*Asema viongozi maslahi wasio na historia wanaiua CCM
*Asisitiza kauli zake ni taratibu hazihitaji vikao
*Sitta ataka CCM isishangae kukosolewa na wapinzani
Na Mwandishi wetu
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinaathiriwa na viongozi maslahi wasio na
upeo wa kujua yale wanayosema yanakisaidia au kukiangamiza chama hicho katika siasa za ushindani wa vyama.
Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Waziri Mkuu mstaafu, Bw. Frederick Sumaye katika mahojiano maalumu na gazeti hili kuhusu kauli zilizotolewa dhidi yake na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda wa CCM, Bw. Hiza Tambwe.
Bw. Sumaye ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), alisema baadhi ya viongozi waliopewa madaraka hawana historia na chama hicho na hawaelewi namna kauli zao zinavyokiathiri chama jambo ambalo sasa ni kero kwa wanachama na watu wenye uchungu wa kweli na CCM.
"Baadhi ya watu wanaokisemea chama sasa hawana historia na CCM, hawana upeo wa kujua yale wanayoyasema yanasaidia au kukiumiza vipi chama. Hii ni kero ndani ya chama hususani kwa watu wenye uchungu wa kweli na CCM," alisema Bw. Sumaye.
Hivi karibuni Bw. Sumaye alikaririwa na gazeti moja akikishauri chama chake kusimama kukabili hoja mbalimbali zinazotolewa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) badala ya kuiachia serikali peke yake kufanya hivyo.
Bw. Sumaye alionya kwamba si sahihi kwa CCM kukaa kimya wakati wapinzani wanaishataki kwa wananchi kuwa imeshindwa kazi, hivyo makada wa chama hicho wanapaswa kuchukua jukumu hilo haraka.
Kufuatia kauli hizo, Bw. Tambwe alikaririwa na gazeti jingine akimshambulia Bw. Sumaye kuwa kauli zake hazikuwa za kiungwana na zililenga kukishambulia chama hicho.
Alidai kwamba kauli hizo zililenga kujenga chuki miongoni mwa wanaCCM na ni chokochoko zinazotolewa na watu wenye nia ya kuwania urais mwaka 2015. Aliongeza kuwa si sahihi kwa mawaziri wakuu wastaafu kutoa ushauri barabarani kwani huko si kukijenga chama bali ni kukibomoa.
Akijibu hoja hizo Bw. Sumaye alisema alichoshauri ni taratibu za kawaida za chama ambazo hazihitaji kikao kwani siku zote CCM inapokuwa na jambo viongozi hufanya mikutano ya ndani na nje kuuhamasisha na kuuelimisha umma.
"Ni taratibu za kawaida za chama, wala hazihitaji kikao kwa sababu siku zote kinapokuwa na jambo viongozi hufanya mikutano ya ndani na nje, kuhamasisha na kuelimisha umma," alisema Bw. Sumaye na kuongeza;
"Nilichosema mimi hii kazi wanayofanya CHADEMA ni kuhamasisha umma na kazi ya siasa na viongozi wetu (wa CCM) katika ngazi mbalimbali wafanye vikao na kuelimisha umma. Hili kweli linahitaji mpaka nilisemee kwenye vikao?" alihoji Bw. Sumaye.
Alizidi kueleza," Nilitegemea Idara ya Propaganda iwe mbele badala ya kupambana na sisi tunaotoa ushauri mzuri kwa chama chetu, iandae utaratibu mzuri kuanzia ngazi za chini namna ya kuhamasisha na kuelimisha umma. Nashangaa sana Mkurugenzi wa Propaganda kusema navuruga chama, eti namtwishwa gunia la misumari mwenyekiti!
"Nilichofanya ni kumpunguzia kazi mwenyekiti wetu. Nataka viongozi wengine wa chama chetu wafanye mikutano ya siasa. Kumwachia mwenyekiti pekee ajibu hoja kwenye hotuba zake si sahihi, chama kimsaidie hiyo ndiyo kazi ya viongozi ndani ya chama.
"Kimsingi sioni kosa nililofanya. Nashauri Idara ya Propaganda ijipange katika ngazi mbalimbali za chama kujibu hoja hizi za CHADEMA zinazochafua chama chetu," alisema.
Akizungumza kwa kujiamini Bw. Sumaye alisema hakudandia ndani ya CCM, historia yake ndani ya chama hicho ni ndefu kwani aliingia Umoja wa Vijana wa TANU mwaka 1969 akiwa sekondari Ilboru na mwaka 1972 alijiunga na TANU kabla ya mwaka 1977 alipokuwa miongoni mwa wanachama waanzilishi wa CCM.
"Chama hiki nimeingia kwa ridhaa yangu kutokana na kukipenda. Sikuingia kutafuta maslahi wala umaarufu kwa matusi. Tangu nimeingia CCM nimekuwa kiongozi. Nina historia ndani ya chama na nazielewa taratibu za chama chetu," alisema Bw. Sumaye.
Alisema jambo lingine linalokiathiri chama hicho ni mtazamo finyu wa baadhi ya viongozi ambapo mtu akitoa jambo lolote anasingiziwa kutaka kugombea urais mwaka 2015.
"Sasa hebu jiulize kama unataka kugombea urais, akili za kawaida zinakubali eti uanze kukivuruga chama chako hicho hicho unachokitegemea ugombee! Kwa nilichosema suala la urais halipo, nimezungumza kama kiongozi wa chama, kudhani hayo ni mawazo finyu. Kama ni hivyo si ningejipendekeza basi nisikivuruge ndio maana waingereza wanasema "common sense is not common" (Busara ya kawaida ni adimu)
"Nazidi kusisitiza kuwa, lazima chama kisimame tusijekuwa tumekaa tu huku upinzani unajenga hoja lazima tuchukue hatua kwa hali hiyo," alisisitiza.
Alielezea kuwa madai kwamba anamtwisha rais gunia la misumari hayana msingi kwani ingewezekana vipi asimame kidete wakati wa kampeni kumnadi na kuhakikisha anaendelea kushika usukani, leo amtwishe gunia la misumari!
Sitta na CCM kukosolewa
Katika hatua nyingine, mwandishi wetu Wilhelm Mulinda anaripoti kutoka Mwanza kwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Samuel Sitta amesema kuwa hakuna haja ya kuwashangaa wapinzani wanaokikosoa CCM kwa vile ni wajibu wao kufanya hivyo.
Bw. Sitta ambaye pia alikuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kipindi kilichopita, aliyasema hayo jana jijini Mwanza wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mahojiano.
"Wala tusiwashangae wapinzani kuikosoa CCM kwani hawawezi kuifisia. Na wao wanataka siku moja wapate nafasi ya kuongoza nchi hivyo katika mazingira hayo hawana sababu
ya kuisifia CCM ambayo iko madarakani," alisema.
Bw. Sitta alisema kuwa wakati sasa umefika kwa CCM kujipanga kikamilifu na kuachana na ukiritimba wa mfumo wa chama kimoja cha siasa uliokuwepo zamani ili kukabili mikikimikiki ya ushindani wa kisiasa nchini katika wakati huu wa mfumo wa vyama vingi.
"Jamani ukiritimba wa mfumo wa chama kimoja cha siasa umekwisha hivyo ushindani wa kisiasa unaotakiwa kwa sasa ni lazima ni lazima kuukabili kwa kushindana kwa hoja
ili kueleweka kwa wananchi na si vinginevyo," alisema,
Aidha Bw. Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo mkoani Tabora alisema kuwa haina maana kujitapa wakati wa ukame kwa vile tatizo hilo ni janga linalotishia maisha ya watu linapoingia katika nchi yoyote ile duniani.
Alifafanua kuwa ukame ni tatizo kubwa ambalo linatakiwa kutafutiwa ufumbuzi pale dalili zake zinapoanza kujitokeza kwa ajili ya kuwanusuru wananchi wasiathirike kutokana na hali hiyo badala ya kujitapa. Hata hivyo, Bw. Sitta hakuelezea alichomaanisha katika kauli yake hiyo.
Bw. Sitta alikuwa jijini Mwanza kwenye mkutano wa mawaziri na makatibu wa kudumu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo wanachama wake ni nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Mimi sina chama lakini nimekuwa nikifuatilia kauli za Tambwe na Makamba kwa kweli alichosema Sumaye ni kweli awa watu wanakipeleka chama chao pabaya
ReplyDeleteAhsante Mh. Sumaye. Nilikuwa natafuta sana neno litakalowafaa watu kama Tambwe, na leo nimelipata. Ni kweli, mtu kama Tambwe ni kiongozi maslahi. Anachoongea anaongea ili asikike ameongea, hata kama anaongea pumba. Kwa akili yake, akiongea anasitiri nafasi yake katika chama, lakini mengi ya yale anayoongea hayana tija. Tambwe ni kama mpiga debe, yupo tu kituoni, atapiga kelele "posta,posta" ilhali akijua watu wote wanajua gari ni ya posta, na kuja kwao hakutokani na kelele zake. CCM kimejaza watu wa namna hii wengi tu, na ndiyo hao wanaolalamikia mikutano ya Chadema huku wamebweteka chini. Ule uzoefu wa ukiritimba wa chama kimoja umeozesha akili za watu wengi CCM, mpaka wamejisahau na wanaona kama Chadema hawana adabu kukisema CCM. Wanasahau kwamba CCM, CHADEMA, NCCR, CUF na vyama vingine, wapo katika kutafuta nafasi ya kuongoza nchi na hivyo wanapaswa kuteka fikra za wapiga kura, ambao wengi walikuwa bado wako chini ya uvuli wa hofu, kutojiamini, na mashaka waliyokuwa wamejengewa tangu enzi za TANU. CHADEMA wanachofanya sasa, ni kuondoa hizo hofu, ili kuwapa wanaowasikiliza, ujasiri wa kutafuta njia mbadala wa kuondokana na dhiki hii inayowaatamia sasa. Kama CCM itaendelea kubweteka kusubiri kudra za jina la Nyerere, safari hii watashangaa. Huu sio tena wakati wa akina Tambwe, ni kipindi cha " ujanja kuwahi " maana hata vitabu vya dini vinatuasa, " asiyefanya kazi na asile."
ReplyDeleteHao Tambwe na Makamba ni makenge sasa. Hata Lowassa anaafadhali kwani anafikiria vizuri kuliko vikaragosi washenzi hao. Wanaharibu kabisa sifa ya chama.
ReplyDeletesumaye na sita bg up yani mko juu juu zaidi. maana nyinyi ni viongozi wa ccm kama mnayaona makosa yanayofanywa ndani ya chama amna haja ya kufumbia macho.ata kama wao wanawalaum ni ufinyu wa akili na uwezo mdogo wa kufikria na kujua/kutambua wanatoka wapi, wako wapi, na wanakwenda wapi? ili ndilo jambo la kwanza kutambua kabla ya yoye. maana ufinyu wa fikra zao ndio maana mtu akitoa ushauri ndani ya ccm kama mwana ccm wana muona kama mpinzani. inamaana wao awategemei mwanachama wa ccm kutenda yaliyo mazuri ndani ya ccm, inasikitisha sana. pili najiuliza sipati jibu kweli familia zao wanaziendeshaje? nina washauri viongozi wote ndani ya ccm ata vyama vya wapinzani kama mtu hajuu utu wa mtu na jinsi ya kuongoza arudi kwa wananchi wampe mawazo wanataka nini na kipi hawataki, maana nimetambua kuwa wenzetu kukosa utendaji mzuri kwasababu awakope akili kutoka kwa wananchi kujua wanataka nini? wakisha tambua ilo nadhani kila kitu shwali. ccm jurudi kuweni waungwana katika kazi zenu kwa jamii. ccm kumbuka maji yakimwagika hayazoleki.
ReplyDeletemwizi mkubwa we sumae huna lolote scandnavia kuondoka kwako imefilisika mwizi tu nawe ndio hao hao kina slaa hamna lolote simnatoka wilaya moja na slaa kajiunge nae tu wala usione aibu mpuuzi we wala usijidanganye kutafuta umaarufu nafasi tena ndani ya nchi hii huna tena nawe sita usibabaishe watu babake mboe umefanya nae kazi watu wanakulinda tu ndani ya ccm wewe na mzee mboe sindio pia mmewafikisha wabongo hapo walipo?mikataba na ubinafsishaji wa mashirika ulikuwa ukiongozwa na nani?kama si ww na babake mboe?tunayajua yote hatuja sahau usijifanye unabusara huna chako yote kuukosa uspika jiuzulu kavae nguo za kaki kama kuruti wa jkt
ReplyDeleteHata hiyo afadhali ya Lowassa siioni. Tatizo kubwa la viongozi wa CCM wanahisi kwamba wataendelea kuongoza nchi hii kwa kucheza na akili za watu maana wao ndo wenye akili za kutosha kuzidi wengine. Ki ukweli CCM wanatakiwa kufanya kazi ya kutosha ila kama bado inaendelea kuwakumbatia viongozi wenye maono ya kina Lowasa, Makamba, Tabwe Hiza nk, basi tuusubiri mwisho wa CCM ambao nauona hauko mbali sana.
ReplyDeleteJamani nampenda SITTA sana, thxs SUMAYE kwa kutuunga mkono, tumeelewa ushauri wako vizuri sana. MUNGU AWABARIKI!
ReplyDeleteNa BADO SSM mwaka huu lazima shetan alaumiwe;
ReplyDeletemjomba ukishangaa vituko vye CHADEMA utaona
UKAHABA wa SSM.
hivi jamani huu urais mnaoutamani mbona utawamaliza wengi? kwa staili hii GIZA LINAFUNIKA SSM
hongera sitta na Summaye waambieni wenzenu ukweli waachane na uchawi wafanye siasa.
Ama kweli sikutegemea hivi karibuni kuona chama chenye upinzani wa kweli. Tukumbuke upinzani utakiamsha chama kilicho madarakani. Hii itakifanya chama kinachotawala kuwa makini katika kuendesha nchi, kuleta maendeleo kwa wananchi na kuheshimu misingi ya utawala bora kama vile kupambana na mafisadi na ufisadi. Hivyo basi mimi kwangu naona CHADEMA wanafanya kazi yao wanavyotakiwa. CCM wamelala. Hivyo tulioyaona katika uchaguzi uliopita 2010 tusishangae yakawa mara dufu na kuleta mabadiliko ya chama tawala 2015. Ile kauli ya "how luck to lead fools" inasafishwa na upinzani kama huu. Viongozi wanaokisemea chama cha CCM ni wazalendo wa kweli kwani wanaona wanayo nafasi ya ku hamasisha chama chao ili kuweza kupambana na wapinzani. Na kwa kufanya hivyo matokeo ni manufaa ya kufanya vizuri kwa chama chochote kilicho madarakani. Huyo anayelenga kukosoa personalities asitunganganye. Alikuwa wapi siku zote kuwakosoa na mbona Sumaye na Sitta tunawajua kama viongozi ambao walikuwa si mafisadi kama anavyotaka kuwaanika leo hii? Be to the point man. Kama huna cha kuchangia hapa kaandike majungu na fitna yapo magazeti mbona mengi tuu kwa ajili hiyo?
ReplyDeleteCCM YA LEO INA VIONGOZI WENGI TU MASLAHI SUMAYE,SITA WANASEMA UKWELI NA UKWELI UNAUMA NIMESUHUDIA WAKATI WA KAMPENI RAISI WETU ANAMPIGIA DEBE MBUNGE WA KIBAHA VIJIJINI KUWA NI MTU MAKINI NA KIONGOZI ATAKAE WAFAA WANA KIBAHA NIKAJUA RAISI KADANGANYWA NA KADANGANYIKA LAKINI JE WANANCHI WATADANGANYIKA KWA UTENDAJI WA MBUNGE MTEULE?CCM INAHITAJI MABADILIKO YA KWELI IKIWA KURUDISHA MISINGI YA AZIMIO LA ARUSHA.
ReplyDeleteTambwe Hiza ni shetani alielaniwa -hana maana hata kidogo.Tatizo la CCM ikiona mtu anapiga kelele sana kukulaumu -badala ya kummaliza kwa hoja wao huona wamnyamazishe kwa kumpa uongozi ndani ya CCM-Hii ni dalili ya Chama dhalim na kisicho makini
ReplyDeleteMWAKA HUU KITAELEWEKA
Siku zote mtu anayesema ukweli hapendwi (hasa na yule anayemkosoa). Ushauri wa akina Sumaye na Sitta si wa kupuuzwa na wana ccm. Mimi ni mwana ccm, lakini ukweli ni kwamba kama tutaendelea kuwakumbatia watu waliofilisika "HOJA" kama Tambwe na Wasira, tujue tunaendelea kuchimba kaburi la CHAMA CHETU (CCM)hapo mwaka 2015. Naomba tujifunze kwa wenzetu Kenya, waliitetea hivyohivyo KANU yao, na matokeo yake mnayaona.
ReplyDeleteNawashauri viongozi mlio juu, tukae chini na tutafakari kwa undani Mustakabari wa chama chetu. Mbonao makada wazuri na wenye busara wanaoweza kukishauri vyema chama, chukulia watu kama akina Dr. Salm, Butiku, Mwakyembe, Marchela, Anna Kilango, Sitta, Sumaye, Mkapa, na wengine wengi. Lakini wote hawa tunawaacha pembeni tunabaki kukumbatia hawa watu waliofilisika kimawazo na wasio na hekima, wanaolopoka badala ya kutumia vichwa vyao! WATATUMALIZA AISEE.
Mwisho tunapaswa kujua kuwa kwa uhakika hawa CHADEMA, hawalali! eebu, angalia, kila siku wanakuja na mbinu mpya, mara Operation Sangara, mara shitua mbavu, mara elimu ya uraia, n.k, hizi zote ni mbinu na zote zinagusa maisha ya mtanzania wa kawaida. Kuwa na dora isiwe sababu, wananchi wa leo wako macho kweli kweli, hawadanganyiki. Tunachopaswa kufanya ni KUFANYA KAZI so BLA BLAA.
Hakuna mtu mkamilifu hasa katika kuongoza nchi kama jamhuri ya Tanzania.Kitachotakiwa hapa ni kwamba:
ReplyDelete1.wote wenye kashfa kubwa hasa za upotevu wa pesa za serikali wakati walipopewa nyadhifa kadhaa wasipewe nafasi katika siasa na baadae tuwashitaki.
2.Wafanyabiashara wasipewe madaraka kwenye siasa.
3.Tuache kuwapa watoto wetu na marafiki vyeo mbalimbali katika serikali.
4.Tusimlaumu mtu anayetaka kusema ukweli,tumwache aseme ukweli wake kwa umma.Kama amepotosha umma wa watanzania tumshitaki kadiri ya sheria za nchi.
5.Siku hizi hakuna siri kwa sababu dunia imeshaingia kwenye daraja lingine kimaendeleo.Hivyo viongozi waliozoea mambo ya kizamani wajihadhari na mienendo yao.
Kama ukitaka kuishia mwisho mzuri ni lazima njia ulizotumia kufika hapo ziwe nzuri.Ukifanya ujanja ujanja kupata kitu fulani yatakutokea puani.Hao akina Tambwe,Rosta, na wengine mnawajuwa...si muwatoe kwenye vyeo tusiwasikie kwa sababu wanaweka madoa ambayo si rahisi kuyafuta.
ReplyDeleteNinachowaomba watanzania waache matusi. Tumepewa nafasi ya kutoa maoni kutukana watu ya nini?Toa ushauri wako upingane kwa hoja. Kama ushauri unaona haufai, basi toa unaofaa.
ReplyDeletesijasikia alichojibu bwana Tambwe lakini nimewahi kumsikia mara kadhaa akihojiwa vituo tofauti vya habari hana upeo wa kutambua mambo nadhani viongozi wengi hasa wa chama tawala wapo kwa maslahi fulani na kusifia watu fulani ili waendelee kuwa katka hayo madaraka,wasikilizeni wazee wanaokijua chama la sivyo hakuna asubuhi
ReplyDeleteHuyo mtu alishemshambulia Sitta na Sumaye ana lake jambo. unataja wizi wa Sumaye je alishapelekwa mahakamani au nani alishalalamika. je , Sitta kama alifanya makosa huko alikokuwa iweje kila mtu anamsifia isipokuwa wewe? Naweza kujua mwandishi bila kuwa na picha. Hata maneno yalivyopangiliwa yanaonyesha ni mtu wa aina gani wewe.
ReplyDelete. Maneno yako ni kama wale wanaolamba matako ya mafisadi.
huku kuwapa madaraka ya juu ktk chama watu ambao ni wapya katika chama kunakipeleka chama kubaya,ni sawa na kumwachia mtu ambaye ameokoka leo kufanya huduma ya Mungu ilihali hata taratibu za kanisa hazijui. CCM kuweni makini na hao mliowapa madaraka kwa kuwaridhisha kesho wataondoka na kuwa wapinzani tena ndipo mtakapo kuwa mmejiponzaaa......
ReplyDeleteKiongozi mwenye busara na hekima ya uongozi siku zote hukubali kukosolewa na hapo ndipo anpojua kasoro yake katika uongozi iko wapi sio kuwa na watu ambao uwezo wao wakufiki ni mdogo badala ya kusikiza maoni ya wananchi waliomchaguwa wanasemaje na wanamatatizo gani yeye anaanza kukimbilia kwa vyama vya upinzani kudai yakuwa wanahamasisha vurugu.
ReplyDeleteHii ni pamoja na msajili wa vyama yeye inonekana kaegemea upande mmoja wa chama tawala ambacho viongozi wake hawataki kukosolewa,Hawa ni viongozi ambao wamelewa madaraka ni siku zote wanafikiri wao ndio wanaostahili kukaa madarakani mpaka siku watakayo kufa.Chama kimoja bila ya upinzani hakiwezi kuleta maendeleo hata siku moja,Kwani kunatabia ya viongozi wengine wachache ambao hujisahau na kuona kama wao ni miungu watu.Unapo kosolewa kama kweli wewe una akili na busara unatakiwa kukaa chini na kufikiria juu ya yanayosemwa na wananchi wako pamoja na vyama vya upinzani.Sio kukimbilia kusema vyombo vya dola vipige marufuku maandamano na nyie viongozi mfanye mambo jinsi mnavyotaka wenyewe na wananchi wafunge midomo yao kwa mabaya mnayo fanya.Halafu mnasema watanzania ni wazuri sana maana kila utakachofanya wao wapo kimya tu.Hii nchi ina amani sana.
Lakini ukweli wa mambo ni kwamba nyie viongozi mlio madarakani ndio vinara wa kupeperusha amani Tanzania.
WaTanzania tunadanyika kirahisi, CCM na CDM ni wale wale. Viongozi wale wale au watoto wao. Hivi jamani hatuoni ni kama kamchezo fulani hawa wanasiasa wanakacheza!!? Je inakuwaje hatuongelei viongozi wapya, damu mpya ambao wanajitegemea bila kuwa chini ya chama fulani? Tuchague viongozi kufuatana na uwezo wao?
ReplyDeleteWewe Sumaye unayoyasema sidhani kama yanatoka moyoni mwako maana balaa lote analolipata Kikwete sasa ni madudu ya uongozi wako wewe na mkapa,mmeuza bandari,madini,rada,epa,ndege ya rais,mashirika ya umma yote.mabenki na mengineyo,mmeuziana Kiwira,mkabinafsisha reli,na mengi mno. sasa wewe kama kada wa ccm msaidie Rais kujenga hoja za kuvunja yanayosemwa na Chadema ni kwa nini mlifanya haya na kikwete anatakiwa kuwafikisha mahakamani lakini anashindwa kutokana na sababu mbalimbali za kichama. Huyo tambwe ni oportutunist tu wapo hapo kwa ajili ya ulaji tu.Nani kasema Sumaye si Fisadi? ujanja ujanja tu wanasiasa kutafuta kinga za baadaye. Sumaye una mambo ya kuwajibu vizazi vyetu vya baadaye.
ReplyDeleteJAMANI MIMI NI MWANA CCM,NA CHAMA CHETU KINAVURUGWA NA WATU WACHACHE SANA WENYE FITNA NA UBABAISHAJI NAO NI MAKAMBA NA TAMBWE
ReplyDeleteTatizo la CCM ni kuwapa madaraka makubwa watu wasio na uwezo wa kufikiri. I-Q yao ni ndogo sana. Makamba na Tambwe wote ni wagosi ni kwamba wamepeana namna ya kula Chama chetu. Tambwe amepata wapi upendo na CCM? Yeye hatujasahau alikuwa CUF damu damu. Makamba ndiye alimvutia CCM ili ale.
ReplyDeletewote mlotoa maoni ni wajinga ndio mliwao. Siasa kimbilio la wezi siku hizi,Nyerere alipokufa walilia unafiki tu,huoni wengine wanakwenda kwenye kaburi lake na waandishi wao na baadaye kuandika habari tofauti za uongo.kulia kwao ilikuwa ni furaha kuona nuksi kaondoka sasa ndio wakati wao wa kujitanua.Nachukia siasa na wanasiasa
ReplyDeletevichwa vya hao kina Tambwe na Mkamba hawana lolote vichwani mwao akili zao tayari zilishaganda; hivi unategemea CCM wanayo akili ya kujiongeza kurekebisha kero? akili zao tayari zilishaganda wanatakiwa kupumzika nanyie Sitta na Mwakyembe si muhame humo kabla akili zenu hazijaganda
ReplyDeletePropoganda daima ni kusema uongo hata ambayo hayapo. Tambwe hana hadhi ya kukaa ndani ya CCM cha mhimu aondoke akae nje pamoja na Makamba maana wote hao wanazidi kuvuruga chama tu.
ReplyDeleteHivi hizi comments wanaziona hawa ssssmmmm
ReplyDeleteKazi kweli kweli