Na Suleiman Abeid, Shinyanga
ASKARI mmoja wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Shinyanga amejiua kwa risasi mbele ya ghala la kutunzia silaha mjini Shinyanga.Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Shinyanga, Bw. Diwani Athumani amemtaja askari aliyejiua kuwa ni G.4425 PC Selemani Lukuta aliyejipiga risasi juzi saa 12.00 jioni muda mfupi baada ya kukabidhiwa bunduki aina ya SMG na risasi 30 kwenda doria.
Kamanda Athumani alisema haijafahamika sababu ya polisi huyo kuchukua uamuzi huo kutokana na kutoonesha dalili zozote za kuwa na tatizo tangu awali.
Akifafanua, alisema siku hiyo ya tukio, askari huyo pamoja na wenzake walikwenda katika ghala la kutunzia silaha ambako baada ya kukaguliwa kama ilivyo kawaida hakuonekana kuwa na tatizo lolote na hivyo alikabidhiwa silaha pamoja na risasi zake na kisha walipewa maelekezo ya kazi kwa siku hiyo.
Baada ya kupewa maelekezo ya kazi kama ilivyo kawaida ya siku zote ghafla polisi huyo alielekeza silaha yake sehemu za shingoni na kujipiga risasi ambayo ilifumua kichwa chake na akafa papo hapo, haijafahamika sababu za kuchukua uamuzi huo, hivi sasa tunafanya uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo, alieleza Kamanda Athumani.
Kamanda huyo amekanusha uvumi ulioenea mjini hapa ukidai kuwa kujiua kwa askari huyo kunatokana na kupangwa zamu za kwenda doria mara mbili kwa siku hiyo, kitu ambacho kinadaiwa ndicho kilichomuudhi.
Haya madai siyo ya kweli, kupangwa zamu mara mbili ni utaratibu wetu wa kawaida, wapo watu wanashinda pale kituoni mchana, lakini jioni hupangiwa kuingia kazini kufanya doria za mitaani, hii siamini kama inaweza kuwa sababu ya yeye kuchukua maamuzi hayo mazito.
Hata wale wenzake aliokuwa amepangwa nao kwenye doria kwa hiyo juzi walikuwa pia na zamu nyingine nyakati za asubuhi, huyu ni moja wa vijana wetu walioingia jeshini mwaka jana, ana mwaka mmoja kazini ni wazi utaratibu huu haukuwa mgeni kwake, alieleza Kamanda Athumani.
Mwili wa marehemu ulitarajiwa kusafirishwa jana kupelekwa nyumbani kwao mkoani Tabora ambako leo anatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya mjini Tabora.
ila serekali yetu pamoja na wakuu wa mapolisi mnatakiw muwe makini sana kwani mtu hawezi tu kukurupuka na kujiua lazima kuna sababu nawapa pole wote waliofikwa na msiba huu mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi ijapo kajiua mwenyewe
ReplyDeletekama mtu ameamu akujiua,hapo serikali nayo ilaumiwe kwa lipi,cha msingi ni kujua kwa nini amejiua,sio kila kitu serikali serikali,hiyo serikali inajua hata mawazo ya watu jamani????tuache mambo ya kulalamika lalamika kila kitu
ReplyDeleteHuwezi kujua amejiua kwasababu gani. Lakini kwani kama na hao wengine walikuwa wanapangwa zamu kama yeye, kwani wanafanana kiakili na kisaikolojia? Jeshi la Polisi ni wanyanyasaji sana. Lazima mijfunze. Siku ingine atawafyatulia wakubwa zake, alafu mtakuwa na maelezo mazuri
ReplyDelete