*Mbunge atenga milioni 12/-kupeleka wapigakura
Na Glory Mhiliwa, Arusha
TIBA ya miujiza inayotolewa na Mchungaji Ambilikile Mwasapile sasa imegeuzwa kete ya wasiasa ambao wameendelea
kujitokeza kwa lengo la kutaka kuungwa mkono kwa kuwapeleka wapiga kura wao kunywa dawa hiyo inayodaiwa kutibu maradhi sugu.
Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Godbless Lema amekuwa mwanasiasa wa tatu kutangaza kuwasafirisha wananchi 200 kutoka kwenye jimbo lake kwenda Loliondo kunywa dawa.
Mbunge huyo aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa amefanya hivyo baada ya kupata taarifa sahihi kutoka kwa ndugu na marafiki waliokwenda kutibiwa kuwa wamepona.
"Nimetenga shilingi milioni 12 kwa ajili hiyo. Lengo langu ni kuwasaidia wenye maradhi mbalimbali jimboni kwangu watibiwe," alisema Lema.
Mbunge wa kwanza kujitolea msaada kama huo alikuwa Bw. phillemon Ndesamburo wa Moshi Mjini (CHADEMA) ambaye awali alitoa helkopta kusafirisha wagonjwa waliozidiwa wakisubiri dawa na baadaye kukodi magari kusafirisha wananchi kutoka Moshi kwenda Loliondo.
Jana gazeti hili liliripoti kuwa Mbunge wa Monduli na waziri mkuu wa zamani, Bw. Edward Lowassa naye amekondi magari kila kata kwenye jimbo lake kupeleka wananchi kunywa dawa hiyo.
Kila mwanasiasa anayejitokeza anasema ameamua kuwasaidia wanancbhi wake wenye matatizo ya maradhi hayo ili waweze kupata dawa hiyo ambayo imegeuka gumzo nchini.
Akifafanua zaidi sababu za msaada huo, Bw. Leama alisema pia maelezo ya Mchungaji Mwasapile kuwa ameoteshwa yamemsukuma, hivyo kuwataka watu wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali kufika ofisini kwake ili wapewe utaratibu na magari ya kwenda Loliondo.
"Nitakuwa sijawawatendea haki wananchi wa jimbo langu kama msaada wa uponyaji unapatikana katika mkoa wangu nikashindwa japo kuwasaidia. Ndio maana nimetenga fedha hizo kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wangu ambao hawana uwezo wa kenda huko," alisema.
Mbunge huyo alikwenda mbali zaidi, akiwasihi wafanyabiashara pamoja na wadau mbalimbali kujitokeza kusaidai watu mbalimbali ambao hawana uwezo ili waweze kunywa dawa na kupona magonjwa mbalimbali.
Kwa mujibu wa mbunge huyo kuna watu wengi wenye maradhi kama ya shinikizo la damu, kisukari ambao wanatamani kwenda kupata dawa hiyo kutoka kwa Mchungaji mwasapile lakini wameshindwak kutokana na gharama za usafiri kuwa kubwa.
Mwandishi wa hii habari acha kuandika habari za uchochezi.
ReplyDeleteInatakiwa utambue kuwa suala la kuisaidia jamii ni la lazima sio siasa.
Lema amekuwa msaada mkubwa kwa watu wa Arusha, ukiachana na suala la milioni 12, Lema ametumia zaidi ya milioni 100 kuisaidia jamii ya wanaarusha wasiojiweza, kuwasomesha watoto wao kuanzia mwanzo wa elimu mpaka mwisho wa elimu yao.
Usiandike habari kwa uchochezi wa kisiasa haipendezi.
Godbless Lema ni Kiongozi wa kuigwa hapa tanzania kutokana na kuwa mstari wa mbele kutetea haki ya wananchi wake.
ReplyDeleteAliteswa na polisi kwa ajili ya kudai haki ya wana Arusha.
Aliilalamikia milioni 90 zilizotolewa kwa wabunge kuwa ni nyingi, na matokeo yake tumeiona, kwani alipopokea tu, aliipeleka kwenye mfuko wa ardf kuwasaidia maskini.
kwanini usiandiketu ameamua kuwasaidia watu wajimbo lake mnarembaaaaa
ReplyDeleteacheni uchochezi/hatawewe mwandishi unapaswa uwapeleke nduguzakooo
Mhmmmm!!
ReplyDeletenachosema ni hivi!!!!!!!!!!!! waandishi mnapenda kukuza mambo, lema hajaaza jana wa leo kusaidia wananchi kwa hiyo kama kimewauma sana toeni msaada pia. acheni kufanya magazeti kuwa ya siasa
ReplyDelete