14 March 2011

Kiongozi wa TASWA kuula serikalin

Na Amina Athumani

SERIKALI imesema itamjumuisha kiongozi mmoja wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kwa ajili ya kumwingiza
kwenye Kamati ya Uhamasishaji wa Michezo.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, katika bonanza la waandishi wa habari lililoandaliwa na TASWA na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Emmanuel Nchimbi,  alisema kutokana na juhudi zinazofanywa na TASWA katika kuhakikisha michezo inakuwa, atamteua kiongozi mmoja wa chama hicho katika kamati hiyo.

Alisema kamati ya uhamasishaji itaundwa hivi karibuni na serikali, ikiwa na lengo la kuhamasisha michezo mbalimbali iliyopo nchini ili iweze kufanya vizuri na kuitafutia njia mbadala ya kuondokana na matatizo mbalimbali yanayoikabili michezo hiyo.

"Nawapongeza sana TASWA kwa kubuni kitu cha namna hii,  bonanza hili linawakutanisha wanahabari mbalimbali, mnapata nafasi ya kufahamiana na kufurahi pamoja, nami naahidi katika kamati ya uhamasishaji itakayoundwa na serikali,  nitamteua kiongozi mmoja wa TASWA," alisema Waziri Nchimbi.

Waziri huyo ameipongeza TBL kwa kudhamini bonanza hilo kwa kila kitu TASWA kuanzishwa kwake hadi leo na kuwaomba kuendelea kulidhamini.

Katika bonanza hilo, Mwandishi wa gaazeti hili, Mwali Ibrahim,  aliuka kinara wa kucheza muziki kwa mitindo ya mugongo mugongo na sugua kisigino zilizokuwa zikiporomoshwa na bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta' na kuzawadiwa fedha talsimu sh. 50,000.

Katika michezo mingine, Business Times Limited (BTL),  ilifanikiwa kutinga hatua za nusu fainali katika michezo ya soka na wavu.

No comments:

Post a Comment