09 March 2011

Toure agusiwa adhabu yake

LONDON, Uingereza

KOLO Toure amegusiwa kuhusu adhabu anayoweza kupewa, baada ya kubainika kuwa alitumia dawa za kulevya.Mchezaji wa York City Knights, Matty Duckworth alifungiwa
 miezi sita kutokana na kuvunja sheria hiyo ya kutumia dawa za kulevya.
Duckworth alikuwa apewe adhabu ya kufungiwa miaka miwili, baada ya kupimwa na kukutwa ametumia dawa kutokana na kumeza dawa Methylhexaneamine (MHA), ambazo anaamini alimeza kisheria.
Lakini Duckworth, mwenye miaka 21, alikata rufani  kutaka kujua kama ilikuwa ni halali kusambazwa kwa dawa hizo, alizopata kwa Jack, na kwamba alisema hakumeza ili kuongeza nguvu katika uchezaji wake.
Adhabu yake ya kufungiwa ilianza Septemba Mosi mwaka jana hadi  Machi Mosi, ikiwa ni miezi sita.
Mchezaji wa Manchester City, Toure alipimwa na kuonekana kuwa na chembe za dawa za kulevya baada ya kumeza vidonge vya mkewe kwa jili ya kutibu tatizo la unene, haionekani kama anaweza kufungiwa miezi sita kama hakupata ushauri kutoka kwa wataalamu.

No comments:

Post a Comment