25 February 2011

'Airtel Flava' yazinduliwa Dar

Na Mwali Ibrahim

KAMPUNI ya simu ya Airtel, jana imezindua huduma ya 'Airtel Flava' inayotoa huduma ya burudani ya muziki kwa njia ya simu.Akizungumza Dar es Salaam jana
, Meneja Masoko wa kampuni hiyo Kelvin Twissa, alisema hudumu hiyo ina muwezesha mtumiaji wa simu kuweza kuchagua wimbo wa kuusikiliza kulingana na hisia zake.

Alisema licha ya kuchagua wimbo wa kusikiliza, pia anaweza kuchagua wimbo na kuweza kutumia wakati wowote, ikiwa ni pamoja na kuutuma kwa watu wengine kadri anavyopenda.

Twissa alisema, ili kuweza kupata wimbo huo mteja wa Airtel atatakiwa kupiga simu namba 15565 na kuweza kuchagua wimbo wa kuusikiliza na hatimaye kuhamishia katika simu yake na kuusikiliza wakati wowote.

"Bila ya kujali aina ya wimbo unaoupenda kuchangamka nao, iwe wa kisasa au wa kizamani kwa hakika kila mtu atapata kile akipendacho kulingana na anachokichagua," alisema Twissa.

No comments:

Post a Comment