Zuhura Semkucha na Patrick Mabula, Shinyanga
MAHABUSU waliokuwa katika Kituo cha Polisi cha Kagongwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamewaua kwa kuwapiga risasi askari wawili
wa Jeshi la Polisi waliokuwa zamu katika kituo hicho.
Tukio hilo lilitokea juzi saa moja jioni kituoni hapo baada ya mahabusu hao kumuita askari mwenye namba F. 5344 PC Salimu kwa madai ya kuwa wanashida na baada ya kufungua mlango huo walimvuta ndani ya chumba hicho na kumunyang'anya silaha.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Bw. Justus Kamugisha alisema kuwa mara baada ya kumvuta na kumuingiza katika chumba cha mahabusu askari huyo walimfunika tisheti usoni na kumnyang’anya silaha aliyokuwa nayo anian ya SMG namba 14303612.
Alisema baada ya kumdhibiti askari huyo ndipo askari mwingine mwenye namba F. 4964 PC Ngwegwe alikwenda kutoa msaada naye akapigwa risasi sehemu za kifuani na kufariki hapo hapo.
Majambazi hao yaliwapora askari hao bastola aina ya Chinese yenye namba XR7526 aliyokuwa nayo kwa ajili ya kazi yake.
Kamanda huyo alisema kuwa muda mfupi baada ya tukio hilo polisi walifuatilia nyendo za watu hao kwa kushirikiana na wananchi na kumkamata mmoja Bw. Audax Buberwa ambaye aliuawa kwa kushambuliwa na wananchi.
Kutokana na tukio hilo wananchi walitoa ushirikiano kwa hilo na kuwakamata watuhumiwa tisa.
Aliwataja kuwa ni Bw. Kwizela Lionel (mtusi) , Goodluck Leonard, Bw. James Leonard (26), Bw. Suleiman Dossi, mkazi wa Mabagala Dar es Saalam, Bw. Simon Fredi mkazi wa Mwanza, Bw. Paulo John mkazi wa Kahama, Bw. Lilakozi Willy ambaye ni Mrundi Bw. John Peter mkazi wa Mwanza, Bw. Emanuel Jockson mkazi wa Bukombe.
Polisi shughulikieni matatizo za uhalifu nchini, msijiingiye kwenze siasa. Tunajua kunamatatizo mengi ndani ya jeshi yanazohitaji kushughulikiwa ili kuboresha utendaji. Siasa si jukwaa lenu...
ReplyDeleteAwali ya yote nampa pole kamanda Mwema kwa kupotelewa na nguvu kazi ya jeshi lake.
ReplyDeletePolisi angalieni jinsi mnavyopewa ushirikiano na wananchi wanaodai haki zao.
Angalieni jisni wanavyojitoa mhanga kuhakikisha wahalifu wanakamatwa. Lakini ni wananchi hao hao mnaowapiga risasi wakati wanadai uhuru wao, na ninyi mnajiingiza kwenye siasa.
nawapa pole sana wana familia waliofiwa na hao maaskari, ushauri wangu ni kwamba: askari wawe makini wakati wakiwa karibu na wafungwa kwani wengi wao ni majambazi sugu wanaojua kutumia sila, na hilo linaonekana lilisha andaliwa tangia siku nyingi lilikuwa likisubiria utekelezaji tu.
ReplyDeletepoleni sana kwa kuwapoteza mashuja wetu
Wala mimi sitoi pole....askari waliua ndugu zetu, acha nao wapate dozi yao
ReplyDelete