25 February 2011

Kaseba amdhihaki Francis Cheka

Na Amina Athumani

BINGWA wa Dunia wa mchezo wa ngumi na mateke (Kicboxing), Japheth Kaseba amemdhihaki Francis Cheka kwamba hamtishi kwa kuwa hana kiwango cha
kutisha, kwani anaitwa bingwa kwa sababu majaji waliamua hivyo.

Kaseba anatarajia kupanda ulingoni machi 16, mwaka huu dhidi ya Mada Maugo ambapo mshindi kati yao ataandaliwa pambano maalumu dhidi ya Cheka ambaye ni bingwa wa uzito wa kati nchini baadaye mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kaseba alisema hapigani na Maugo kwa ajili ya kuzichapa na Cheka, isipokuwa anacheza kama sehemu ya mchezo kuwapa raha mashabiki wake.

"Cheka anastahili kuitwa bingwa kutokana na maamuzi ya majaji tu, kwa sababu siku zote majaji wanaubeba mchezo, lakini ukiangalia kiwango na uwezo wake ni ule ule sioni kama kuna sababu ya kumwogopa namchukulia kama mabondia wengine," alisema Kaseba.

Akizungumzia pambano la awali dhidi ya Cheka lililopigwa mwaka jana, Kaseba alisema kilichomwangusha ni kukosa maandalizi, lakini kwa sasa anajianda vya kutosha.

Kuhusu pambano dhidi ya Maugo, alisema litakuwa rahisi kwake kwa kile alichodai kuwa anamfahamu vizuri mpinzani wake na kwamba hiyo ni sehemu ya maandalizi tu ya micheyo mingine.

1 comment:

  1. Huyu KASEBA asifikiri ngumi (Boxing) ni sawa na KICKBOXING. Kama mchezaji lazima akubaliane na uwezo wake na wamwenzake, kwani michezo si ushabiki, pamoja na kupata kipato, pia tunapata burudani, marafiki, umoja na kujijenga kimwili (afya). Huyu KASEBA alipigwa kwa KNOCK OUT kabisa, na hakuwa na uwezo hata wakusimama na kujitetea. Alafu leo analazimisha majaji walimpendelea CHEKA, je angeshindwa kwa point? Kwanza inabidi amuombe radhi CHEKA kwa shabiki wake kumpiga vibaya siku ile alivyopigwa ulingoni. Tunakuomba KASEBA usipoteze heshima za BOXING Tanzania na usitutie hasira na maneno yako machafu.

    ReplyDelete