sawa.Amin
ReplyDeleteSadaka Mtoleeni Mungu aliyewaponya. iweje akuponye Yesu sadaka ukamtolee Mungu sanamu kwa mfano?
ReplyDeleteSerekali ya CCM ni ya kiazandiki. wao hawataki jumuiya ya kimataifa ijue kuna dawa ya ukimwi wasije wakakosa misaada!! washenzi wakubwa haya misaada yenyewe inafikia katika mifuko ya mafisadfi na sio waathirika..mungu awalaani ccm na serekali yao..msimamo ni mmoja tu... dawa ya kiroho haitapimwa kisayansi
ReplyDeleteMh.Waziri wa afya ninaomba uwasiliane na chama cha msalaba mwekundu ili waende Loliondo wakaweke mahema kwa ajili ya wagonjwa wanaotoka mikoani.Ninakuomba uwache kufuata maneno ya mitaani.Ninaomba ufanye ziara ya kustukiza dhidi Mch.Mwasapile ili upate ukweli wa mambo kuliko kusikia maneno ya watendaji ambao ni waongo sana na wachonganishi kati yako na wananchi ambao wanamagonjwa sugu.
ReplyDeleteHili ni suala la KIIMANI na siyo kisayansi, na ninaamini kila mtu anajua nini maana ya kuamini katika kitu, wale walioamini ndio wanaopona, na kama wanapona serikali kuwazuia wale walioamini na kuchukua hatua ya kwenda kupata matibabu siyo sahihi. Matatizo ya miundo mbinu yapatiwe ufumbuzi, mfano serikali imeanza kujipatia pesa kwa kutoza kodi magarin yanayoingia kijijini, hiyo kodi itume kuboresha miundombinu. ushauri wangu ni kwamba wale waliokwisha fika huko wote wapatiwe dawa, kama inawezekana babu apatiwe msaada wa vyombo masufuria na kuni za kutosha na usafiri wa kwendea dawa polini, ili angalau wale wote walioko kwenye foleni, kufikia Ijumaa week ijayo wawe wameishaondoka, wakati huo wananchi waelezwe kwamba matibabu yatalejea tena baada ya muda fulani ili mazingira yaboleswe, vilevile babu azidi kumwomba Mungu amfunulie na kumpatia maelekezo ya namna ya kwenenda maana mambo haya ni ya Kiimani zaidi sasa kukurupuka na kufanya kama binadamu anavyotaka vile vile kunaweza kusababisha muujiza huu kutuponyoka. Ambao hawamwamini Mungu katika hili wakae pembeni ili wapishe Mungu afanye kazi yake. Mimi ninaamini katika uponyaji wa Kimungu na ningewashauri serikali wasaidie na siyo kuzuia, na kwa kuiondolea serikali wasiwasi, siyo wote watakaokunywa hiyo dawa watapona, wengine watarudi tu huko hospitali kama tulivyokwisha kusikia, hili ni swala la kiroho zaidi, mwacheni Mungu kwa kutumia mtumishi wake awaguse watu wake aliowakusudia.
ReplyDeleteAsante Mungu kwa kutuletea uponyaji wako. Naiomba Serikali ishirikiane na Mchungaji huyu ili aweze kuwaponya watanzania wanaoteseka kwa magonjwa haya kwa muda mrefu.
ReplyDeletekakobe mbona hueleweki siasa au dini. yako ndo ya ukwel ya wenzio ya uongo acha siasa kwene iman
ReplyDeleteJamani lakini mwategemea nini kutoka Serikali na chama chenye wivu, chuki, unafiki na matabaka. Vigogo wengi wa Serikali na chama tawala walishakwenda kule na kupewa hiyo dawa. Magari mengi ya serikali na chama yamekuwa yakiingia na kutoka tangu watu waanze kufurika kwa Babu. Someni gazeti la Mwananchi la Jumapili tarehe 6 March 2011). Sasa wao na familia na vimada wao wamekwisha kunywa dawa hiyo na hawataki wengine waipate kwani hiyo itaharibu ule usemi wao wa "sisi tuko imara, mafukara wafilie mbali, wasijefanana na sisi" Hii serikali ya ccm imezoea utawala wa kuamrisha bila kuwapo na mjadala: hii ni kuwadharau wananchi ambao ndio waliowaweka madarakani.
ReplyDeleteWakome tabia hiyo. Lakini nitumie nafasi hii kuupongeza uongozi wa mkoa wa Arusha, na hasa Kamanda wa jeshi la polisi kwa kukataa kusitisha dawa hiyo na badala yake akaongeza askari wa kulinda usalama ili wananchi wapate dawa hiyo katika hali tulivu. Huyu ni kiongozi aliyeona mbele. Pia mkuu wa mkoa amekuwa na busara ya kuishauri serikali kutositiza utoaji wa dawa hiyo. Siyo kila kiongozi wa serikali ni kichwamaji, mwenye kusema ndio bwana mkubwa. Wako wengine pia wenye uwezo wa kufikiria na kuchambua mambo. Lakini hao ni wachache sana.
Inachekesha KWELI hivi mnafikiri hatujui mmekunywa nyie kwanza halafu sasa ndio mnabinua vidomo vyenu,o sijui mazingira,oh watu wengi, na sema hivi hakuna anaye penda kufa alihali anauwezo wa kupambana mwageni jeshi ikiwezekana hata vifaru hatutoki mpaka na sisi tunywe.pelekeni upuuz wenu huko.
ReplyDeleteCCM ndivyo walivyo.Na utashangaa watu wakigoma kuondoka utasikia wakisema sababu ni chadema.
ReplyDeleteMuulizeni Mahita hakwenda na kunywa?je alikwenda na choo chake?Waziri usijitie aibu.
WASIO AMINI DAWA HII WAENDE ZAO HUKO WASITUVURUGIE SISI TUNAOAMINI. MANAKE VURUGU ZOTE ZIMETOKANA NA WATU WASIOAMINI WHIYO DAWA IPIMWE KWANZA.
ReplyDeleteWANAOPINGA NENDENI ZENU HUKO TUACHENI SISI NA DAWA YETU TUPONE KIVYETU. KAMA HAMUAMINI TUONDOKEENI HAPA HAMJAITWA.
Namshukuru Sana Mh Ndesamburo kwa kujitolea Helcopter kusaidia wagonjwa. Kutoa ni moyo wala si utajiri. Mwenyezi Mungu aendelee kukubariki na kukujazia zaidi Mh NDesa
ReplyDeleteWapo matajiri kama EL, Rostam, Jk na wengine wengi na wana mabilioni kibao lakini ni wabinafsi. Sijui hizo hela watamaliza?? Au watakufa waziache??
Pongezi serikali pongeza waziri Lukuvi kwa kuliona hili.naimani mmetumia uamuzi wa busara katika kuamua suala hili ili watu wote wapate huduma ya huyu mzee.ni kweli kabisa uamuzi wowote ule wa kumzuia huyu mzee ungelileta fujo kubwa sana na ikawa sababu ya watu kuumizana.pia kwa muda huu kama serikali mngelipeka huduma muhimu pale ili yasije kutokea maradhi ya maambukizi.kwa kuwa hao watu waliopo huko ni theluthi tu ya wagonjwa,wengi watakuja huko kutoka mataifa mbalimbali kuja pata tiba ya huyo mzee.namtakia maisha marefu na afya iliyo sawa huyo mzee.
ReplyDeleteSASA NIKWELI SEERIKARI YA TANZANIA HAINA DOGO HATA WATU WANAOTIBIWA MNAANZA KUWAKATALIA, MNATAKA KUPELEKA UFISADI HATA KWA MPONYAJI, NINYI MMEUWA WATU KWA RISASI SASA HATA WANOPONA KWA DAWA MNAWAKATALIA? SERIKARI ACHENI FUJO, KAMA NI UFISADI FANYENI KWENYE HIMAYA ZENU NASI KWATU, TUACHENI NASI TUPONE MBONA VIONGOZI WASERIKALI WANAFANYA MAMBO YA KISHIRIKINA WANANCHI TUNAFUMBA MACHO. WAPUUZI NYIE, KAENI MBALI NA UFISADI WENU.
ReplyDeletejamani nendeni mkapate tiba sahihi iliyoletwa na MUNGU,Msidanganywe na hao wasio na imani.mimi nimepona kabisaaaaa!
ReplyDeleteMIMI NASHANGAA,WAZIRI WA AFYA,HIVI WATU WENGINE HUWA MNATENGA MUDA NA KUFIKRI NA BAADAE KUTENDA???HIVI HAO MNAOWAITA WASHAURI WAZURI NDIVYO WANAVYOWASHAURI KUKURUPUKA NA KUFANYA MAAMUZI YA KIHUNI??HIVI HUO UONGOZI MNAJUA NI KWA AJILI YA NANI??MNA LAANA NA SERIKALI YENU.DHAMBI ZENU ZIMEANDIKWA KWENYE KITABU CHA HUKUMU MBINGUNI:::::WAACHENI WANA WA MUNGU WAPONYWE NA MTUMISHI WA MUNGU::ZUIENI WAGONJWA WASIENDELEE KUJA KWA KUWEKA VIZINGITI BARABARA ZINAZOKWENDA KWA BABU WAKATI MAZINGIRA NA MIUNDOMBINU IKIBORESHWA!!!
ReplyDeleteNASIKIA HARUFU YA DECI, NGOJA MTAAIBIAKA MUDA SI MREFU MTAKAPORUDI MAKWENU NA BADO VIRUSI VINAPEKECHA. NAKUMBUKA KUNA JAMAA PAMOJA NA WAZIRI MWABULAMBO (SASA MAREHEMU) WALIFUATA KEMRON KENYA! WAKAAMBIWA DAWA HAIJAPIMWA WAO KICHWA NGUMU. HE SI WAKAFA! SERIKALI ACHENI WOGA WA BURE, SHERIA ZIPO, MTU HAWEZI KUAMKA TU AKAANZA KUNYWESHA WATU VITU VISIVYOJULIKANA ETI KAOTESHWA! NGOJA ATAKUJA MTU ANYWESHE WATU DAMU YA WATU KWA GEA YA KUOTESHWA NDIO MTAJUA UPOTOFU HUU. DUNIA NZIMA INATUCHEKA KWA KUNG'ANG'ANIA UPUUZI HUU.
ReplyDeleteHIVI NYIE SI NDIO MLIKATAA MAHAKAMA YA KADHI ETI ITATUMIA HELA YA SERIKALI? SASA KAMA HII DAWA NI YA YESU, MIUNDO MBINU YA SERIKALI MNATAKA YA NINI? HUDUMIENI WENYEWE BASI!
ReplyDeleteSERIKALI ACHA WOGA KAZA BUTI HAWA WASILAZIMISHE SUALA LA IMANI YAO TUGHARAMIE WOTE. YAANI KILA ANAYEKULA AKAVIMBIWA AKAOTA BASI ADAI MIUNDO MBINU? HAYA NA MIE PALE KIJIJINI NINA BABU YANGU ANATIBU MSHIPA LETENI MIUNDO MBINU HARAKA! TENA SITAKI MAHEMA NATAKA HOTELI YA KITALII, BARABARA YA VUMBI NOOOOO NATAKA YA LAMI AU VIGAE! DECI ILIKUWA HIVIHIVI WAKALIZWA. HUYU BABU KAKAA KIMJINIMJINI WACHA ATAKAPOWATOKA BARUTI NDO MTAJUA KAMA KASTAAFU AU LA! WAMAFIALE, VUTA NJULUKU ZA WAJINGA
Mimi nashangaa sana, sisi Wakristo tukipata kitu kizuri huwa hatubagui mtu. Tunahudumia wote. Lakini dini nyingine kwanza wanalalamika tusipewe hata barabara kwa ajili ya kusaidia wagonjwa. Wewe unafikiri hii dawa ingekuwa msikitini, wakristo mngesogelea? Si ndio hapo mngekatwa majambia. Ndio maana huyo jamaa hapo juu anapinga saana. Kisa udini. Sisi tutaendelea kung'ara tu kwa Msaada wa Yesu. na hatutamfanyia roho mbaya mtu wa dini nyingine. Ni nyie tu na roho zenu
ReplyDeleteKwenye kichwa cha habari kisaidizi kuna swala la Helicopter. Mbona ktk taarifa za ufafanusi hakuna habari hizo?
ReplyDeleteKama mnajua ni swala la kiimani kwa nini mnataka serikali igharamie miundombinu,??au ndio mnataka kutuambia ukristo ndio dini ya serikali.. Watanzania acheni kuwa na vichwa vya panzi,mtatapeliwa hadi lini?Mtakufa kwa kula takataka msizozijua kwa upumbavu wenu! Serikali imetoa imeeleza bayana kuwa kiutaratibu..hiyo dawa isajiliwe mamlaka ya chakula..hamjaelewa nini? Unadhani watu wakifa kwa kunywa dawa hii itatokea nini kama sio kuitwisha serikali mzigo usio wa lazima mara iundwe tume,mara uchunguzi..na hata nchi za wengine watatushangaa kuripoti maelfu ya watu wamekufa and we can not tell the source of the death!! Aisee sikujua kama watanzania badu mu-wajinga kiasi hiki!!Mnajigamba kila kukicha eti "mtanzania wa leo sio wa miaka ya nyuma.." Kwa taarifa yenu 80% ya watanzania bado mpo 50years back!!
ReplyDeleteKama ni swala la kiroho kama wanavyodai,basi acheni kuombaomba misaada mara miundombinu.Isitoshe huyu askofu Laizer anazeeka vibaya,haeleweki anataka siasa au anataka nini baada ya kuchoka migogoro na waumini wake kwenye makanisa,sasa kahamia kwenye nchi!!>>.Ni huyuhuyu aliyekuwa nyuma ya maandamano ya CHEDEMA arusha akimkataa meya,helikopta ya Ndesamburo kusaidia,loliondo....tukiunganisha wapembuzi wa mambo tunapata zaidi ya dawa.!
Kimsingi mi naona huyu mzee anaendesha mchezo mchafu na huu utapeli usitishwe mara moja.Kwanza ni mhujumu uchumi na ni fisadi kwa sababu tangu aanze kuchakachua hela za watu hajalipa kodi ya mapato anayopata,do you know this is an offense?Na hata huyu Laizer kuna 10% najipatia kwa huyu babu mchawi ndio maana anasapoti huu uchafu.
Yaani unaona wazi kuwa aliyeandika hapo juu March 13, 1:07 ni wa dini gani. Dini yake ni kutukana na kuuwa kwa majambia.
ReplyDeleteLa pili unaona chama chake ni CCM chama cha watu waliozoea vitisho na matusi.
Wee endelea na dini yako na sisi na dini yetu. Hujaitwa wala hujaalikwa
Jibu hoja,hatutaki kujua anayechangia anatoka dini gani na chama gani.
ReplyDeleteTiba iendelee, isisitishwe. Serikali acheni hizo!
ReplyDeleteASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema viongozi ndani ya Serikali, wamekuwa wakitenda mambo mengi mabaya dhidi ya wananchi na kuficha uozo wao kwa gharama yoyote.
ReplyDelete“Simameni daima katika ukweli; liwalo na liwe. Ukiogopa kufa leo utakufa kesho. Ukiogopa kusema ukweli leo eti ...kwa kuogopa kufa utakufa kesho,” aliasa watanzania Kadinali Pengo, kweli tumechoka tunataka mabadiliko.
Serikali iache kutuzingua, Huyo waziri anayesema dawa mpaka isajiliwe kwani zile zilizosajiliwa ndo zinaponya? acha watu wanywe dawa Mungu amekwisha isajili binadamu hataweza!!!
ReplyDeleteAnonymous wa March 13, 2011 12:18 AM umesomeka, tunakushukuru kwa kuwa mfuatiliaji. Kilichotokea ni kwamba hiyo element ya helkopta ilitufikia tukiwa tunakwenda mitamboni, hivyo tuliipachika kwenye page...yaani kwenye ukurasa ambao umeshapangwa ki-graphics kama unavyoonekana kwenye gazeti (hard copy)... hatua hii inakuwa imeshapita kwenye copy anayotumia webmaster. Hata hivyo, webmaster siku iliyofuata baada ya kuona gazeti, alibaini kuwa kuna headline saidizi ambayo haiko kwenye copy yake, akaipachika bila kuweka text yake ndani ya story. Sisi tunaoshughulika na hard copy, hatukuona haraka tatizo hilo kwa kuwa si wengi wanaopenda kusoma gazeti mara mbili (hard copy na kwenye web). Ni masuala ya kiufundi, next time tutayatazama.
ReplyDeleteMiruko
News Editor
Maoni ya wengi nimeyasoma, ila wengine lugha mbaya wengine mzuri basii! kama watu wamepona tunataka ukweli na ushahidi gani zaidi? Swala la dini linaingiaje hapa? Swala la muhimu ni huduma kwa jamii! Na serikali iangalie maslahi ya wananchi wake! Nilisikia mpaka viongozi wa juu kabisa wa nchi hii walishaenda huko! kama wamepona kwa nini wasiweke hadharani ushuhuda wao? Ugomvi na kejeli tuache kwani kama ni ya Mungu yateandelea na kama ni ya wanadamu basi yatakuwa na ukomo! Katika hayo yote tumshukuru Mungu kama watu wanapona na serikali itoe mazingira mazuri zaidi kwa huyo mchungaji kuhudumuia Taifa la Mungu!
ReplyDeleteMimi naona serikali isiwazuie watu ambao tayari wapo kwenye folen ila watafute njia mbadala ya kuwasstopisha ambao hawajaanza safari kwani walioko kwenye foleni wameshatumia garama nyingi sana kuwarudisha itakuwa nikuto kuwajali wao wajiulize ingekuwa ni wao wanafanyiwa hivyo wangejisikiaje?
ReplyDeleteKwa mtazamo wangu, swala la dini ni silaha hatari sana.Kwanza imani inatofautiana uwe muislamu au mkiristo, ukizingatia serikali haina dini na kazi ya serikali ni kulinda imani ya watu.kwa maana hiyo sasa serikali ifanye kazi yake na iache siasa kwa wananchi.
ReplyDeletePili, kama dawa inaponya watu na hakuna ambaye amedhurika yes,ni dawatoka kwa Mwenyezi Mungu and we should appreciate that.Mungu katumia mtu wake kuonesha dawa baada ya mateso makubwa inayokumba dunia.Watanzania mbona hatujiamini pale inapokuwa imetokea dawa ya kutuponya? au mlitaka dawa ingundulike ulaya ndo mgeamini? Be proud of your country, acha udini na ukabili. Serikali play your role to ensure kila mtu anapata tiba kwa amani na wengi zaidi waongezeke ili Tanzania lisiwe taifa la maradhi (Disease free zone).Mungu amtangulie mchungaji na aendelee kumpa nguvu ya kuponyesha wengi na asiyumbishwe na mtu wa dini yeyote.
Baadhi ya wachangiaji wanaotaka dawa ikapimwe...! Swali; je hizo Mnazokunywa huko kwa waganga wa kienyeji zimepimwa na nani? Acheni maneno mbofumbofu.
ReplyDelete