03 February 2011

CUF yalia na CHADEMA

*Yashutumu kuwatenga katika Kambi Rasmi Bungeni
*Yadai CHADEMA na wabaya wao watakufa na kuiacha


Na Rabia Bakari

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimedai kuhujumiwa na Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutokana 'kauli za kichochezi' zinazotolewa dhidi yake kuhusu sababu za kukataa kushirikiana nao bungeni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Bw. Julius Mtatiro alisema kuwa licha ya kuhujumiwa na CHADEMA lakini pia wanasikitishwa na kauli zilizotolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa kwa kudai kuwa CUF sio chama cha upinzani nchini.

"Tunasikitishwa na kauli hiyo ya Dkt. Slaa na nikimnukuu anasema kuwa 'CUF siyo chama cha upinzani Tanzania tena, eti kwa sababu kiko serikalini Zanzibar' na kwa hiyo CHADEMA hawawezi kushirikiana na CUF katika kuunda kambi ya pamoja bungeni.

"CHADEMA wanaishambulia sana CUF hivi sasa, wanataka kuwaaminisha Watanzania kuwa kitendo cha CUF kuwa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ni dhambi kubwa mno na kuwa Watanzania wasiiunge mkono CUF Tanzania bara, jambo ambalo ni ndoto za alinacha na kamwe halitatokea kwani Watanzania wa sasa hawadanganywi kwa propaganda zisizo na maana,"aliongeza.

Kauli ya Bw. Mtatiro inatokana na Tamko la Kamati kuu ya CHADEMA lililotolewa na Dkt. Slaa, kuwa CC ya chama hicho imemuagiza Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, kuunda baraza kivuli kwa kuhusisha wabunge wa CHADEMA pekee.

Akitoa tamko hilo, Dkt. Slaa alisema: "Kamati Kuu imeendelea kuzingatia umuhimu wa vyama vya siasa kushirikiana katika kuimarisha nguvu ya upinzani hapa nchini. Hata hivyo, kamati kuu imezingatia kuwa Chama cha Wananchi (CUF) wamejiunga na CCM kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

"Na kwa kuwa sheria inayoruhusu uwepo wa vyama vya siasa inahusu pande zote za muungano na kwa kuwa vyama vingine vya upinzani vyenye wabunge vimo katika ushirikiano na CUF, Kamati Kuu imeona kuwa CHADEMA haiwezi kuwa na ushirikiano wenye tija na vyama hivyo.

"Sasa kwa mfano tukiazimia kitu kinachopingana na serikali, Katibu Mkuu wa CUF ambaye ndiye Makamu wa kwanza wa Rais huko Zanzibar unategemea atakubaliana nacho ili apingane na serikali, hivi vyama vingine navyo tayari vimeshakuwa sehemu ya watawala maana wameamua kushirikiana na CUF katika kamati yao," alisema Dkt. Slaa.

Akizungumzia maazimio hayo, Bw. Mtatiro alisema kuwa CUF haiwezi kuwalamba miguu viongozi wa CHADEMA kwani hakuna faida yoyote wala umuhimu ambao wao wameonesha tangu walipojaribu kila namna kuwafanya wafanye kazi kwa umoja na vyama vingine na kugonga ukuta.

"Mara zote CHADEMA wamekuwa na historia ya kuvisaliti vyama vingine vya upinzani huku wakikimbilia kwa umma kuomba waungwe mkono wao peke yao," alidai.

Aliongeza kuwa CHADEMA kina matatizo mengi sana tangu mwaka 2007, na waliwavumilia kwa kiasi kikubwa na hata baada ya uchaguzi mkuu kuisha mwaka jana, CUF iliiomba CHADEMA iweze kushirikiana na vyama vingine vya upinzani ili kuwa na kambi ya upinzani imara zaidi na yenye nguvu.

"CHADEMA walikataa kabisa suala hili kwa maelezo kuwa “wao wako tayari kuungana na CUF tu katika kambi ya upinzani na kuwa hawaviamini vyama vya NCCR, TLP na UDP, na tulijaribu kuwasihi lakini hawakutaka kubadili msimamo huo.

"Lakini baada ya yote hayo, jana (juzi) CHADEMA wametoa kauli ya kinafiki,  eti wao hawawezi kushirikiana na chama kinachoongoza dola, yaani CUF na kuwa wao CHADEMA wako tayari kushirikiana na NCCR-Mageuzi," aliongeza.

Bw. Mtatiro alisema kuwa hivi karibuni NCCR ndio walikuwa kikwazo kwa CHADEMA kushirikiana na vyama vingine, hata mwezi haujapita wamegeuka na kudai CUF ndiyo adui.

"CHADEMA ni chama popo sana, hawajui wanachofanya, wamelewa madaraka na kuchanganyikiwa vibaya baada ya kupata majimbo 20 Tanganyika, sasa hawana haja na CUF na vyama vingine, wanadhani majimbo 20 ndio Ukombozi wa Tanzania umemalizika.

“Ni sawasawa na maskini sana anayeamka ghafla anajikuta tajiri, hajui namna gani atatumia utajiri wake, anaanza kuwatukana majirani zake alioishi nao kwa shida na raha katika umaskini wao, anawatukana majirani huku anaendelea kuponda mali na wasichana warembo katika kijiji hichohicho, siku moja mali zinaisha……hadithi ya tajiri mjinga inaishia hapo," aliongeza Bw. Mtatiro kwa jazba.

Aliendelea kukishutumu chama hicho kuwa kinafanya kusudi kutoa kauli za kichochezi, wakiamini kuwa CUF ikifa bara wao watapumua mno.

Alisema ni wazi CHADEMA wanaiogopa CUF, huku wakifahamu fika kuwa chama hicho kina mtandao mkubwa na kina mbinu ya kujiimarisha bara na hatimaye kuongoza nchi.

Bw. Mtatiro alidai kuwa kitendo cha CHADEMA kuwadharau Wazanzibari, kudharau maamuzi ya wananchi wa Zanzibar katika nchi yao, kudharau katiba ya Zanzibar ni kitendo cha kijinga mno.

"Wazanzibar ndio walioamua kwa kupiga kura kuwa wanahitaji serikali yao, ya umoja wa kitaifa kwa maslahi ya nchi yao ya Zanzibar kwa kujali amani maendeleo na ustawi wa taifa lao.

"Wazanzibari ndio walioamua kuwa chama kitakachoongoza katika uchaguzi kitatoa rais na mawaziri na cha pili kitatoa pia makamu wa kwanza wa rais na mawaziri. Wakapiga kura, wakatoa maamuzi haya, wakayaingiza katika katiba yao ya Zanzibar katika mabadiliko ya 10 ya katiba," aliongeza.

Alisema ni ujinga kudai CUF kuwa katika mfumo wa serikali iliyoamuliwa na wananchi katika upande mmoja wa nchi ni dhambi.
  
Alihoji kuwa, CUF ilipopata nafasi ya pili Zanzibar CHADEMA walitaka ikiuke matakwa ya wananchi na kukataa kuingia serikalini ili iwafurahishe CHADEMA ambao Zanzibar hawana hata mjumbe wa mtaa wala tawi?

"Nani asiyejua kuwa CUF ni chama chenye nguvu na mtandao Zanzibar na Tanganyika na ni chama cha pekee cha upinzani chenye wabunge kutoka pande zote za muungano? Nani asiyejua kuwa CHADEMA ni chama kilichoko Tanganyika peke yake?

"Nani asiyejua kuwa CHADEMA kinaumizwa sana na mafanikio na utulivu wa kisiasa Zanzibar yaliyochangiwa kwa kiasi kikubwa na busara na viongozi wa CUF ambao hawakuweka maslahi ya chama mbele katika kulinda uhai na maisha ya Wazanzibar?" alihoji.

Bw. Mtatiro aliyewania ubunge katika Jimbo la Ubungo na kushindwa na Bw. John Mnyika wa CHADEMA, alidai kuwa CUF kama chama chenye nguvu kubwa Zanzibar watazidi kuheshimu maamuzi ya wananchi walio wengi kila mara bila kujali kama CHADEMA watakasirika au la.

Aliongeza kuwa chama kipi ili kuwatumikia Watanzania, kuwatetea katika madhila yote na manyanyaso wanayofanyiwa.

"Tutaendelea kuwa katika SUK na kulinda maamuzi na matakwa ya wananchi wa Zanzibar lakini kwa upande wa Tanzania bara ambako katiba iko wazi, kuna chama kimoja kinachoongoza dola na vingine vyote vikiwa vyama vya upinzani, tutaendelea kuheshimu matakwa ya kikatiba yaliyopo Tanzania bara," alisema.

Aliwataka CHADEMA wafahamu kuwa CUF kitazidi kuwa chama cha kitaifa kwa kuzidi kupata wabunge wengi kutoka Bara na Zanzibar, kujiimarisha pande zote za nchi hadi waione njema inayosubiriwa na Watanzania wote.

Bw. Mtatiro aliongeza: "CHADEMA na watu wote wanaoitakia mabaya CUF watakufa na kukiacha chama hiki kikishamiri kama tegemeo la pekee la Watanzania," alisema.

43 comments:

  1. Duh, Mtatiro, siasa huiwezi kabisa! Hebu tupe busara ya kumwita katibu mkuu wa CUF Maalim Seif ni kiongozi wa upinzani. Anampinga nani?

    ReplyDelete
  2. eng. Mwakapango,E.PAFebruary 3, 2011 at 10:02 AM

    Ndungu yangu Julius Mtatiro unajua kweli unachokiongea? Infact tungekutana na mimi kabla hujafanya decision ya kujiunga na CUF nisingekushauri ujiunge na chama hicho. sasa ukiongea huwa atuelewi unaongelea nini? mambo ya pemba, unguja au zanzbar? CUF haina mtandao wa kutosha isipokuwa ina mtandao wa kipemba zaidi kuliko utaifa! na usijaribu kabisa kuilinganisha CHADEMA na CUF kwani hata kwetu sisi tuliopembeni tunaona kabisa kuwa CHADEMA ina watu makini, waliojiandaa kuchukua dola na si kwa ushindi wa mezani kama CUF mnavyoota. hebu angalia bunge lililopita mchango wa CUF na CHADEMA mbali kabisa CUF inawabunge wengi wa pemba ambao hawana interest ya kuongelea mabo ya bara na kwanza hawana muda huo! hebu kwa hesabu za haraka haraka CUF imekuwa ikipata ruzuku nzuritu lakini imeshindwa kutengeneza mtandao wa kutosha bara, toka historia ya mfumo wa vyama vingi inaanza haijawahi kupata mbunge zaidi ya mmoja bara ambako kuna wabunge wengi. itakumbukwa CUF mliposusia uchaguzi mwaka 2000 mlishindwa kushawishi watu hata wapigie vyama vya upinzani kula na wakapigia maruhani leo mnataka nini tena? politica carrier aliyopewa Maalim Sefu sharrif ni kielelezo tosha kwamba hamko mbali na serikali ya chama cha mapinduzi, leo sefu haishi kwenda ikulu ya DaresSalaam CHADEMA watapangaje naye mikakati ya kukiwajibisha chama hicho? open your eyes Julius tafuta chama progressive sio tu wabunge pemba! pemba! pemba! tunataka chama cha kitaifa na tunapozungumzia chama mbadala baada ya CCM ni CHADEMA hiyo hata Mrema Anajua. mnang'ang'ania baraza kivuli la nini jitangazeni na nyinyi kwa kuwatetea wananchi ili wawachague kwa wingi ili muongoze wapinzani bungeni. kuiombea CHADEMA isambatike ni sawa sawa na dua la fisi kuomba mkono wa binadamu udondoke. CHADEMA ni chama cha watanzania wote tofauti kabisa na ilivyokuwa NCCR MAGEUZI ambao wengi walifanya mchezo wa kuigiza kwa kumfuata Mrema huku nwakiwa si wapinzani wa kweli. TUACHIENI CHADEMA YETU IENDELEE KUWASUKUMA CCM WATUFANYIE KAZI NZURI. PEOPLES POWER!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Mamaa!!!!CUF yafa kwenda lala,mtatiro hoi elimu haijakusaidia rudi tena shule kama hujui CUF na CCM wamefunga ndoa basi huna mchango katika jamii,nilivyokuwa nakufahamu tukiwa chuo sivyo ulivyo labda umerogwa.Kwa taarifa yako CHADEMA ndio mkombozi wa watanzania muulize kikwete kwenye maadhimisho ya sheria akwambie Mbowe alivyong'ara na kushangiliwa na wanasheria,muulize naibu waziri mmoja wa serikali yenu alivyopata wakati mugumu kukitaja chama mpaka akatumia salamu ya CHADEMA kuwasalimu wasomi na kujibu hoja zao

    ReplyDelete
  4. Anachosema Mtatiro ni sahihi.CHADEMA wamekuwa wakibadilika katika kauli zao. Mara ya kwanza walisema tatizo halikuwa CUF bali vyama kama NCCR,UDP na NCCR_ Mageuzi ambavyo kwa mtazamo wao waliona si wapinzani wa kweli. Leo wameigeukia CUF, sasa tuwaelewe vipi? Mi kwa mtazamo wangu watatakiwa kushirikiana na vyama vyote vya upinzani vilivyo bungeni. Kama vitawasaliti, wananchi wataona na bado watakuwa na uwezo wa kufanya mabadiliko. Upinzani ukienda Bungeni kwa kugawanyika, CCM itapeta. "A house divided can not endure" Ni wakati wa kuweka masilahi ya nchi mbele kuliko ya vyama.Na watanzania tusiwaamini sana wanasiasa, wawe CHADEMA, CUF, NCCR, UDP n.k, wote ni wachoyo wa madaraka!hatuwezi kuwa na uhakika nani mkweli!

    ReplyDelete
  5. Ukweli kuhusu DOWANS: From the East African

    Powerful businessman and ruling party MP for Igunga in Tabora, Rostam Aziz, is to be a beneficiary in the Dowans Tanzania award.

    According to the proceedings from the International Court of Arbitration of the International Chamber of Commerce also known as the International Commercial Court (ICC), which recently awarded Dowans Holdings S.A. and Dowans Tanzania $65 million as compensation for breach of contract by the Tanzania Electric Supply Company (Tanesco), Mr Aziz was appointed Dowans’ attorney-in-fact as far back as 2005 “to manage the company’s affairs outside the Republic of Costa Rica.”

    According to the resolutions of the Dowans Holdings board of directors, two directors of the company, Bernal Zamora Arce and Noemy del Carmen Cespedes Palma, granted in the name and on behalf of the company, a power of attorney in favour of Mr Aziz.

    Powers granted to Mr Aziz include: “To transact, manage, carry on and do all and every business matters and things requisite and necessary or in any manner connected with or having reference to the business and affairs of the company and, for such purposes, to conduct all correspondences appertaining to such businesses and affairs.”

    The directors further granted Mr Aziz the power “to open and to close bank accounts... and to draw cheques on our accounts... and to sign all kinds of documents in connection with our accounts or money,” read part of the resolutions signed by the firm’s secretary, Mrs Palma.

    It goes further to give Mr Aziz, the immediate former CCM treasurer and shareholder in the short lived RVR Rail Consortium that brought together Kenya and Uganda railways, the power to “pay, settle, deduct and allow all taxes, rates, charges, deductions, expenses and all other payments and outgoings whatsoever due and payable or to become due and payable for or on account of any property, whether movable or immovable and whether in possession or in action, now or hereafter belonging to us or to which we may become entitled.”

    Mr Aziz has consistently denied having any links to the Richmond company that was involved in the scandal that saw former prime minister Edward Lowassa resign his post (see Box). Dowans is the successor company to Richmond.

    According to documents tabled in the arbitration proceedings, which The EastAfrican has seen, one Mr Gire, a cofounder of Richmond (REDVCO) who faces a court case in Tanzania over the same issue, is said to have told the ICC that the owner of the company is Mr Aziz.

    The ICC was told Mr Aziz was such a “powerful and influential” individual that some laws were amended in his favour. The Richmond scandal was the subject of a Parliamentary probe that led to the resignation of the Mr Lowassa.

    ReplyDelete
  6. Ukweli wa DOWANS unaendelea: 2

    According to the report of the proceedings, the ICC accepted the finding that Mr Aziz was so “powerful and influential” as to have diverted the contract to the claimant, Dowans, outside the Public Procurement Act.

    The contract went to favour “his friends and himself through the claimant and to have influenced the MEM (Ministry of Energy and Minerals) to force Tanesco’s Mr Hans Lottering to sign the POA (agreement for emergence power supply).”

    Mr Lottering testified before the ICC that he was told that “something would happen” to him if he did not sign the POA. He was formerly Tanesco’s general manager-transmission under Net Group Solutions of South Africa.

    The evidence presented before the Tribunal shows the involvement of Mr Aziz in getting the whole procurement out of the PPA and diverting the lucrative contract to a “business of him and his business friend” derived from the testimony of Henry Surtee.

    The Tribunal accepted the testimony of Mr Lottering that, “even using the international tendering (open tender method) which is the most inefficient and the longest method, if not interfered with, Tanesco would have procured the POA more efficiently and within a much shorter period than the period of 18 months that the Ministry of Energy and Minerals took to procure POA through the committee formed outside the law.”

    Last week, Minister for Energy and Minerals William Ngeleja named the owners of Dowans Tanzania as Dowans Holdings S.A and Portek Systems and Equipment PTE Ltd.

    ReplyDelete
  7. Ukweli wa DOWANS: 3; source; www.the eastafrican.co.ke (Jan 31)

    He named the directors of Dowans Tanzania as Tice (Canadian), Gopalakrishnan Balachandran (Indian) and Hon Sung Woo (Singapore). Others are Guy Arthur Picard (Canadian), Suleiman Mohammed Yahya Al Adawi (Oman) and Stanley Munai from Kenya.

    Under the country’s Company Ordinance Act, there is no restriction on owners’ citizenship or country of origin of a company.

    A firm can be registered in Tanzania even if its owners are 100 per cent foreigners.
    “The nature of owners is not a concern when opening a company in the country; it could be owned 100 per cent by foreign individual(s) or corporate firm(s),” Business Registration and Licensing Agency chief executive officer Esteriano Mahingila said.

    The CEO also confirmed that the Dowans files contained the same list of directors as mentioned by the minister of energy and minerals.

    “These files are public documents, whoever wants to peruse or even photographing them are allowed,” Mr Mahingila told The East African, “the file is here.”

    The government was yet to decide whether to pay the $65.8milion (about Tshs 94 billion) to the owners of Dowans Holdings SA and Dowans Tanzania.

    It is noted in the award ruling presented for registration at the high court that the practice regarding arbitrations is that an award has to be registered with the High Court for it to be a decree as if one issued by the High Court.

    However, if a party isn’t satisfied with an award, “there are two routes available either to apply to the Tanzanian court to remit the award to the arbitrators for reconsideration of certain issues or to apply to the high court to set aside the Award.

    “To apply to set aside an award, it must be that the Award was improperly obtained or that the arbitrators misconducted themselves,” reads part of the ruling by the ICC.

    ReplyDelete
  8. CAFU, mbona mnataka kuwa ndumila kuwili. badala ya kulia na CHADEMA, ninyi fuatilieni haki zenu CCM. Hamjui kuwa ninyi ni sehemu ya uongozi wa taifa tena mkiwa na umakamu wa rais. tatizo na kutoelewa nafasi yenu serikalini. badala ya CAFU kupigizana kelele na CHADEMA, mnapaswa kutumia nguvu hizo kuielewesha serikali kuwa nini ni viongozi na mna nafasi yenu tena ya umakamu wa rais hata bara kwani tanzania ni moja na rais ni wa jamhuri. kuingia upinzani mtasema nini kuhusu CCM+CAFU VISIWANI????

    ReplyDelete
  9. Ndoa ya CCM na CUF iko wazi Chadema wako sahihi acha wao CUF washirikiane na CCM wao ndio popo na mamluki wa CCM kwani umoja wa kitaifa ni wa vyama viwili tuuuuu?waaache kuyumba yumba CHADEMA msimamo mmoja tunataka Tanzania yenye uwazi na maendeleo

    ReplyDelete
  10. CUF, wanafiki tu! Kwani hawakumbuki kuwa mwaka 1995, waliunda kambi ya upinzani wao pekee yao, wakaicha nje NCCR ambayo ilikuwa na wabunge zaidi ya 20 bara, wakati wao walikuwa na mmoja tu bara?

    Isitoshe, hizo kanuni za bunge zinazotanbua kambi rasmi ya upinzani bungeni, si CUF hawa hawa walitunga na wakalazimisha neno kambi "rasmi" liingizwe kwenye kanuni ili wao wawe vinara wa upinzani! sasa sheria ni msumeno. huwezi badilisha kanuni au sheria ili kukidhi matakwa ya watu fulani. Leo wataomba kubadilisha kanuni za bunge kutambua kambi isiyo rasmi sijui ndogo, kesho wabunge wa ccm wasio mawaziri au wakuu wa mikoa nao watataka spika abadili kanuni ili nao waunde serikali ndogo isiyo rasmi bungeni! huu utakuwa ni uwendawazimu!

    ReplyDelete
  11. CUF si chama cha upinzani tena. Huo ni ukweli usiopingika. NCCR mageuzi ni vibaraka wa CCM pia. Kwahiyo Chadema ndicho chama pekee cha upinzani.

    ReplyDelete
  12. Tuangalie mstakabali wa nchi kwanza juu ya chama kinachoangalia watz na maisha yao na kutoa uozo ulipo serikalI YA CCM kama kuna hata siku moja CUF walifanya hivyo basi tutakiita chama cha upinzani na kama bado basi si chama cha upinzani hata kidogo,CHADEMA endeleeni na msimamo huo ili kuikomboa nchi na ufsadi uliopo ndani ya serikali(CCM&CUF)Pia vyama vingine ni mamluki wa ccm hakuna haja ya kuungana navyo.

    ReplyDelete
  13. Mimi ni yule yule Hafidh mwanaharakati na mpenda mageuzi kutoka Zanzibar.

    Nimesoma karibu comments zilizomo humu nyingi zikitoka kwa wana chadema lakini bahati mbaya sana mawazo yao karibuni wote ni Pumba tupu hamna hata mmoja aliechangia hoja za msingi.sasa naamini kweli chadema ni vifuu na hata ukimuona mtu anambiwa eti ana PHD ni kiongozi kutoka Chadema pia nae anaongea Pumba.
    Mimi nataka niwaulize tu kwa maelezo yenu mliotoa - wengi mnasema kua CUF si chama cha upinzani na hakiwezi kuhoji eti kwa sababu kipo ndani ya serikali! hizi ni pumba . chukueni mfano wa jirani zetu Kenya Serikali iliopo madarakani ni ya kujumuisha vyama zaidi ya viwili, mbona waziri mkuu Raila Odinga anahoji kule na kuna wakati mwengine anapingana na Rais wake? ndugu zangu hii haitaki hata elimu ya Chuo kikuu kutafakari suala hili. kwa hiyo kua na serikali ya pamoja bado unaweza kuhoji ikiwa upande mmoja utakwenda kinyume.
    Pili Chadema mwanzo mlikubali mjiunge na CUF lakini kwa masharti ya vyama vengine viachwe na hasa hasa NCCR lakini badae mnasema CUF haiwezekani imo ndani ya serikali !! sasa na hawa wengine jee pia wamo ndani ya Serikali ?!! kweli wanachadema mnaburazana kama watoto wa Bata. akielekea wa mwanzo nyote mnafata hata kama anaenda ktk shimo. Jengeni hoja msifate mkumbo tuu Chadema bado haijaifikia CUF kwa kuweza kutoa wabunge Zanzibar na Tanganyika.

    ReplyDelete
  14. chadema hawajawahi kusema wataungana na cuf hata siku moja we mzanzibari kaa kimya maana cjawai kusikia maalimu seif yuko Mbeya anahamasisha watu wajiunge na cuf jiulize kwa nini ? Chadema hakuna kuungana na cuf kuunda upinzani kwa kuwa cuf ni serikali.wananchi wakiamua masuala ya kijinga tuwaunge mkono tu hata kama sheria zinakataa? hilo watu wa bara hatuwezi kukubali neno kambi rasmi bungeni aliunda hamad rashid kwa kujua cuf itaendalea kuwa chama pekee cha upinzani mambo yamebadilika chadema uchaguzi ujao inachukua dola kwa maana ya rais

    ReplyDelete
  15. Wewe Hafidh unaufahamu vizuri uongozi wa Mwai na Raila ukoje? Usiulinganishe na CUF na CCM. CUF na CCM ni kwa Zanzibar tu na si nchi nzima wakati wa Kenya ni uongozi kwa nchi nzima. Uko makini kweli? CHADEMA ishirikiane na CUF ili iwe´je? CUF waendelee na ndoa yao na CCM, mbona wanatka ndoa na watu wawili?

    ReplyDelete
  16. Siamini kama haya yanatoka kwa kiongozi wa CUF. "wanataka kuwaaminisha Watanzania kuwa kitendo cha CUF kuwa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ni dhambi kubwa mno na kuwa Watanzania wasiiunge mkono CUF Tanzania bara"

    Nani kasema umoja wa kitaifa ni dhambi?

    Umoja wa kitaifa Zanzibar ni ndoa yenu CUF na CCM. Sisi hatusemi ni dhambi, ila inawaondolea CUF sifa ya kuwa chama cha upinzani.

    Au kutokuwa kwenye upinzani ni dhambi?

    Kama mnalilia upinzani rasmi bungeni, KUBALIANENI NA CCM tena, kikwete aachie ngazi ili CHADEMA waunde serikali halafu CCM na CUF muwe kwenye KAMBI RASMI bungeni.

    ReplyDelete
  17. Huyu aliesema comment zinazounga mkono CDM ni pumba hana lolote sasa kaeleza nini kinachoeleweka hapo ni huo upupuwake anafichaficha hapo juu, ataona aibu mwenyewe. Sisi tunasema nyinyi CUF mkapige rangi huko CCM kama kibarua sisi hatumo. Nyinyi mkafajilie mafisadi sisi tutaendelea kuwa kosoa na serikali yenu.


    Sisi tunashangaa matusi yote ya nini kama kweli nyinyi na wapinzani kweli. Na nyinyi mmeshaanza kubwabwaja kama M/KITI wenu Makamba. Tunajua Rashidi kakosa kuteuliwa uwaziri sasa mashambulizi yake anakuja kuyaficha CDM. Kuwa na subira utateuliwa kesho usiwe na wasiwasi. CDM haitaki watu wanafiki. Kuhusu Vyama vingine kama NCCR TLP na UDP na hawa lazima tuwaangalie mwenendo wao.


    Mmesahau ya kuwa mlikalia vile viti vya cdm wakati CDM walipotoka nje na kuwazomea sasa imekula kwenu. Kwani kipindi hicho mlikuwa upinzani au mlikuwa upande gani? Labda mtufafanulie watanzania tuwaelewe vizuri zaidi.Sasa mbaki kama mlivyokuwa hatutaki chochoko zenu zisizo na msimamo.

    ANGALIZO KWA CDM: Muwe makini na hawa wajamaa wakipata mpenya watawasambaratisha na hawa wametumwa kusambaratisha sio siri. Wanaonyesha wana siri kali sana hawa hakuna kuwapa nafasi. Wao wakiona haja BUNGENI ambayo inawafaa kuunga mkono waunge mkono kama wakiona haiwafai basi ni uhuru wao kama mwanzo kwa sababu hawaeleweki.

    ReplyDelete
  18. nyie wanachama wa CHADEMA wote ni wapumbavu msiokua na akili hata kidogo, badala ya kuchangia mada kwa kuangalia maslahi ya nchi, nyie mnaangalia maslahi ya CHAGGA DEVELOPMENT MANIFESTO(CHADEMA, Ni nani asiejua sababu kubwa ya CHADEMA kutoungana na CUF-(chama cha wananchi)ni chuki ya viongozi wa CHADEMA kwa dini ya kiislaam na ZANZIBAR, Viongozi na wanachama wengi wa CHADEMA wanaumia sana wanapoona ZANZIBAR sasa ina amani na maendeleo yananukia!!Roho zao zinataka kupasuka kwa chuki, FURAHA YAO ILIKUA NI KUONA ZANZIBAR IWE KWENYE MACHAFUKO MIAKA YOTE NA HATIMAE IWE SOMALIA NO.2 AFRIKA!! ubaya wa CUF na CCM kuunda serikali ya pamoja kwa maslahi ya ZANZIBAR na WAZANZIBAR Uko wapi? mbona CHADEMA ndio mlikua mstari wa mbele kutaka mpasuko wa kisiasa umalizwe ZANZIBAR? kumbe ulikua ni unaafiki!!! Kwa taarifa yenu, CUF ndicho chama pekee chenye sura ya KITAIFA TANZANIA, ina wabunge BARA, UNGUJA, NA PEMBA, .CCM, ina BARA na UNGUJA CHAGGA DEV MANIFESTO Ina BARA(KILIMANJARO NA ARUSHA)!!! Tumieni akili wakati wa kuchangia MADA WAPUUZI WAKUBWA NYIE!!!!

    ReplyDelete
  19. C.U.F kweli ni chama cha wananchi!!!! BARA, UNGUJA na PEMBA, CCM ni BARA na UNGIJA, CDM ni BARA(MOSHI na ARUSHA)

    ReplyDelete
  20. CUF inakua na mtandao nchi nzima kwa kuwa ni chama chenye muelekeo wa UISLAAM!! acheni kutubabaisha!! CHADEMA ndicho chama chenye nguvu TANZANIA, hata C.C.M wanajua!! peoples power!!

    ReplyDelete
  21. MIMI ninasema CHADEMA ni marufuku kuungana na wajaahidina wanaovaa kanzu BUNGENI,CUF waondoke wakavalie KANZU zao kwenye BARAZA LA WAWAKILISHI!! Wasituletee uswahili kwenye BUNGE LETU, WANAFIKI WAKUBWA!!

    ReplyDelete
  22. Ndugu mbona una jazba sana nani kakuambia waliopo CHADEMA wote ni wachaga au wakristo? Zito kabwa ulimbatiza wewe kuwa mkristo? au mbunge wa Sumbawanga Mh. Said Arfi ni mkiristo huyo au hata Halima pia ni jina la kikristo? wewe ndio mbaguzi wa kutupwa kama huna cha kuchangia basi watu wasiseme ukweli kuwa CUF imekosa sifa ya kuwa mpinzani eti mnaleta ukabila na udini ndani yake? Matusi siku zote hayasaidii wala kujenga. Jipangeni upya mchukue majimbo mengi mwaka 2015 sio mbali mtaunda kambi yenu ya upinzani mnayoitaka

    ReplyDelete
  23. huyo Halima JAMES MDEE ni mkiristo,ZITO na ARFI hawatakiwi CHADEMA, ARFI na ZITO waliwekewa sumu kwenye chakula Wakiwa kwenye mkutano wa CHAMA!!!! kila siku wanaitwa ni MAMLUKI(Waislaam) Wanataka kukiua CHAMA!! HAWAFAI KUWA NDANI YA CHAMA CHA WAKATOLIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  24. NAONA KILA MTU NA NA HASA HAWA WATU WA CHADEMA KWA KWELI HAWAELEWI SIASA YA NCHI HII KWANI MWAKA 2005 MBOWE APOGOMBEA URAIS WAPINZANIA WOTE WALIKATAA KUMUUNGA MKONO KIKWETE SASA LEO NDO MKAE MANASEMA KWAMBA MBOWE NI MPINZANIA UA CHADEMA NI WAPINZANI NA WAKATI HAWANA UPINZANIA WOWOTE BALI NI TAWI LA WACHAGA LA KUENDELEZA MAISHA YAO NAOMAB TUSIKIHUKUMU CHAMA CHA CUF KWANI BILA CUF HAO MBWA CHADEMA WASINGEKUWA HAPA WALIPONA KUFANIKIWA KUPATA MAJIMBO HAYO ISHIRINI KWANI WATU WALIKUFA JANUARY ISHIRINI NA MOJA CHADEMA WALIKUWA WAPI NA MBONA HAWAKUWASEMEA NA PIA KUNA WATU HAPA COMMENT ZAO ZINALENGA KUUTKANA UISLAM NASEMA NYIE MBBWA KM HAMNA LA KUCHAMGIA BORA MKALALE MAKWAO AU MKATAFUTE MABWANA NANI ALISEMA KUWA CUF NI CHAMA CHA WAISLAM NA KATIBA GANI HIYO AU NANI ALITOA MAELEKEZO HAYO NCHII KWANZA TUMELETA UHURU WAISLAM NA SOMENI HISTORY NA KAMA KUNA MTU ANAPIBISHA KTK HILI BASI MPUMBAVU WAISLAM WALIANZA HARAKATI ZA UHURU WA NCHII KABLA NYIE MBWA HJAWA NA MAWAZO NA WAISL WALIMPA NYERERE NYUMBA YA KUISHI PALE KARIAKOO NA ALIKUJA AKAKUTA KILA KITU TAYRI LEO UNATUKANA UISLAM WAKATI SASA UNAKULA NA KUNYA KWA SABABU YA UISLAM PAKE NYIE MSIOTAKA KUSOMA MAMBO NA KUSHIKIWA AIKILI ZENU CHADEMA ACHENI UDINI NA SIASA ZA CHUKI

    ReplyDelete
  25. Hamadi Rashidi na Mamluki wenzako mnataka marupurupu tu hamna lolote bora\ CHADEMA wamewatosa. Nyie sio wapinzani ni mafisadi tu

    ReplyDelete
  26. CUF,nganagari wanajua sana kuwa wao ni sehemu ya chama tawala,basi tu wanataka tu kuwababaisha wananchi,ndo maana hata wakiandamana hawapigwi wala kufanyiwa vibaya lakini wakiandamana CDM moto unawaka,hapo ndo ujue kuwa hawa ndo hao hao wenye nchi hii.

    ReplyDelete
  27. acha jazba mchangiaji,baba yake feeman mbowe ndiye aliyeshirikiana na nyerere kuleta uhuru!! na kuhusu CDM kuungana na C.U.F hilo haliwezekani kwa kuwa C.U.F ina wabunge Waislaam Wote!!! hatutaki kunajisi kambi ya upinzani kwa kuweka waislaam wengi kiasi hicho!! Waislaam waliopo C.C.M wanatosha kwenye kambi ya chama tawala, sisi CDM tuna mipango yetu, CUF wanaweza kuivuruga!!! subirini 2015!!

    ReplyDelete
  28. ahhaaaa kumbe CHADEMA mna siri nzito dhidi ya Uislaam na Waislaam!!!!!!!!!!!!!!mnatuambia tusubiri 2015!!!!!!!!!! ddduuu!!!! ama kweli usilolijua ni kama usiku wa giza!!! jamani waislaam tuamke, CHADEMA ni wauwaji!!!!!

    ReplyDelete
  29. JAMANI MBONA MTATWANGANA MANGUMI, NIWAMBIE KITU VIJANA 2010 MMEONYESHA NJIA, 2015 MTUONGOZE TENA TUWAHI KWENYE VITUO VYA KUPIGIA KURA ENDELEENI KUTAMKA CHADEMA CHADEMA HIYO NI KAMPENI TOSHA KWA CHADEMA KUSHINDA .. PEOPLES POWER

    ReplyDelete
  30. Mimi nimekuwa mwanachama mwaminifu wa chadema tangu 1996, lakini kutokana na michango ya mawazo ya Wan-chadema wenzangu, nimeanza kuwa na wasiwasi na chama changu!! ila isiwe ni ujanja wa C.C.M kutuharibu akili zetu!!!! nitayafanyia kazi haya maoni ya wanaojiita wakereketwa wa CHADEMA!! kama yatakuwa na ukweli itabidi kufikiria mara mbili mbili kuendelea kuwa kwenye hiki chama! ila watanzania ukabila na udini ni sumu mbaya sana kwenye maendeleo na amani ya TAIFA lolote duniani!!

    ReplyDelete
  31. waislam wenzangu tutafute elimu, tusome, tuwasomeshe watoto wetu,fikra zetu bado duni,wasomi wa dini yetu wanalifahamu hilo,maada zetu ni duni,waislam waliofahamu hilo enzi hizo ndo sasa viongozi wetu mahahiri, kwani wazee wao walifahamu mapema. leo hii vijana wetu wana kazi ya kula mirungi na kushinda mabarazani na kulalama maisha magumu.... jamani tuamuke twende na wakati siyo kulalama tu

    ReplyDelete
  32. CUF msilete mambo yenu ya kipumbavu kama mmesha fungwa goli limeshaingia muhesabu moja msubiri la pili litawanyoa tu. Vumilieni kwa sababu mliyataka wenyewe. Nyinyi CUF mlishafunga ndoa na CCM, mnaishi pamoja CHADEMA haina uwezo wa kuingilia ndoa yenu. Kwa sababu mlivalishana pete bila kualika majirani na pete yenyewe mlivalishiana chumbani sio sebuleni.

    ReplyDelete
  33. kweli kazi ipo, hivi nyie cuf mfano mbowe akatangaza sasa hivi tunaungana navyamavingine vya upinzani afu ikatokea kunaisue imetokea zenj kambiyaupinzani wanaona haikosawa wanataka kupinga je cuf mtajipinga wenyewe au mtaisaliti kambi yenuuuuuuuu??????????? swala lanyie kujiunga na ccm zenj sio baya coz mliokoa jahazi but kamamnataka kweli tuamini mlifanya kwa maslah ya taifa basi mkubali kuwa hamuwazi kujiunga kambi ya upinza coz ikitokea isue ya zenj itabidi muwasaliti wa zanzibar kwakushindwa kusimamia haki mkae upande wa serikali (namaanisha mtawasaliti wapinzani wenzenu watakaokuwa wanatetea maslah ya wanzanzibar) mie naona nyie shirikianeni na wenzenu mkiwa nje yakambi kama chadema walivyo wasihi kuwa na umoja kati ya wapinzani. ila msibebe uwaziri kivuli ambao sikumoja utawatokea puani, au nipeni siri kwani kuwa kambi ya upinzani ndoutakuwa peponi? kwani kama hauko kambi ya upinzani hoja zako hazisikiki? Mnawasingizia eti chadema hawataki ushirikiano na wapinzani wakati mwanzoni waliwaita mkakataa???????????? napia kama hawataki ushirikiano na wapinzani mbona wamemuunga mkono mkkafulila wa NCCR katika hoja yake binafsi ya dowans? tatizo nyie mliwatenga wakati wachaguz ndogo bungen mkawa upande wa ccm ndomana wanakuwa na wasiwasi na nyie, samahanini sana kama nyei hajayenu ni madaraka tu na si kumkomboa mtanzania maskini tuachieni chadema wetu mtetezi wa wanyonge oneni mikoa waliyo pita kwakishindo wanavyo fanya mabadiliko!!!!!!! kwahili sidanganyiki tafuteni lingine ukitakakujua wako fit wanakubalika mijini na kwawasomi idi nahiv vijijini nakowameanza kubadilika, isue si kambi ya upinzani tunaangalia maslah ya nnchi

    ReplyDelete
  34. HE He!!!!!!!!!!!!!!! tena muishie hapo hapo, kama hii webu imeingiliwa na mafisadi ili waisambaratishe chadema mkome kama mlivyokoma kunyonya ziwa la mamae! mnasema waisilamu tuwe macho kwani nikiongozi yupi wa chadema aliyewahi kuwatenga waisilamu au kutangaza udini! hata Dr slaa tuhuma anazobebeshwa siye yeye kafanya ila wanadai maaskofu ndo walikuwa wana mnadi kwani yeye aliwaomba!!!!!!!! kama maaskofu nao walimpenda kamasiye tunavyo mpenda coz wanahisi ndiye atakaye komboa hili taifa wakaanzakumpigia kampeni chadema walaumiwa kwakupendwa!!!!!!! kwani kosa lao nikuwa namvuto mioyoni kwa jamii nzima!!!!!!!!!! mbona kikwete nae masheh walimnadi msikitini wakidai nichaguo la Mungu!!!!!!!! samahani sana wengi humu nasi ni waisilamu ilatuna ipenda chadema coz sera zake zina tija hivyo huyo anaye sema waisilamu tuwe macho akome. kama chadema wanaudini mbona kwenye mazishi ya Arusha watuwote walizikwa kwaheshima tena viongoza wachadema wakaubeba mwili wa muhislam kwaheshima zote! hizo hoja za udi hazipo kawadanganye vijijini na ambao hawajasoma ila waislamu wote wasomi wanawaunga mkona chadema kama huamini kafanye sensa vyuoni. kwataarifa yenu hamtoingangusha chadema kwa udin labda mutueleze tuuma ya ufisadi juu yao au mja na sera za kawafunika, ila kwamajungu haya mnazidi kijidhoofisha

    Amina Juma

    ReplyDelete
  35. Does CUF want to be polygamous?
    It has married CCM in Zanzibar and now wants to marry CHADEMA in mainland! by force? No, let her do not. Let her marry CCM mainland instead.

    ReplyDelete
  36. Udini na ukabila tu ndo umetawala katika hoja zote hizi! Watu mmekosa hoja ya utaifa mmebakia na Udini na ukabila!

    Mtu mwenye mawazo hujadili hoja na kuitafutia ufumbuzi lakini wengi wa hapa wachangiaji wamejadili mtu na kikundi cha watu. Hii haina tija kwa taifa. Na mjadala wenu heri muuze laptop zenu maana hazisaidii Taifa.

    Mjadili CHADEMA wameshakataa kujiunga na Vyama vyote vya Upinzani sasa what next?! Vyama hivi viweje Bungeni, tuunde kanuni kuviweka vifanye kazi ya kiliberali au la! Hizi ndiyo hoja ili kila chama kitimize wajibu wake kama ilivyokusudiwa.

    Udhaifu gani umepelekea tufike hapa mpaka CUF kukataliwa na CHADEMA kwa kukubali kuunda serikali ya umoja wa kitaifa! Nini kifanyike pindi hali kama hiyo itajitokeza hapa Tanzania Bara, kuna faida yeyote CHADEMA inapata kwa kuitenga CUF? CHADEMA inahofia nini zaidi nyuma ya hoja yao ya ndoa ya CUF na CCM nk ndiyo maswali ya kuhoji na kuyapatia ufumbuzi. Kwa sababu sisi ni Taifa changa sana kidemokrasia si kama Ujerumani na Uingereza ambao vyama viwili vinaweza kuunda serikali. Nini kifanyike ili tuwe kama wenzetu waliokomaa kisiasa nk. Hizi hoja hazihitaji elimu kubwa kutambuwa. Siasa za vijiweni na ushabiki wa Simba na Yanga haziwezi ku apply kwenye masuala nyeti na tata ya Kitaifa. Kinyume chake watu hatujadili haya. Hivi hatujuwi wewe na mimi tunatakiwa kuiacha nchi salama kwa maslahi ya watoto ambao leo wapo chekechea, shule za msingi na wengine hawajazaliwa?

    Kwa mantiki hii, natoa hoja kwa Mhariri wa gazeti la Majira wale woote wanaoonekana kuchochea chuki, udini, ukabila, utengano, mshikamano na umoja wa Taifa letu maoni yao yasiwekwe kwenye tovuti hii.

    Tunataka maoni yatakayotujenga Watanzania bila ushabiki wa chama ama itikadi yeyote!

    By Carwin

    ReplyDelete
  37. Mtoa maoni hapo juu tafakari haya.

    Hapa watu wana-react (samahani nimekosa neno kiswahili) kutokana na hoja/majibu ya wanasiasa wetu wanapojibu hoja za wenzao.

    Soma kichwa cha habari hii. Tunashangazwa na wanasiasa wanapoibuka kwa jaziba kutoa hoja za wenzao badala ya kujieleza hata kwa busara taratibu. Utafikiri ni wanamipasho!

    Maoni kama haya yawafikie na wajue kuwa wao ndio wanaochochea matusi na mambo mengine unayoyaona kwenye maoni ya wengi.

    Kama kuna hoja ya kitaifa, waandishi wa habari pia walaumiwe. wanatuletea habari za kimipasho na ushabiki badala ya hoja.

    Andikeni habari za uchunguzi na upembuzi. Acheni kutuletea mipasho. Kama mtu alililia kitu fulani, jaribu kuandika kama mpembuzi wa kile kinacholiliwa na si kutuletea hisia za mtu.

    Ukisoma habari nyingi humu, utagundua kuwa sehemu kubwa ya mjadala huwa ni ama hisia za watu au mambo yao badala ya hoja ya kitaifa.

    Kwa hiyo watoa maoni wanachangia kufuatana na habari ilivyowakilishwa.

    ReplyDelete
  38. Hapa hatuhitaji kila mtu kuvutia kwake! Watanzania tubadilike katika kuangalia na kutoa maamuzi kwa viongozi wa siasa na vyama vyao! Tunacho hitaji ni utendaji wa kila mtu na nafasi yake! tuwatetee watu na pia kuwachagu kutokana na uwezo wao wa kuongoza na kuchochea maendeleo ya watz! Maswala ya Udini hayana nafasi! Watu wamesema CHADEMA ni vigeugeu! mi nadhani si kweli kwani kiongozi yeyote makini lazima awe flexible kwakuangalia njia salama za kumfikisha kwenye mafanikio. B4, hawakuwakubali NCCR,UDP,TLP... kutokana na kuonekana kutokua serious we all know that kua nikweli! upande wa CUF ni vizuri wameungana na CCM kwa Z'bar kwani wameleta amani huko,huoni kua nao lazima wamebadilika? nia yao ilikua nikuchua dola kamili! ila imewapasa kuungana kwaajili ya amani(moja ya sababu!).b4 kuungana na Serikali walikua na nguvu ya kiupinzani! Kwa akili ya kawaida tunategemea upinzani wao leo utakua kama wa zamani? ingekua hivyo kwenye chaguzi za juzi za speakers basi wange waunga mkono CHADEMA!

    ReplyDelete
  39. Nimeupenda saaana mwangaza uliotolewa na gazeti la East African kuhusu DOWANS kupitia mtandao na kuwekwa bayana na mchangiaji. Sasa KIKWETE unasubiri nini kukiri maana nafahamu kuwa unajua ukweli huu utakuumbua siku chache za usoni??? Mjinga Salva Rweyemamu (Msemaji wa Ikulu)pinga ukweli huo basi kama ulivyoainishwa hapo maana umezoea kukanusha in favour of the damn President. PCCB mko wapi kwa sasa?? Kanusheni ukweli huo tuwaone kama nyie ni wajanja!!! You are really stupid!! Yaani kamati ya Mwakyembe ilithibitisha kampuni kuwa hewa kwa kutumia millioni za watanzania bure?? Mwakyembe ulitusaidia, lakini sasa utaumbuka!! (Kumbuka yale uliyoyaficha ili kutokuiathiri serikali ......). Sasa yanaanza kubainika moja baada ya jingine. Je, Una/ Uliiheshimu taaluma yako lakini??? Mnawazidishia watanzania hasira tu ya kuwatoa madarakani kwa nguvu. Tunisia, Misri, Jordan na Yemen ni nchi na si visiwa. Wanaumia sasa. Tanzania haiwezi kukwepa kikombe hiki. Moto umeanza sasa Africa!!! Rostam, siku zako zinahesabika duniani. Utakufa kifo cha ajabu sana FISI WEEE!! Maana huna haya. Halafu unasikitisha kwa jambo moja; Huwa hukumbuki maneno unayoyasema. Maana unatuambia kuwa wewe unafanikisha kuwaleta wawekezaji!! Kashfa lukuki!! Sasa kanusha hili ambalo liko katika mtandao dunia nzima. Shame on you!!! Nasema hiviiiiii Kikwete na serikali yako, mnamuogopa Rostam kwanini; anawalala??? au?? Kumbuka kisa cha Nyerere na yule Mgiriki aliyejinadi kuwa nchi yote aliiweka mfukoni mwake. Siku si nyingi, Mtakiona cha mtema kuni. Nyambafuuuuu!!!

    ReplyDelete
  40. Ugalatia wa Chadema !
    udini ndio unaowatafuna CHADEMA ukweli chadema inaowaogopa waislamu huu ndio ukweli tumeona kina Zitto Kabwe misuko suko wanayoipata Chadema kw asababu ya dini yao huu ndio ukweli na CUF ina viongozi wengi waislamu kuwaingiza kwenye ushirikiano na Chadema vongozi wa kanisa hawatarohusu hili milele na kanisa litawakana Chadema huu ndio ukweli.
    Ikiwa Chadema kweli ina intrest ya kuleta mabadiliko Tanzania wakati uchaguzi tu Tindu Lisu alisema hawakubali mabadiliko ya katiba ya Zanzibar sasa watu wamepiga kura kuamua muundo wa seriklai wanayoitaka ina maana Chadema ingekua ni chama Tawala Zanzibar ingekataa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na kuipinga katiba ya Zanzibar?

    Chadema inahitaji viongozi imara kama BOB MAKANI na MTEI sio Viongozi waliopata udhaifu wa Kikwete kwenye CCM kuamini wao ni viongozi zaidi Tanzania nikiwa Mtanzania naamini Chadema haijawa tayari kuweza kuongoza wacha ijifundishe kwenye Municipalities tuone uwezo wao kwani hata policy zao Chadema haziko clear huu ndiio ukweli.

    ReplyDelete
  41. peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeesssssssssssss?


    poweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeerrrrrrrrrrrrr

    ReplyDelete
  42. cuf msihofu kwani kuwa huko kwenye kambi ndio nini? UMOJA WA KITAIFA KWETU NI BORA KULIKO HILO. KINGINE CUF TULIJITAKIA WENYEWE KUWAKUMBATIA HAWA UCHAGUZI WA 2005 WAKAPATA ADVANTAGE,HAWA WANAAMRISHWA NA KANISA NANI WA KUSHIRIKIANA NAYE. SABABU ZOTE WALIZOTOA HAZINA MSINGI.SISI WANANCHI TUMEICHAGUA CUF ITUWAKILISHE BUNGENI HAMJACHAGULIWA NA MBOWE NA SLAA

    ReplyDelete
  43. CUF ambao mumeungana na CCM (zanzibar) mtawezaje kuwa kwenye upinzani rasmi (CHADEMA) ilhali pale wapinzani rasmi (CHADEMA) walipotoka nje ya bunge wakati Rais Kikwete (CCM) anahutubia, kupinga matokeo ya urais miluwazomea (CHADEMA) na kwenda kukaa kwenye viti vyao mkiongozwa na Hamad Rashid? Wabunge (CUF+CCM) wakerekwetwa wakabaki kumshangilia Kikwete akihutubia. Je bado tu hamjaelewa (CUF) mlipoangukia au ndio zile tunazoita ghilba ili watu wawaamini?

    ReplyDelete