LONDON, Uingereza
CHELSEA imeweza kuanza kunusa muujiza wa kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu.Siku nane zilizopita walikwua wamzidiwa kwa pointi 15 na vinara wa
ligi hiyo, Manchester United.
Lakini juzi usiku walicheza mechi na kushinda mabao 3-1 dhidi ya Blackpool, ambapo kwa mara nyingine tena Fernando Torres hakufunga, sasa tofauti ya pointi imekuwa ni tisa.
Mfungaji wa mabao mawili ya Chelsea, Frank Lampard alisema: "Tunatakiwa kuamini kuwa tunaweza kufanya, ingawa bado kuna kazi kubwa. Tunatakiwa kujipatia wenyewe changamoto.
"Timu zilizopo juu bado kuna tofauti kubwa ya pointi, lakini ni nzuri kuangalia juu kuliko kupigania katika nafasi nne za juu. Kama tutashinda kila mechi tunaweza kuwa na nafasi kubwa. Lakini itakuwa ngumu sana."
Haitakuwa ngumu sana kama Chelsea, inaweza kushinda mechi zake zilizosalia ikiwemo ya Old Trafford itakayochezwa Mei 7, mwaka huu.
Kocha wa Blues, Carlo Ancelotti alishuhudia timu yake ikipata pointi tatu, baada ya
John Terry kufunga kwa kichwa, Lampard alifunga kwa penalti na kisha tena alifunga bao la tatu kwa kuunganisha pasi nzuri ya Salomon Kalou.
Alisema Chelsea, inaweza kuendelea kupigania ubingwa wake: "Tuko nyuma kwa pointi tisa na pengine ni mbali sana kufiria kuwa tunaweza kupigania ubingwa.
"Ni vyema kwetu kwenda mechi moja baada ya nyingine. Hiyo italeta urahisi kwetu. Lakini ninafikiri kuwa tuko katika wakati mgumu."
Kocha huyo alizidi kumtetea mshambuliaji wake mpya aliyesaini kwa ada ya pauni milioni 50, Torres ambaye juzi alicheza mechi ya tano lakini hakufunga goli.
Alisema Ancelotti: "ninamfuarahia."
Mchezaji Jason Puncheon, ndiye aliifungia bao pekee la kufutia machozi Blackpool.
Kocha Ian Holloway alisema: "Sasa tuna mechi tisa katika msimu kujaribu kujinusuru wenyewe katika ligi ngumu.
"Kama wewe ni Daud, unakutana na Goliath, unatakiwa kupimpiga jiwe usoni na hatoweza kufanya hilo dhidi ya Chelsea.
No comments:
Post a Comment