LONDON, Uingereza
MATUMAINI ya Kolo Toure, kuweza kukwepa adhabu ya kufungiwa kucheza soka kutokana na kutumia dawa za kulevya yamefifia, baada ya
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu(FIFA), Jerome Valcke kusema kuwa kutojua hakukubaliki kama sababu ya kukutwa ametumia dawa hizo.
Mlinzi huyo Manchester City, anaonekana kukosa muda kulifahamisha Shirikisho la Soka la Uingereza, kama anataka kipimo kingine kuchunguzwa baada ya kupimwa awali na kuonekana ametumia dawa.
Toure anaamini kuwa chembe za dawa alizokutwa nazo kwenye damu yake ilitokana na dawa za mkewe ambazo alichukua na kumeza ili kutibu tatizo lake la kuongezeka uzito, lakini Valcke amsisistiza kuwa kabla ya kumeza dawa hizo Toure, alipaswa kuwauliza madakari wa klabu kuhusu athari zake.
Alisema: "Wakati unajua utakuwa kwenye hatari ya dawa zinazokatazwa, kuna madakari wa kutosha katika timu kuhakikisha unawauliza na kukagua vidonge ulivyo navyo.
No comments:
Post a Comment