08 March 2011

Magufuli aibeza CHADEMA

Na Mwandishi Wetu, Kagera

WAZIRI wa Ujenzi, Bw. John Magufuli amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuacha kutoa matusi katika mikutano yake hatua
iliyomfanya kuwaombea dua ya ‘washindwe na walegee katika jila la Yesu’.

Kauli hiyo aliitoa juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Chato ambao uliandaliwa kwa ajili ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye yuko katika siku ya nne ya ziara ya kikazi mkoani Kagera.

“Tulipata ugeni katika wilaya yetu ya Chato lakini wakubwa wao hawakuja, hakuna cha msingi walichosema bali matusi tu. Mimi nasema washindwe, washindwe na walegee katika jina laYesu,” alisema huku akishangiliwa.

Alisema Watanzania wanachotaka ni kuona wanatatuliwa matatizo yanayowakabili na hasa changamoto za barabara, walimu, maji na siyo kusikia matusi katika majukwaa. “Watanzania wa Chato na Watanzania wote nchi nzima hawadanganyiki, wametoa ridhaa yao kwa miaka mingine mitano, kwa hiyo ni waelewa. Tuna kazi ya kuzitimiza changamoto zinazowakabili Watanzania, tuacheni tufanye kazi waliyotutuma,” alisema.

Akifafanua zaidi, alisema: “Viongozi wa CHADEMA wanapiga kelele na hawatoi njia mbadala ya kutatua matatizo tuliyonayo... wananchi hawataki kusikia matusi bali wanataka kuona suluhisho la matatizo yanayowakabili.”

Aliwataka Watanzania kuwadharau na kuwapuuza kwa sababu hawana jipya huku akisema kuwa: “Tuwaache watupige mawe kwani hata mwembe wenye matunda mazuri ndiyo unaopondwa mawe na watoto. Kwa hiyo nao acha watupige mawe sababu matunda yetu ni mazuri,” alisema.
        

16 comments:

  1. Magufuli, maombi kwa kutumia Jina la Yesu, hayakubaliki. Ninaomba usiisome Biblia kwa kuigeuza. Kumbuka mara zote Mungu hugeuza maombi ya kumtakia mabaya mtu mwenye nia safi, kuwa baraka. CCM iliyokwishashindwa kuwaletea watu wa Mungu maisha bora na badala yake imewaneemesha mafisadi kama wewe Magufuli kupitia mikataba mibovu, uwaziri na ubunge, ndiyo itakayoshindwa na kulegea. Na hapa mimi sisemi kwa Jina la Yesu kwani kulitaja Jina la Bwana bure ni kuvunja amri zake. Ukiwa mkristo uliyebatizwa na kuitwa John,je unaikumbuka amri hiyo? Au ndiyo unaiabudu CCM na Kikwete ili azidi kukupa madaraka? TAFAKARI!!!

    ReplyDelete
  2. Kutoa maoni ni uhuru wa kila mtu,na kuabudu pia ni uhuru wa kila mtu,huwezi kumzuia mtu eti asitaje jina la yesu ikiwa yeye Imani yake kwanini asiwaapize kwa nguvu zake?kwani chadumaa walikwenda kutoa lugha za kasfa pale chato na yeye ndio mbunge wa pale unategemea nini lazima atajwe Bwana,hv wewe unajidai Mkristo tegemeo lako ninini?John anamtegemea Yesu na ndio alimuwezesha akaweza kusoma na kumaliza shahada zake kwa afya njema na leo anapata hata hivyo vyeo kwa nguvu zake YESU na sio CCM!!!

    ReplyDelete
  3. chadema ukweli ulivyo hamna muelekeo mzuri ndani ya nchi yetu sababu kila mtu akisema kitu mna kipinga sasa nyie tuambieni mnachokitaka hasa na kiwena ahueni kwenu ni nn? mwisho wenu sasa unahesabika hatutokubali nchi ichafuke huku tunawaangalia jueni hilo wa kwanza kuwa mkaa ni nyie

    ReplyDelete
  4. Magufuli sasa naona unaanza kuota mapembe tunakuomba uache mara moja tabia ya kuikashfu CHEDEMA!!!!!!!!!Wananchi tunakuona unfaa kuwa kwenye serikali ya chadema 2015 halafu unaleta za kujua. sasa twambie pinda alivyokuja ametatua nini kero za wananchi kama si ziara ya million hamsiuni kwa kufungua shule ya million kumi.

    ReplyDelete
  5. “Viongozi wa CHADEMA wanapiga kelele na hawatoi njia mbadala ya kutatua matatizo tuliyonayo...

    Umefikiria kabla hujatoa hii statement au umechemka Dr. Magufuli?!
    CDM wanasema hivi
    JK na serikali yake awachukulie hatua mafisadi wote waliotuingiza kwenye mkataba wa DOWNS/RICHMONDs, EPA, Meremeta, Kiwira,Kagoda,
    JK na serikali yake awachukulie hatua wale wote waliosababisha uzembe wa milipuko ya mabomu ya Gongo la Mboto (notorious offender it happened in Mbagala)
    JK na serikali yake apunguze baraza la mawaziri ili kubana matumizi ya serikali.
    JK na serikali yake apunguze posho za mawaziri na makatibu wakuu na wakurungezi ili fedha hizo ziweze kuwalipa mishahara mizuri watumishi wa serikali iliyopendekezwa na TUCTA
    JK na serikali yake atekeleze angalau nusu ya ahadi zake alizozitoa kwenye kampaini eg Kujenga reli ya umeme DSM to MZA/KGM, Kuifanya Kigoma kuwa Dubai ya TZ, Hospitali zote za mikoa kuwa za rufaa, Kununua meli kubwa ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa,
    Maisha bora kwa kila Mtanzania
    JK na anunue bajaji 400 za kubeba akina mama wajawazito (SIC)

    Bado tu unaamini CDM hawatoe njia mbadala

    ReplyDelete
  6. Makufuli, usilitaje bure jina Mungu maana Mungu atakuhesabia hatia unapofanya hivyo. Acha kujitafutia umashuhuri kupitia jina la Yesu. Ndani ya sisiemu hakuna Yesu, huyo yesu unayemtaja kuwalegeza CHADEMA ni mwingine ambaye hana nguvu, na siye yule aliyekuja ili wanyonge wapone na hata kuamua kutoa uhai wake kwa ajili ya walionyanyaswa. Nakushauri utubu kwa Mungu kwa kulitaja jina la Yesu pasipostahili

    ReplyDelete
  7. Mh. Dr. Magufuli naheshimu sana mawazo yako ila hili la kufanya mzaha na jina la Yesu halikubaliki! tafadhali naomba uombe msamaha.

    ReplyDelete
  8. Namheshimu Dr Magufuli kwani angalau aliisotea shahada yake ya PhD kulinganisha na wenzake akina JK. Na wakati mwingine hujikakamua kusimamia sheria japo pengine nachakachua kama walivyo baadhi ya wanasiasa wa CCM. Ila kwa Habari ya kutaka wa CHADEMA walegee ..... simuheshimu hata kidogo! Nina imani aliposema maneno yaliyonukuliwa hapa, alitaka kumfurahisha Pinda na wananchi wengine wa Chato. Ajaribu kufikiria zaidi anapotumia maneno kama haya.

    ReplyDelete
  9. Mh. Dr.Maghufuli umepotoka, kumbe na wewe mnafiki? Tafadhali usipoteze imani yangu kwako. Kwan kati ya viongozi wa Serikali ya CCM nilio na imani nao, mmojawapo ni wewe. Omba toba kwa kusema uongo na kutumia jina la Yesu bure.

    ReplyDelete
  10. pumba-vu kweli namna hihi unaanza kuiangusha nchi kama rai-si, kwa taarifa watanzania walikuwa wameanza kukutegemea kuwa wewe ni mzalendo wa nchi hii na 2015 hata kiti cha uraisi kinakusubili wewe kumbe busara zako zinaanza kuwa ndogo kwa matusi uliyotoa dhidi ya chadema hata mazuri yao hujaona hata moja!!! kumbe bio za sakafuni.... turudishie imani yetu kwako la sivyo hatujaona mwaminifu nchi hii wa kukomboa watawaliwa.

    ReplyDelete
  11. Dr Magufuli umeona ubaya wa Chadema sasa nakuomba Dr. ona ubaya pia wa CCM na uyaseme. Acha kuwa mnafki mbona huwasemi akina Rostam, Lowasa, Chenge, Karamagi na wengine waliotufikisha hapa tulipo? Rostam kwan,ini awe Rais kwa kivuri cha JK. Rostam akisema hiki ccm na serikali yake lazima ifuata ama kweli huyu jamaa ameiweka nchi mfukoni mwake. hebu anza na huyu kabla kuondoa kama wale walala hoi mnaowabomolea nyumba zao usiku.
    acha ujinga.

    ReplyDelete
  12. Infwakti ni kwamba ukishajijua u mwenye dhambi, basi usiogope kutenda nyingine kwa kuwa jehanamu hakuna vifungo kulingana na idadi au ukubwa wa dhambi. So Magufuli kip it up, nena na tenda utakavyo, kwa jina lolote litajwalo chini ya jua. Tunachoitaji nchi hii kwa sasa ni mkusanyiko wa kero nyingi kwa kiasi ambacho kitawezesha akili za wale waliolala kuamka. According to me: A civil unrest is a result of accumulation of nuisance, little by little, that eventually leads to an avalanche of discontent, the result of which topples the order of leadership that created it

    ReplyDelete
  13. Kwa jina la Bwana na nkwa jina la Bwana,mlibariki Slaa kuchukua mke wa mlalahoi badala ya kumkemea ati ni mambo binafsi ati leo mnashambulia magufuli. Mnabariki dhambi ya kukufuru,Slaa kaliasi kanisa na miongozo ya Bwana yesu badala ya kumkemea mnasema mambo binafsi. Kwa Mungu baba kuna hilo. Dhambi ya Magufuli inafanana na ya Slaa kupora mke wa mlalahoi. Msimtaje Yesu kwenye maslahi yenu mnayoyapenda.Bwana awashukie na kuwaadhibu nyie mnaotetea dhambi

    ReplyDelete
  14. DAKTARI WA FALSAFA BWANA JOHN POMBE MAGUFULI, ni hivi tumia udaktari wako na falsafa yako kusoma alama za nyakati. Ukitaka kuporomoka anza vita na CHADEMA, HAKIKA TUATAKUSAHAU KATIKA SIASA. WATU KWA SASATUMECHOSHWA NA CCM, HATA KAMA MWANACCM ATAGOMBEA NA JIWE, JIWE LITASHINDA!

    ReplyDelete
  15. Mbona hamkushinda uchaguzi mliopita? viti vingapi mnavyo? hatuwapi kura wezi wageni mnaweza kuleta maafa makubwa. nyie mmezungukwa na wezi tu wanaoitaka ikulu. nani atampa mchaga ikulu uliwahi kuona katika historia ya nchi yetu,hao walioko madarakani tu balaa,hebu angalia Mramba nafasi alizoshika na kuweka wachaga wenzie leo tukiwapa ikulu itakuwaje?

    ReplyDelete
  16. haya sasa naye huyu anajimaliza. tumsubiri mwakyembe naye

    ReplyDelete