10 March 2011

TANROADS yaanza kumwelemea Magufuli

*Adaiwa kujali sifa binafsi si matatizo ya wizara

Na Mwandishi Wetu

WAKATI hali ya mambo ndani ya Wizara ya Ujenzi  ikiendelea kuwa tete, waziri wa wizara hiyo, Dkt. John Magufuli amerushiwa
lawama kwa kile kilichoelezwa kuwa kutotilia maanani matatizo ya ndani, badala yake kuweka kipaumbele kwa majukumu ya kisiasa yanayompa sifa binafsi.

Chanzo cha kuaminika ndani ya wizara hiyo kimeliambia gazeti hili kuwa imani waliyokuwa nayo wafanyakazi hao inazidi kushuka siku hadi siku kutokana na Dkt. Magufuli kushindwa kupatia ufumbuzi wa haraka kero zilizodumu kwa muda mrefu ndani ya wizara hiyo ikiwemo uteuzi wa wakala mbalimbali ikimewemo TANROADS.

"Wizara ya Ujenzi chini ya mheshimiwa Magufuli imepoteza mwelekeo kwa kile tunachoona, ameweka kipaumbele zaidi kwa shughuli zinazompa sifa binafsi, anatafuta 'cheap popularity' kwa wananchi na kujisahau kutekeleza vipaumbele vya majukumu muhimu ya Wizara yake," kilisema chanzo hicho na kuongeza;

"Inashangaza waziri kutembelea mikoani na kuwaamrisha wakuu wa mikoa na wilaya kuwaweka ndani makandarasi bila kufuata taratibu. Jambo hili analifanya kienyeji sana 'unprofessional.' Kuna utaratibu wa mambo yote kwenye mikataba na hatua za kuchukua kama mkandarasi anashindwa kufanya vizuri. 

"Tatizo ni kwamba waziri hajui na hataki kujua labda kuponzwa na sifa anazomwagiwa na wananchi, ndio maana anaacha huku wizarani mambo yamelala wala haoni umuhimu wa kuwateua watendaji wakuu mapema."

Majira lilidokezwa kwamba tangu Dkt. Magufuli arudishwe  wizarani hapo, kurugenzi na wakala zote za wizara zimeendelea kuwa na watendaji wakuu waliokaimishwa kwa muda usiojulikana.

"Hii imetuchanganya kwani tuliamini Mheshimiwa Rais Kikwete ametuletea Magufuli akiamini kwamba ana uwezo wa  kudhibiti hali mbaya ya wizara na wakala zake. Badala yake Mheshimiwa Waziri yuko moto kutoa amri nzito zinazompa sifa binafsi, hata wakati mwingine kuvuka mipaka bila kushirikisha  wakuu wake wa kazi."

"Kwa mfano amri za bomoabomoa nchi nzima na amri  za kuwatisha makandarasi bila kufuata taratibu ni hatari katika kipindi hiki ambacho serikali inakabiliwa na changamoto nyingi juu ya kero za wananchi ambazo hazijazipatiwa ufumbuzi.

"Kwa ujumla wizara imepoteza mwelekeo, badala ya kuwa wizara ya kujenga, imekuwa ya bomoabomoa. Ikumbukwe kwamba hata hayo mabango yaliyowekwa barabarani yaliwekwa kwa ridhaa ya serikali hivyo kuyaondoa ni vyema utaratibu ukafuatwa kuepuka kuiingiza serikali katika kesi za fidia kama ilivyojitokeza katika uuzaji holela wa nyumba za serikali, Dowans nk. Hivi sasa  wizarani hakuna anayejua afanye nini zaidi ya kusubiri utekelezaji wa Waziri Magufuli."

Chanzo kingine ndani ya Wizara hiyo kilisema hatua ya Dkt. magufuli kuchelewa  kupanga miundo na watendaji wakuu wizarani na kwenye wakala imechangia kupunguza kasi ya utendaji wizarani hapo.

"Nashindwa kuelewa kwanini anachelewesha jambo hili au hajapata anaowataka yeye? Waziri Magufuli anasifiwa sana na wananchi wa kawaida ambao wao hawaoni kasoro hizi. Huenda amejisahau kwa sifa hizo na kusahau majukumu yake mengine ya ndani ya wizara. Aangalie matatizo yaliyo ndani ya wizara na kuyashughulikia haraka."

Vyanzo hivyo vilimshauri Dkt. Magufuli kutumia muda mwingi zaidi kupanga safu za wizara yake bila upendeleo ili kukabiliana na majukumu mazito yanayoikabili wizara na kuleta mafanikio kwa serikali na taifa kwa ujumla.

Majira lilipomtafuta Dkt. Magufuli simu yake iliita bila kupokelewa. Lilipotuma ujumbe wa maneno kuomba apokee simu, lilijibiwa kuwa "Unayemtafua yuko Kagera."

Lilipompigia simu msaidizi wake aliyefahamika kwa jina moja la Samike, alisema katibu mkuu ndiye mwenye jukumu la kutoa ufafanuzi wa masuala yote yanayohusu wizara hiyo kwa kuwa ndiye mtendaji mkuu.

12 comments:

  1. NI UKWELI USIOPINGIKA MAANA SIFA ZA NJE HAZIKUSTIRI MWISHO NI KUPOROMOKA, INABIDI AKAE NA NAIBU WAZIRI WAKE NA MAKATIBU WA WIZARA IPANGE MIKAKATI,MAANA HIYO WAZARA INA KERO NYINGI SANA SIO HIZ ZINAZOONEKAN KWA NJE LAKINI KUNA MOTO UKO NDANI YA MAJIVU!!NA UKIZINGATIA KATIBU MKUU ALIYEBOBEA KWA .....CHAMBO SASA KAHAMISHWA

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  3. "Hii imetuchanganya kwani tuliamini Mheshimiwa Rais Kikwete ametuletea Magufuli akiamini kwamba ana uwezo wa kudhibiti hali mbaya ya wizara na wakala zake. Badala yake Mheshimiwa Waziri yuko moto kutoa amri nzito zinazompa sifa binafsi, hata wakati mwingine kuvuka mipaka bila kushirikisha wakuu wake wa kazi." Kilisema chanzo

    Hii kauli ni ya mtu anayetaka kutudanganya kuwa Kikwete atoe maamuzi kwa kila kitu Dk Magufuli anachotaka kufanya. Kikwete sio mtendaji mzuri na hilo linafanya asiwe na sifa ya kuamua maamuzi mazito. Kwani meli ya kuvua samaki, ambayo Maguduli aliikamata, sasa hivi watuhumiwa wako wapi? Hatuna serikali makini, hivyo mawaziri wachache wanaofanya kazi kwa umakini hawathaminiwi.

    Ni kawaida kwa Magufuli kusimamia kwa umakini, hata Kikwete anafahamu hilo. Tatizo huyu mlalamikaji anataka hapo wizarani wanunuliwe mikate na vitumbua kila siku halafu ndo Magufuli aende kufanya kazi za nchi. Kama mlikuwa mmezoea mbwenyenyo kutoka kwa mawaziri waliopita, hapo mmekikwaa kisiki cha mpingo. Magufuli hafanyi kazi kwa kutaka sifa, huyu ni kiongozi makini na anayejua kuwajibika.

    ReplyDelete
  4. wewe mlalamikaji unalako jambo au unataka position flani, ndo maana unapiga kelele, magufuli hana muda huo maana uwozo uliopo ni mkubwa sana, kwa hiyo anatakiwa kufanya hivyo sasa wewe unataka awe anakaa ofisini anangalia CNN

    ReplyDelete
  5. Tumemkubali Magufuli kwa Utendaji wake Tangu zamani, Hao wanaolalamika either wamenyimwa ulaji au wanatafuta naafasi. Sikubaliani na malalamiko hayo. Tunataka Kiongozi anayeshinda Field siyo ofisini.
    Kwa kuonesha kuwa hizo ni chuki binafsi dhidi ya magufuli walala mikaji hawataki hata kutaja majina yao.

    Sifa binafsi za kiongozi mzuri zinajulikana kwa watu wote mahala peupe. Sasa mtu akifanya kazi jamii ikamkubali mnasema anajipendekaza anatafuta kukubalika. huu ni upuuzi. Sishangai huu mfumo wa serikali yetu ambayo hamtaki watu wafanye kazi wakubalike na jamii.

    Magufuli endelea sisi wananchi tunakukubali anachana na hawo waliokaa ofisini wanasubili wapewe madaraka.

    ReplyDelete
  6. NAKUBALIANA NA WALALAMIKAJI. HUU SI MTINDO MZURI WA KUFANYA KAZI KAMA WAZIRI. HIVI SASA NCHI INADAIWA FIDIA YA MABILIONI ALIYOSABABISHA MAGUFULI KWA KUVUNJA MIKATABA YA WAKANDARRASI WAKATI WA MKAPA. WATZ MJUE HILO.

    SUALA SIO WANAOLALAMIKA WANATAPA POST, ,ISHU NI KWA KIASI GANI BW. POMBE ANAFANYA WIZARA HIYO IFANYE KAZI KAMA TIMU MOJA. KAMA ANADHANI ANAWEZA KUFANYA MWENYEWE BILA WASAIDIZI WALIO NA MAMLAKA AENDELEE.

    ReplyDelete
  7. Majungu ndo hayo sasa mmeanza waswahili haya kazi kwenu na waziri wenu. Mmekaa sikuzote na kawambwa mkiwa na viongozi wote katika idara na wakala zenu zote na viongozi wake mlichokifanya tumekiona ni ufisadi tu mmeongeza garama za ujenzi barabara za lami bila sababu. sasa mmebanwa ndo mnajifanya anajitafutia sifa. Kwendeni zenu wanafiki na mafisadi wakubwa nyinyi.

    ReplyDelete
  8. Watanzania tuna laana tena kubwa sanaaa. Kwa hiyo kukaimu ndo shida kama mnaona kukaimu ni kushindwa kuimizawajibu wenu si muwapishe watanzania wenzenu? acheni majungu na fitina jamani. tunawaziri kibao wababaishaji hata hawajulikani wanachokifanya mwaka mzima kila siku worksho/semina/meetings hakuna kitu sasa mnaona mchapakazi kaja mnalalamika. poteleeni mbali huko

    ReplyDelete
  9. KWAHIYO JK ALAUMIWE KWANI POMBE AMESHAITIA SANA HASARA NCHI KWA UTENDAJI WAKE IMEKUWAJE AMEMRUDISHA TENA UJENZI? INAMAANA RAISI HANA TAARIFA ZA HASARA ALIZOSABABISHA POMBE?

    ReplyDelete
  10. achane mambo ya ajabu walalamikaje mmezoea ubwete sasa mtu wa kazi anafanya kazi yake mnaanzakumpima na mtampimasana tu mtabakia kulalalika siji watanzania tuna matatizo gani kiukweli maana hadi inatia hasira kwa kiasi kama hiki upuuzi mtupu watu wakikosea mnalalamika wakichapa kazi mnalalamika eti wanataka sifa pumbavu zenu

    ReplyDelete
  11. Mimi nashindwa kuelewa Tanzania tunaelekea wapi? siasa zimewapumbaza watu kuanzia viongozi na wananchi. Hivi inaingia akilini kweli Mtendaji Mkuu wa wakala anateuliwa na magufuli na siyo anaomba kazi kwenye board. kama utaratibu ni huo basi kwa mheshimiwa huyu mpenda sifa kazi za wakala wa amjengo, Barabara, Temesa na nyingine zilizochini yake magufuli basi hazitajazwa leo maana ninavyomuona kwa kuwa amepewa meno basi atalipa visasi. Pale wizarani kwa mfano kuna wahandisi ambao walienda kugombea ubunge hao wasitegemee kitu na badala yake wanaweza kufukuzwa. Anachofanya Magufuli ni kuteua wale wanaomnyenyekea akishindwa kujua kuwa nafasi hizo zinataka sifa za elimu siyo siasa. Ninashauri wizara ibadilishe utaratibu iachie bodi au tumieni makampuni ya ushauri katika kutafuta wataalamu hao na sio magufuli.
    Pia nampongeza Waziri Mkuu kwa kumpunguza kasi yake ya kubomoa bila sababu za msingi. Nilidhani angetumia tu akili yake ya kuzaliwa na PhD yake kujua kuwa pale ambapo barabara hazijengwi sasa hakuna haja ya kubomoa. Hii inawapa wananchi matatizo na kuwaacha bila makazi ambayo mtu wa kawaida kujenga nyumba aliwanyima wanae chakula akajenga kibanda chake leo kinabomolewa bila sababu ya msingi. Magufuli asifikiri kuwa kubomolea watu ndio atapata huo urais anaotaka.aelewe kuwa ni watu wachahce mno wanaompa sifa za kijinga na yeye amejawa na kulewa sifa hizo. Be aware John

    ReplyDelete
  12. Watanzania acheni unafiki huyu Dr. magufuli siyo kama anataka sifa huyu anawajibika na kufata sheria unajenga barabarani unategemea nini hiyo wizara malalamiko kutwa tumechoka magufuli kaza uzi hawa wanaokushangaa ndiyo wale watu wasijuwa nini maana ya UZALENDO (infasracture) imekufa watu kujenga bila mpangilio mfano ni pale bonde la jangwani licha ya kuona kuna hatari ya maji kujaa lakini wapi na ipo siku wakijahamishwa kuna watu watapiga kelele angalau walikwisha katazwa, sasa malalamiko ya hao watu wizarani ni ulaji wameminywa sasa hivi lawama magufuli wapenda maendeleo tunakupa hongera Dr MAGUFULI

    ReplyDelete